Siasa za Olimpiki: Tunapeleka washiriki wangapi?

Valencia_UPV

JF-Expert Member
Mar 31, 2016
6,215
7,381
Ndugu zetu Kenya wamepeleka wanamichezo 93 sisi hapa tunapeleka watalii wangapi Olimpiki Japan? Au ndo bado tunachakata majina kupitia kamati kuu ya Olimpiki?

images (35).jpeg

IMG-20210727-WA0052.jpg
 
Nchi ambayo viongozi wake wanawaza kujipendekeza kwa Rais, viongozi waliokoswa ubunifu....hawana jipya

Wanachowaza ni kupambana na upinzani tu
 
Kila mshiriki anayeenda Olympic lazima awe amequalify kwa kufikisha vigezo vya kushiriki..sio kila mwanamichezo anaweza kwenda kushiriki.kwa Tanzania waliofuzu Ni watatu na wote Ni wanariadha...mfano kwa riadha fully marathon lazima uwe umekimbia kwenye mashindani ya yanayotambulika chini ya saa 2 dk 11 (2:11) ndio sifa kushiriki. Simbu na mwenzie wamefikia huko ,ndio maana wamequlify.....tatizo linakuja kwa miaka yote hiyo kweli kamati ya Olympic Tanzania na vyama vya michezo zimeshindwa kuandaa wanamichezo wakutosha wa riadha na ngumi etc wakaqulify? Kuna uzembe mahali.

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Kuna mwaka ninakumbuka Tanzania ilipanga kupeleka wanamichezo 9 kwenye mashindano ya Jumuiya ya madola, lakini wakapelekwa 6 tu (wengine watatu wakaachwa kwa sababu ya taifa kushindwa kuwalipia nauli na gharama zingine), lakini msafara uliokwenda kwenye mashindano hayo ulikuwa na jumla ya watu 20, kati hao washiriki (wanamichezo) walikuwa 6 tu na watu wengine 14 waliobakia walikuwa ni maafisa na viongozi waliokuwa wanasindikiza washiriki.
 
Safi sana
 
Tanzania is not a sporting country. The government can only repress the dissenters but not investing in sport. They always send a bunch of tourists to such sporting events because the government never invest in sport.
 
Hii nchi ina Mawaziri Wapumbavu na Watendaji Wapumbavu. Waziri wa Utalii, Waziri wa Michezo na Waziri wa Mambo ya nje wote hovyo kabisa. Wenzetu wametumia hapo kujitangaza sisi Bendera imebebwa na Mjapan ni aibu kubwa
ingekuwa nchi nyingine makini hao mawaziri wangeshikiwa bango mpaka wakajiuzulu halafu waandishi wetu takataka badala ya kuhoji vitu vya msingi wanahangaika na umbeya
 
Kila mshiriki anayeenda Olympic lazima awe amequalify kwa kufikisha vigezo vya kushiriki..sio kila mwanamichezo anaweza kwenda kushiriki.kwa Tanzania waliofuzu Ni watatu na wote Ni wanariadha...mfano kwa riadha fully marathon lazima uwe umekimbia kwenye mashindani ya yanayotambulika chini ya saa 2 dk 11 (2:11) ndio sifa kushiriki. Simbu na mwenzie wamefikia huko ,ndio maana wamequlify.....tatizo linakuja kwa miaka yote hiyo kweli kamati ya Olympic Tanzania na vyama vya michezo zimeshindwa kuandaa wanamichezo wakutosha wa riadha na ngumi etc wakaqulify? Kuna uzembe mahali.

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
unakuta kila mwaka viongozi ni haohao kina Bayi hamna chochote cha maana wakati wao waliibuliwa wakiwa vijijini leo wanatafuta wakimbiaji mijini
 
Ukitaka nchi yenye makabila mengi na dini tofauti kama Tanzania iendelee ni lazima uwe na Demokrasia na Uhuru na Haki za binadamu na utawala bora.

Vinginevyo utumie Kabila moja au mawili makubwa au dini moja kubwa kugandamiza wengine kwa kiwango cha kuwatia hofu mpaka wenywee na kuufyata mkia.

Tanzania Kwenye soka bado hatujawekeza vya kutosha kwa sababu watu hawapo huru kutumia vipaji vyao kujitafutia maslahi makubwa ndani na nje ya nchi kutokana na kukosekana kwa uraia pacha.

Marathoni hatujawaandaa watu wa Ukanda wa Kati na Kaskazini kutokana na kujaribu kuwazibiti badala ya kutumia vipaji vyao kuendeleza Taifa.
Ni wazi kuwa Kwenye Mbia za Marathoni Wa Makabila ya Wameru, Wairaq ,Warangi,Wanyaturu ,Wasonjo, Wabarbeig na Wamasai ndio wanaotisha kwa Kukimbia.
Hawa walipaswa watumiwe vizuri sana na uwekezaji wenye tija kwa vijana wenye vipaji. Leo tungewapita Kenya kwa Mabali sana na Ethiopia mana Sisi Tuna Makabila Mengi zaidi.

Lakini kutokana na Katiba inayotoa Mwanya wa Upendeleo, Ukabila na Udini basi Kila anayeingia madarakani anawaza kupendelea watu wa Kabila au dini yake na kupuuza maeneo mengine kwa kusema wale wasubiri mana sasa ni zamu Yetu.

Tutachelewa sana kwa Katiba hii ya Wakoloni weusi inayolinda Genge la watu wachache na familia zao chini ya Mwavuli wa Chama cha CCM badala ya kulinda maslahi ya Taifa na Mama Tanzania.

Sent from my TECNO L8 Lite using JamiiForums mobile app
 
Kuna mwaka ninakumbuka Tanzania ilipanga kupeleka wanamichezo 9 kwenye mashindano ya Jumuiya ya madola, lakini wakapelekwa 6 tu (wengine watatu wakaachwa kwa sababu ya taifa kushindwa kuwalipia nauli na gharama zingine), lakini msafara uliokwenda kwenye mashindano hayo ulikuwa na jumla ya watu 20, kati hao washiriki (wanamichezo) walikuwa 6 tu na watu wengine 14 waliobakia walikuwa ni maafisa na viongozi waliokuwa wanasindikiza washiriki.
Ccm wameiharibu sana hii nchi.
 
Back
Top Bottom