Chama cha riadha (AT), kamati ya olimpiki (TOC) na CCM tafadhali someni huu uzi

MamaSamia2025

JF-Expert Member
Mar 29, 2012
13,642
30,444
Baada ya comments zangu kadhaa mitandaoni kuhusu michezo ya olimpiki nimepokea messages nyingi sana zikinisihi niandike uzi kuhusu mchezo wa riadha na nini kifanyike ili twende mbele. Baada ya tafakuri ya kina nimeona niandike huu uzi kwa maslahi mapana ya taifa. Kama kawaida maoni yangu kuhusu riadha ndo utakuwa msimamo wa JF. Haipingwi. AT, TOC na chama pendwa CCM vumilieni spana za hapa na pale kwenye huu uzi. Nia ni nzuri kwa taifa.

Kwanza kabisa kwa wale wasiojua ni kuwa riadha sio kukimbia tu. Kuna kurusha mkuki, tufe, kisahani, long jump, high jump nk. Tembelea www.worldathletics.org uone michezo yote inayohusu riadha. Kwahiyo kama taifa lingekuwa serious tungepeleka kwenye olimpiki wachezaji wa michezo mingi inayohusu riadha. Kwenye kukua kwangu nadhani kama sikosei hayati John Bayo ndo mtanzania niliyewahi kusikia alishiriki mashindano ya kimataifa ya kurusha tufe. Lakini miaka yote imekuwa ni mbio ndefu tu wanaoenda kutokea Tanzania. Kwanini inakuwa hivi? Jibu utalipata kwenye spana nitakazowapiga AT, TOC na CCM.

Chama cha Riadha Tanzania (RT)

Hiki chama ni miongoni mwa taasisi zilizofeli Tanzania. Kunahitajika mapinduzi makubwa kwenye hiki chama ili kupata mafanikio kwenye riadha. Viongozi waliopo hawawezi kuleta matokeo yoyote chanya. Kama miaka ya nyuma wanariadha walikuwa wanatokea kwenye mashindano ya UMITASHUMTA na kwenda kukichafua kwenye World Junior Championship inashindikanaje leo hii ambapo kuna utitiri wa marathon zenye ufadhili mnono wa makampuni kama CRDB? John Yuda alikuwa fundi gereji mwaka 2000 ambapo aliacha kazi gereji na kuanza mazoezi kidogo kisha kwenda kushika nafasi ya pili mbio za nyika mwaka 2001. Fabian Joseph mwaka 2002 alikuwa mwanafunzi akishiriki UMITASHUMTA ila mwaka uliofuatia akawa staa mkubwa duniani. Ikumbukwe enzi hizo hakukuwa na makampuni makubwa ya kitanzania yanayofadhili riadha. Zilikuwa ni jitihada binafsi za watanzania wenzetu waliokuwa wakikuza vipaji vya vijana kwa kutumia hela zao binafsi. Mungu atawaadhibu RT kwa hii hujuma mnayoifanyia nchi. Inaonekana hakuna mipango yoyote ya dhati kukuza vipaji vilivyozagaa nchi nzima.

Pia RT ina watu wenye roho mbaya ambao wako tayari kukwamisha jitihada za wadau wanaotaka kukuza riadha. Mfano hai upo.Miaka iliyopita kulikuwa na charity organisation ya Shoe4Africa iliyokuwa inasapoti sana riadha ila cha kushangaza ile taasisi ilipotea nchini na kwenda kuwekeza zaidi Kenya. Huko Kenya taasisi inapata ushirikiano wa kutosha kiasi kwamba imeenda mbali sana hadi kufanikiwa kujenga hospitali ya kisasa na kusaidia mambo mengi ya michezo, elimu na afya. Tembelea www.shoe4africa.org uone wakenya wanavyonufaika. Kwa hapa Tanzania hawa shoe4africa walisaidia hata kina Simbu kwenye vifaa vya michezo. Baada ya kuondoka shoe4africa sijawahi kusikia RT ikishirikiana na taasisi nyingine kama hiyo.

Nina mengi ya kuandika ila itoshe kusema RT mmefeli kukuza vipaji. Mjiulize hawa kina Simbu wakistaafu hali itakuwaje?

Kamati ya Olimpiki (TOC)

TOC hauwezi kuepuka lawama. Hii kamati imejaa watu wabinafsi wanaojali maslahi yao tu. Ni kamati iliyokosa kabisa ushawishi. Katibu mkuu wa kamati ya olimpiki anamiliki world class sports complex huku nchi yake ikiwa haina kitu kama hicho. Kama sio ubinafsi ni nini? Hii kamati ina viongozi waliodumu madarakani kuliko mwenyekiti wa CHADEMA. Ni kamati ambayo haina cha kujivunia kwenye olimpiki tangu kuanzishwa kwake. RT na TOC ni kama mkusanyiko wa watu wa familia moja. Kujuana kwingi mno. Mara nyingi mtu akitoka RT au TOC basi huingia kwenye siasa. TOC pia imefeli kutengeneza vipaji vipya. Ni kamati inayolalamikiwa kwa miaka mingi kuhusu matumizi ya fedha.

Chama Cha Mapinduzi (CCM)

Hiki chama kilichobeba matumaini ya watanzania wote akiwemo Mbowe na genge lake nacho hakiwezi kukwepa lawama. CCM imeshindwaje kuboresha viwanja wake na kuwa na hadhi ya olimpiki? Uwanja kama Sheikh Amri Abeid, Arusha unakosaje Tartan Floor kwa ajili ya riadha? Hata Basketball court hazina hadhi ya olimpiki. Hatuwezi kupata wanariadha wenye viwango kwa kufanya mazoezi kwenye viwanja duni. Wanaohusika ndani ya CCM wachukue hatua ya kuboresha hivi viwanja.
 
Msingi wa kupeleka wanashiriki wa michezo ya riadha kama unavoita au inavoitwa kwa kingereza " track and Field" ni qualifications...wote unaoona wameshiriki ni kwasababu wameqaulify katika mashindano mengine makubwa.

Hapo ndio msingi wa tatizo kwanza ni kuwekeza wanariadha wengi wapate nafasi ya kuqualify , who sponser Hawa watu waende kutafuta hizo nafasi za kuqualify, Je tuna wakufunzi wazuri wa kutengeneza Hawa washiriki? Mimi naamini mikoani Kuna vijana Wana uwezo mkubwa sanaaaaaa.

Titizo lingine kubwa ni Hawa viongozi wa riadha kila mtu ana vijana wake inapotokea opportunity yeyote ya kwenda nje kushiriki mashindano hiyo ni vita kubwa sana maana kila mtu anataka kijana wake aende...matokeo yake tunapeleka watu ambao hawaqualify..wale wazee pale RT wanaangalia sana pesa.
 
Baada ya comments zangu kadhaa mitandaoni kuhusu michezo ya olimpiki nimepokea messages nyingi sana zikinisihi niandike uzi kuhusu mchezo wa riadha na nini kifanyike ili twende mbele...
Umeenda vizuri,ila kumtaja Mbowe ndo umechemka!
 
Tanzania tunakosa medali yaani
Hata shaba

Ova
Mzee wa Kino ogopa katibu mkuu wa TOC anamiliki world class sports complex huko Kibaha ambapo mashindano ya kimataifa hufanyikia na yeye kulipwa chake. Mzee Bayi ni wale wazee wa mjini kwelikweli.
 
Mzee wa Kino ogopa katibu mkuu wa TOC anamiliki world class sports complex huko Kibaha ambapo mashindano ya kimataifa hufanyikia na yeye kulipwa chake. Mzee Bayi ni wale wazee wa mjini kwelikweli.
Huyo mzee bayi ndiyo kikwazo mwenyewe

Ova
 
Back
Top Bottom