Siasa za mishahara minono kwenye taasisi za Serikali zinavyoharibu ndoto za vijana wengi wa Kitanzania

Maisha bila janja janja,akili yakujiongeza mambo hayaendi

Ova
 
Hata kama sina ninachojua lakini kwanini nafanya kazi hapa na wewe kwanini upo huko Unalia lia

Kila mtu na bahati yake pia, Wewe huna bahati ya kuhama

Ungekuwa na bahati ungehama, Nyota yako ina giza giza na ukungu kwa mbali ndio maana upo hapo ulipo

Na kwa kulia lia huko utaendelea kuwepo hapo kila siku

Nakushauri njoo PM nikupe ushauri, Kuna mambo lazima upewe connection na usaidiwe kwenye Maisha haya

Ukiwa unashupaza shingo na kusema mbona Wengine wamefeli nawafahamu lakini wapo hapo kuna mambo mengi nyuma ya Pazia

Kuna baadhi ya kazi watu wanapewa nafasi kutokana na Reputational au heshima mzazi aliyoweka kwenye taasisi hiyo, Hivyo moja kwa moja ni rahisi kuamini hata akiharibu tutampata wapi?

Mimi nilitegemea mtu ungeniuliza kwanini watu Wengine wapo huko na waliingia vipi na hawana vigezo na waliingiaje huko?

Je, hao wanafanyaje? Ningeweza kukueleza hata PM sio hapa jukwaani.

Kuna uzi hapa ulikuwa unaeleza mambo ya wakinga na utajiri wao, Kuna member baada ya kusoma Jibu langu alikuja PM tukaongea mengi

Huyu Member anaweza toa ushahidi hapa

Jifunze kujifunza vitu na watu ndio connection yako,
Umeeleza kitaalamu sana
 
Wanabodi, vijana badala ya kufikiria maarifa ili waweze kuendeleza wapatacho wao wanawaza mishahara minono kwenye taasisi za kiserikali ambazo Kiuhalisia mishahara hiyo minono haipo kwa vijana wanaoanza kazi.

Maneno ya wanasiasa majukwaani kutamka mishahara ya wakurugenzi(Directors) wa mashirika hadharani kama NSSF, PSSF, NHC, TANAPA, TRA na baadhi ya Private commercial Bank imepelekea vijana kuhisi huko ndio kuna pesa na mishahara minono.

Vijana lazima watambue sio rahisi kufika kwenye nafasi ya ukurugenzi haraka haraka na kufikia kiwango cha mshahara unaotamkwa na wanasiasa jukwaani.

Kama hiyo mishahara ni mikubwa kiasi hicho kwanini wao wanasiasa wameacha kazi kwenye hayo mashirika na kukimbilia kugombea Ubunge?

Vijana wanapokosa mshahara waliousikia toka kwa wanasiasa wanapoajiriwa na taasisi hizo hujiingiza kwenye mambo ya rushwa, uwizi na ubadhirifu wa Mali za uma.

Ndoto nyingi za vijana zimevunjika na kufa na Wengine kuishia jela kabisa baada ya kujihusisha na vitendo vya uwizi na ubadhirifu wa Mali za taasisi baada ya kukosa mishahara walioisikia toka mdomoni mwa wanasiasa.

Hakuna mshahara mkubwa au mdogo hata siku moja, cha muhimu ni bajeti.

Bajeti ndio msingi kwa mfanyakazi kama ilivyo kwa sisi wakinga malengo ndio msingi wa biashara yako.

Nashauri vijana hizo taasisi zina malipo ya pesa za Kawaida kukuwezesha kuishi na kukopa pesa kwenye Saccos au Bank pamoja na mikopo ya magari.

Hizo taasisi za Serikali watu wanaacha kazi kila siku kufuata maslahi sekta binafsi.

Kwa mfano:
Kuna watu wanalipwa laki 5,Lakini mwisho wa mwezi anakopwa na mtu anayelipwa million 8. Tatizo hapa ni Bajeti kwa mtu wa Milioni 8.

Wanasiasa ni watu hatari sana, Wanasisitiza watu wajiajiri huku wao wakipiga magoti kwa wananchi wakihitaji wapate kura ili wawe wabunge na kujipatia pesa.

Vijana Jifunze toka kundi la Halima Mdee na wenzake 18 baada ya kushindwa kuvumilia kuishi bila kazi wakajipeleka wenyewe wapate ajira, Kwa miaka yote ya Ubunge kwanini wanashindwa kuishi? Hapa ndipo linaingia neno bajeti.

Wanasiasa wanasisitiza Serikali iweke mazingira mazuri ya watu kujiajiri huku wao wenyewe wakiambiwa posho zao hazikatwi kodi wanakuwa wakali kama Mbogo, ni rahisi wanasiasa kutamka mishahara ya hizo taasisi hadharani lakini sio mishahara yao.

Wanasiasa hata siku moja hawataki kutamka kiwango cha chini cha mshahara kwenye taasisi hizo wanaogopa watu watalinganisha na pesa wanazovuna ndani ya mwezi mmoja, Wao wanatamka mishahara ya kiwango cha ukurugenzi wa taasisi, Kiwango ambacho kinawa changanya vijana na kufikiria mambo makubwa ambayo sio uhalisia.

Napenda Kusisitiza bajeti kwa vijana ndio msingi mkuu kwako, Usikubali ndoto yako ikazimwa ghafla kwa kujihusisha na wizi, Rushwa na ubadhirifu kutokana na maneno ya wanasiasa kuhusu ukubwa wa mishahara ya wakurugenzi wa taasisi hizo ambao sio uhalisia wa mshahara kwa kijana anayeanza kazi.
Aisee
 
Back
Top Bottom