Siasa za mishahara minono kwenye taasisi za Serikali zinavyoharibu ndoto za vijana wengi wa Kitanzania

GUSSIE

JF-Expert Member
Dec 2, 2014
3,866
11,100
Wanabodi, vijana badala ya kufikiria maarifa ili waweze kuendeleza wapatacho wao wanawaza mishahara minono kwenye taasisi za kiserikali ambazo Kiuhalisia mishahara hiyo minono haipo kwa vijana wanaoanza kazi.

Maneno ya wanasiasa majukwaani kutamka mishahara ya wakurugenzi(Directors) wa mashirika hadharani kama NSSF, PSSF, NHC, TANAPA, TRA na baadhi ya Private commercial Bank imepelekea vijana kuhisi huko ndio kuna pesa na mishahara minono.

Vijana lazima watambue sio rahisi kufika kwenye nafasi ya ukurugenzi haraka haraka na kufikia kiwango cha mshahara unaotamkwa na wanasiasa jukwaani.

Kama hiyo mishahara ni mikubwa kiasi hicho kwanini wao wanasiasa wameacha kazi kwenye hayo mashirika na kukimbilia kugombea Ubunge?

Vijana wanapokosa mshahara waliousikia toka kwa wanasiasa wanapoajiriwa na taasisi hizo hujiingiza kwenye mambo ya rushwa, uwizi na ubadhirifu wa Mali za uma.

Ndoto nyingi za vijana zimevunjika na kufa na Wengine kuishia jela kabisa baada ya kujihusisha na vitendo vya uwizi na ubadhirifu wa Mali za taasisi baada ya kukosa mishahara walioisikia toka mdomoni mwa wanasiasa.

Hakuna mshahara mkubwa au mdogo hata siku moja, cha muhimu ni bajeti.

Bajeti ndio msingi kwa mfanyakazi kama ilivyo kwa sisi wakinga malengo ndio msingi wa biashara yako.

Nashauri vijana hizo taasisi zina malipo ya pesa za Kawaida kukuwezesha kuishi na kukopa pesa kwenye Saccos au Bank pamoja na mikopo ya magari.

Hizo taasisi za Serikali watu wanaacha kazi kila siku kufuata maslahi sekta binafsi.

Kwa mfano:
Kuna watu wanalipwa laki 5,Lakini mwisho wa mwezi anakopwa na mtu anayelipwa million 8. Tatizo hapa ni Bajeti kwa mtu wa Milioni 8.

Wanasiasa ni watu hatari sana, Wanasisitiza watu wajiajiri huku wao wakipiga magoti kwa wananchi wakihitaji wapate kura ili wawe wabunge na kujipatia pesa.

Vijana Jifunze toka kundi la Halima Mdee na wenzake 18 baada ya kushindwa kuvumilia kuishi bila kazi wakajipeleka wenyewe wapate ajira, Kwa miaka yote ya Ubunge kwanini wanashindwa kuishi? Hapa ndipo linaingia neno bajeti.

Wanasiasa wanasisitiza Serikali iweke mazingira mazuri ya watu kujiajiri huku wao wenyewe wakiambiwa posho zao hazikatwi kodi wanakuwa wakali kama Mbogo, ni rahisi wanasiasa kutamka mishahara ya hizo taasisi hadharani lakini sio mishahara yao.

Wanasiasa hata siku moja hawataki kutamka kiwango cha chini cha mshahara kwenye taasisi hizo wanaogopa watu watalinganisha na pesa wanazovuna ndani ya mwezi mmoja, Wao wanatamka mishahara ya kiwango cha ukurugenzi wa taasisi, Kiwango ambacho kinawa changanya vijana na kufikiria mambo makubwa ambayo sio uhalisia.

Napenda Kusisitiza bajeti kwa vijana ndio msingi mkuu kwako, Usikubali ndoto yako ikazimwa ghafla kwa kujihusisha na wizi, Rushwa na ubadhirifu kutokana na maneno ya wanasiasa kuhusu ukubwa wa mishahara ya wakurugenzi wa taasisi hizo ambao sio uhalisia wa mshahara kwa kijana anayeanza kazi.
 
Kuna ukweli kidogo sn degree holder anayeanza kazi halmshauri kama HR anaanza na 720,000 lakini HR huyo huyo mwenye degree anayeanza kazi siku moja NSSF anaanza na 1,840,000 nje na posho, mtu anaingia kama dereva NHIF anapata mkopo wa hadi 50M lakini mtu mwenye masters halmashauri anayeanza kazi tofauti na mkuu wa idara anaweza kukopesha hadi milioni 10 tu? Wewe huoni kama kuna tatizo hapo? bado huyo ana posho kibao, tukubali kuna tatizo kubwa sn hapa.
 
Hayo mashirika uliyoyataja yanalipa vizuri sn tofauti na local and central government mkuu, fanya utafiti vizuri TANROAD PS mwenye certificate anaanza na laki 8 hiyo ni fair kweli?

Tafuta mtumishi wa TANROAD yoyote ambaye ana miaka 2 kazini ambaye hana nyumba na usafiri hata mmoja labda awe amelogwa mpaka dereva mazee. Sijawahi kuona mtu anaomba kuhama kutoka NSSF, PSSSF, TANROAD, LATRA, TANAPA, TANESCO, TRA n.k kwenda halmshauri au mkoani kwa RAS tuache utani kuna gap kubwa sn
 
Kuna ukweli kidogo sn degree holder anayeanza kazi halmshauri kama HR anaanza na 720,000 lakini HR huyo huyo mwenye degree anayeanza kazi siku moja NSSF anaanza na 1,840,000 nje na posho...
Mimi mpaka sasa kwa umri wangu huu sijawahi ona mtu anafanya kazi Halmashauri ana GPA ya 5.0 au hata 4.5

Halmashauri mpaka mwaka 2020 nilipozitembelea watu wanapiga soga na story tu ofisini, Mtu anaaga live kwa Bossi wake anasema Bossi Leo naenda kuvuna mahindi yangu shamba, Anaruhusiwa na kupewa gari ya ofisi anaambiwa mafuta uongezee kidogo kwenye gari

Halmashauri watu wana muda wa kufanya kazi nyingi za ziada, Ofisi za uhasibu Zinakuwa bize sana sana wakati wa kufunga mwaka tu kwenye Halmashauri nyingi

Baada ya mwezi wa kufunga mwaka kuisha kazi yao kubwa ni kuandika cheque na voucher ili kutafuna pesa za uma

Kwanini ulipwe pesa sawa na mtu anayeumia kazini?
 
Wewe utakuwa mgonjwa siyo bure, waliopo NSSF, PSSSF, sijui TANROAD GPA zao ni wote ni zaidi ya 4.5 au GPA ndiyo inafanya kazi
Mimi ninaofanya nao kazi hakuna mwenye GPA chini ya 4.5

Sisi tulikuwa tunaajiriwa toka University moja kwa moja, Tunapigiwa simu na Chuo

Hata kazi za juzi ambazo watu inabidi wafanye Aptitude wengi wana GPA zaidi ya 4.0

Matokeo yao pia ya Sekondari ni mazuri sana sana yanavutia sana sana labda washindwe interview

Wakati watu wanasoma mliiwaita wametumwa na vijiji, Wanalipwa pesa Mnalalamika

Sasa mwenye GPA ya 4.8 alipwe sawa na wewe mwenye GPA chini ya 4.0?

Hata kama mtu alibebwa lakini na yeye anabebeka pia
 
Mimi ninaofanya nao kazi hakuna mwenye GPA chini ya 4.5

Sisi tulikuwa tunaajiriwa toka University moja kwa moja, Tunapigiwa simu na Chuo...
Wewe utakuwa na tatizo la akili siyo bure, PS, dereva sijui RMA nao wa GPA zaidi ya 4.0? watu tunaishi nao tumesoma nao inamaana hatuwajui?

Hao wanaohama toka halmshauri kwenda huko wote wana GPA ya 4.0 na zaidi? Wewe na GPA yako ya 4.8 umefanya nini cha maana kama siyo ujinga ujinga na kujifisia na makaratasi lakini kiuhalisia huna lolote unalojua.
 
Wewe utakuwa na tatizo la akili siyo bure, PS, dereva sijui RMA nao wa GPA zaidi ya 4.0? watu tunaishi nao tumesoma nao inamaana hatuwajui? hao wanaohama toka halmshauri kwenda huko wote wana GPA ya 4.0 na zaidi? wewe na GPA yako ya 4.8 umefanya nini cha maana kama siyo ujinga ujinga na kujifisia na makaratasi lakini kiuhalisia huna lolote unalojua
Hata kama sina ninachojua lakini kwanini nafanya kazi hapa na wewe kwanini upo huko Unalia lia

Kila mtu na bahati yake pia, Wewe huna bahati ya kuhama

Ungekuwa na bahati ungehama, Nyota yako ina giza giza na ukungu kwa mbali ndio maana upo hapo ulipo

Na kwa kulia lia huko utaendelea kuwepo hapo kila siku

Nakushauri njoo PM nikupe ushauri, Kuna mambo lazima upewe connection na usaidiwe kwenye Maisha haya

Ukiwa unashupaza shingo na kusema mbona Wengine wamefeli nawafahamu lakini wapo hapo kuna mambo mengi nyuma ya Pazia

Kuna baadhi ya kazi watu wanapewa nafasi kutokana na Reputational au heshima mzazi aliyoweka kwenye taasisi hiyo, Hivyo moja kwa moja ni rahisi kuamini hata akiharibu tutampata wapi?

Mimi nilitegemea mtu ungeniuliza kwanini watu Wengine wapo huko na waliingia vipi na hawana vigezo na waliingiaje huko?

Je, hao wanafanyaje? Ningeweza kukueleza hata PM sio hapa jukwaani.

Kuna uzi hapa ulikuwa unaeleza mambo ya wakinga na utajiri wao, Kuna member baada ya kusoma Jibu langu alikuja PM tukaongea mengi

Huyu Member anaweza toa ushahidi hapa

Jifunze kujifunza vitu na watu ndio connection yako,
 
Mimi ninaofanya nao kazi hakuna mwenye GPA chini ya 4.5

Sisi tulikuwa tunaajiriwa toka University moja kwa moja, Tunapigiwa simu na Chuo...
mkuu kuna kitu ina itwa connection ina nguvu kulko degree tatu kuna jamaaa ni kilaza na mjua ila yupo kitengo kizito TRA. Kama un connection wew soma kama umetumwa
 
Mimi ninaofanya nao kazi hakuna mwenye GPA chini ya 4.5

Sisi tulikuwa tunaajiriwa toka University moja kwa moja, Tunapigiwa simu na Chuo....
Wanataka kusema anayefanya kazi kituo cha afya alipwe sawa na anayefanya kazi MNH.

Au mhasibu wa halmashauri alipwe sawa na mhasibu wa BoT.

Hawajui mzigo wa kazi ni tofauti kabisa.

Na hata kupata kwenyewe hiyo kazi ni tofauti, mashirika mengi lazima mpige interview ya kufa mtu while huko chini tamisemi ama wizara husika inakusanya graduates tuu na kuwagawa.
 
Mimi ninaofanya nao kazi hakuna mwenye GPA chini ya 4.5

Sisi tulikuwa tunaajiriwa toka University moja kwa moja, Tunapigiwa simu na Chuo...
Peleka ujinga wako wa GPA nenda REA kaulize mishahara vs GPA yako?

Saivi baada ya MAGU KUZUIA AJIRA JOB MOVEMENTS WITHIN GOVERMENT NI KUBWA MNO na Receiving employer haangalii GPA hayo yanabaki kwenye makaratasi huko mkaajiriwe Teaching institutions.
 
Peleka ujinga wako wa GPA nenda REA kaulize mishahara vs GPA yako?

Saivi baada ya MAGU KUZUIA AJIRA JOB MOVEMENTS WITHIN GOVERMENT NI KUBWA MNO na Receiving employer haangalii GPA hayo yanabaki kwenye makaratasi huko mkaajiriwe Teaching institutions.
Toka Halmashauri mpaka BOT

Hiyo haipo
 
Toka Halmashauri mpaka BOT

Hiyo haipo
Katika taasisi zooote kama unaakili kwanini umechagua BOT unahisi wana hela kuliko baadhi ya Taasisi kama hujui nyamaza mkuu, kuna Taasisi mid level officer wala hukai nae meza moja mkajadili maendeleo binafsi unaweza kuacha kazi.

Najua ninachokisema, kama GPA yako ilikupeleka POT good for you ila wenzanko wapo vyuoni wanafundisha huko, hawana tofauti na walimu kwa workload
 
Katika taasisi zooote kama unaakili kwanini umechagua BOT unahisi wana hela kuliko baadhi ya Taasisi kama hujui nyamaza mkuu, kuna Taasisi mid level officer wala hukai nae meza moja mkajadili maendeleo binafsi unaweza kuacha kazi. Najua ninachokisema, kama GPA yako ilikupeleka POT good for you ila wenzanko wapo vyuoni wanafundisha huko, hawana tofauti na walimu kwa workload
Hueleweki unachoandika
 
Back
Top Bottom