Ndugu yangu,Enginner,
Kazi za mbunge ni
Kipimo cha ufanisi wa mbunge wakati wa muhula wake sharti kiendane na kazi zake kama inavyotajwa hapo juu.
- Kutunga sheria;
- Kuisimamia serikali; na
- Kuwakilisha wananchi.
Ni makosa kwa wananchi kudhani mbunge anatakiwa kujenga shule, vituo vya afya, barabara, visima vya maji na kadhalika. shughuli hizi pamoja na nyinginezo zianzofanana na hizo ni wajibu wa serikali. Lakini iwapo serikali itakuwa imetekwa na mafisadi haiwezi kuwa na rasilimali za kutosha kugharimia shughuli za maendeleo kwa ajili ya manufaa ya wananchi. Kyela haina shule, barabara, vituo vya afya au miundombinu ya huduma nyingine, ambavyo ni hafifu, basi kelele za Mbunge wenu Mwakyembe dhidi ya mafisadi ndio mahali pake; anaisimamia serikali ipasavyo. Shukuruni Mwenyezi Mungu kwa maana mnaye mbunge mahili anayefanya kazi zake kwa ipaswavyo.
Mtu yeyote anayejinadi kujendga visima vya maji, kujenga barabara, kununulia watoto sare za shule na kadhalika sharti atambulike kuwa ni mtu asiyefaa kuwa mbunge, kwa sabau, ama hana uelewa na kazi za mbunge au ni malaghai. Je, Kyela mnataka kulaghaiwa?
Ni juu yenu kusuka au kunyoa!
wakhtanabahu
Injinia ebu nielezee kidogo sifa za mwakyembe (LOL). najua huwezi!!!
Alipoulizwa kiini cha mgogoro kati yake na Bw. Mwakipesile unasababishwa na nini, Dkt. Mwakyembe alisema kuwa yeye hana mgogoro wowote na mkuu huyo wa mkoa, bali yeye RC huyo anayekwamisha maendeleo ya mkoa huo kutokana na muda wote kukaa Kyela kwa lengo la kumwondoa mbunge mwaka 2010.
huu uchafu wa mwakyembe na mwakipesile unaniudhi kweli.ngoja nakuja kugombea ubunge kyela kwa tiketi ya nanii!mizee mizima inashambuliana kwenye vyombo vya habari.Haki ya nani yaani basi tu
huu uchafu wa mwakyembe na mwakipesile unaniudhi kweli.ngoja nakuja kugombea ubunge kyela kwa tiketi ya nanii!mizee mizima inashambuliana kwenye vyombo vya habari.Haki ya nani yaani basi tu
Ndugu yangu,
Kama kazi za mbunge ni hizo tu unazozisema wewe, basi hatuhitaji kuwa na wabunge wa majimbo. Tuanzishe wabunge wa kuchaguliwa kufuatana na kura za chama kama zinavyofanya baadhi ya nchi.
Pesa nyingi sasa ziko kwenye halmashauri ya wilaya na hata mipango mingi ya maendeleo inaamuliwa huko na sijui kwa kazi za mbunge kama ulivyoandika, nini wajibu wa mbunge kwenye halmashauri ya wilaya yake?
Nakuhakikishia, kazi ya mbunge ni zaidi ya ulizozitaja. Maendeleo sehemu kubwa kwasasa hayaletwi na serikali peke yake. Sehemu kubwa wananchi wanachangia na Mbunge hapo ni kiungo muhimu mno.

Ili kuwa fair, ni vema Muungwana akampiga chini mwakipesile na wanakyela nao wakampiga chini huyo mwakyembe.Tumechoka kila siku kusikia kelele zisizoisha juu ya ugomvi wao ambao hauwasaidii wananchi zaidi ya kuwaacha maskini wa kutupwa.
mwee tubhuke nkughala ubwalwa iwikiendi jifikile bha kana nongi
Hii kitu nadhani hata JK anahusika. Amebadilisha Wakuu wa Mikoa yote akamwacha Mwakipesile pale pale. Kweli Mbeya watapata Maendeleo kwa staili hii?? MC.
Ugomvi - Kakosana karibu na kila kiongozi Kyela
Majigambo - Anadharau madiwani hawajasoma huku anaongoza wilaya ambayo zaidi ya asilimia 99 ya wananchi wake hawajafika chuo kikuu.
Uwongo - Sisi huku tunasema NTUNGULU FIJO. Dr kuzua jambo kwake sio kitu kigumu
USANII - Ukimsikia mikutano yake utacheka. Kuna sehemu anaulizwa tatizo la barabara, anasema wacha niongee na mhandisi, anapiga simu na kujadiliana na Mhandisi kwamba aache huko anakojenga barabara, aje Kyela maana wananchi wake wanateseka. Huo kama si usanii ni nini? Hizo simu huwa anwapigia wapambe wake. Mfano huo huo anaurudia kwenye vijiji vingine akiongelea mabomba ya maji. Anasahau huko nyuma huyo mhandisi alikuwa wa barabara, sasa kageuka wa maji.
Sifa zake:
Huku wanasema NKIFU maana yake Jasiri wa kuongea
Pia alifanya kazi nzuri Richmond.
Sisi tulimbeba Dr 2005 na kusukuma gari lake, ila sasa simtaki kabisa na wala hilo sifichi. Jamaa hata kuongoza mukutano tu kunamshinda, yeye ni manguvu tu na majigambo kwamba yeye kasoma, hajui hata wengine ni Wahandisi bwana!
Hizi habari zinanishtua sana. nimewahi sikia watu wanamwita prof J. kwa hizi sifa ninahisi mwakyembe wa 2005 sio wa leo sasa ngoja nifanye utafiti na kukusanya data hapo kyela ili niprove. lakini mimi sikumsukuma kabisa. pole kwa kumsukuma. uongo ni muongo hilo siwezi kataa. kwa kunipa sifa zake ambazo ni positive na negative inabidi nifanye utafiti mpya. lakini kuna diwani hapo hata mimi silidhiki na utendaji wake wa kazi hususani wa hapo mjini. nitakuja baada ya utafiti mkubwa kidogo. maana hii imenishtua sana.
Kaka Lole,Mapambano ya hwa jamaa kwenye vyombo vya habari inaeleka havina mshindi.
Mimi nataka kufadhili pambano la NDONDI KAVU KAVU kati ya Mwakyembe na Mwakipesile.
Sisi tunataka tujue nani zaidi.
Wengine kina Engineer na wapambe wa pande zote tafuteni washabiki ili mufurahishe roho zenu.