bambumbile
Senior Member
- Aug 30, 2009
- 109
- 0
hizi post za wanakyela na mwakyembe zimenikumbusha wimbo wa sikunyingi wa bongofleva uliimbwa na GWM[gangstars with matatizo] ulikokuwa unasema''kila kukicha kwa visavisa duhh''hivi majimbo mengine kuko shwari au kwakuwa hakuna waandishi wa habari?au huyu mwakyembe ni tishio sana mpaka watu wanakosa usingizi au yeye ndiye anaenyimwa usingizi na mgombea anaemuona ni kiboko yake?
kwanini kyela tuuuuuuuu?????
mwakyembe amesoma chuo cha uandishi wa habari ambacho ni chuo kikuu cha dar es salaam, (IJMC). hii ndio kauli yangu ya jana. labda nianze na kiswahili kilichotumika.
amesoma kitenzi kinachoonyesha wakali uliopo timilifu.
mwakyembe amesoma chuo cha uandishi wa habari ambacho ni chuo kikuu cha dar es salaam, (IJMC). hii ndio kauli yangu ya jana. labda nianze na kiswahili kilichotumika.
amesoma kitenzi kinachoonyesha wakali uliopo timilifu.
Wewe dogo mbona huelewi lugha? Mwakyembe hajasoma IJMC na badala yake yeye alisoma TSJ ambayo kwasasa inaitwa IJMC.
Hayo majina yanaendana na sheria, huwezi kutumia jina ambalo haliko kwenye cheti chako.
Ni sawa na daktari aliyemaliza Muhimbili miaka ya 80, leo aandike amesoma chuo kikuu cha Muhimbili. Lazima aendelee kusema amesoma UDSM. Hawa waliosoma Muhimbili baada ya kuwa chuo kikuu kinachojitegemea ndio wana haki ya kutumia jina jipya. Hivyo hivyo hata kwa chuo cha ardhi.
Kimjusi wamekibana kwenye MLANGO, macho yamemtoka PIMA kwa AIBU, hadi udenda unamtoka. Kijana alifikiri sisi mazezeta wenzake waliosomea kwenye taa za karabai za Mwakyembe alizopewa na Rostam Azziz. Kijana, kaanze upya maana hapa tutakukoma huku tunakuangalia USONI.
hapa pamekosa mantiki maana unaweza kutumia neno kama zezeta mahali ambapo si pake. wakati mwingine haya mambo yanaendana na mtazamo. kwa haya maneno tunapata mtazamo wa jinsi ulivyo.
Mhandisi, ona hata Robert Mugabe, wanaandika kuwa amezaliwa Kutama, Rhodesia na si Zimbabwe. Ila kijana wetu atakuwa hajui. Nampenda yule dogo mwengine ambaye yeye husema wazi kabisa kuwa ni dogo na angelipenda kujua mambo ya zamani. Watu humpa shule safi ambayo hata wengine tulifaidi maana tulikuwa tunayasikia juu juu. http://www.nndb.com/people/973/000022907/
Wewe dogo mbona huelewi lugha? Mwakyembe hajasoma IJMC na badala yake yeye alisoma TSJ ambayo kwasasa inaitwa IJMC.
kwa hili umeelewa. hapa umeweza kuonyesha uhusiano uliopo kati ya TSJ na IJMC. kama utaelewa hivi hakuna tatizo.
Hayo majina yanaendana na sheria, huwezi kutumia jina ambalo haliko kwenye cheti chako. hapa inategemeana na muktadha
Ni sawa na daktari aliyemaliza Muhimbili miaka ya 80, leo aandike amesoma chuo kikuu cha Muhimbili. Lazima aendelee kusema amesoma UDSM. Hawa waliosoma Muhimbili baada ya kuwa chuo kikuu kinachojitegemea ndio wana haki ya kutumia jina jipya. Hivyo hivyo hata kwa chuo cha ardhi.
kwa kuelewa pale juu inaonyesha umeelewa huitaji elimu zaidi. cha msingi ni kuelewa na si kukalili.
The School of Journalism and Mass Communication is a teaching , and research School of the University of Dar es Salaam. The School owes its origin to the former Tanzania School of Journalism (TSJ) which later got transformed into the Institute of Journalism and Mass Communication on 1st 2003 under the University Act, No.2 of 1972
hapa nilifikiri umeelewa kulink kati ya TSJ na IJMC. sasa kama hutaki kuelewa tatizo si lako ni la fikra yako isiyokubali kuelewa. kubishana katika hili hakuna kitu cha maana sana. suala ni kuelewa tu,ni suala la nyakati mbili tofauti. TSJ na IJMC unapotumia inatakiwa uelewe unatumia kwa wakati gani? Rhodesia na Zimbabwe kuna tofauti gani?mtu akisema mugabe amezaliwa zimbabwe hana kosa. na mwingine akisema alizaliwa RHODESIA. kwa mtu anayeelewa kuwa rhodesia ndio zimbabwe ya leo hakuna matatizo. kwa mtoto ambaye anakalili hapa ni ishu kubwa sana. kama unasoma cv na kukalili ishu ya TSJ na IJMC ni tatizo kwako!!! lakini kama unaelewa originality ya IJMC si tatizo. hapa kama hamtaelewa mna matatizo
Unashindwa hata kuona kwamba kuna tofauti kati ya TSJ na IJMC?
Ni very simple, Mugabe hakuzaliwa Zimbabwe kwasababu Zimbabwe haikuwepo, alizaliwa Rhodesia.
Mwakyembe hakusoma uandishi wa habari UDSM maana TSJ haikuwa sehemu ya mlimani.
Kijana mbishi sana! Au niseme una ubishi wa kijinga.
kuna mkono wa wakubwa kuiharibu mbeya,wanachofanya ni divide and rule.Kuna watu mbeya wanatumiwa na mafisadi na wao wanawakubali pasipo kufikiria hatima ya mkoa huo.Kuna watu kutoka nje ya mbeya wameamua kupandikiza chuki kati ya viongozi mbalimbali ili kufanikisha malengo yao waliyojiwekea kisiasa.Mpaka wakuu wa nchi wamo katika kufanikisha hili.Mwakipesile ni mtu namba moja katika kutumiwa kwani mwanzoni alitumiwa dhidi ya mwandosya wakati wa kampeni,yupo pia limbukeni mwingine anaitwa mwakalinga.Lakini nawashangaa wanambeya wanakubalije kutumiwa kiivyo,tuamuke tuchukue hatua.Vita iliyopo ni ya kufifisha juhudi za kupambana na ufisadi kwa kuhakikisha mwakyembe anang'olewa...
Tunaamini mbeya kuna watu wasomi na makini ambao hawako tayari kutumiwa,Kuweni makini wanambeya mtatumiwa na mafisadi........
injinia mimi sina tatizo na wewe,inawezekana unasema ukweli lakini ninaingiwa na mashaka nawe.wewe always uko dhidi ya DR. mda si mrefu ulikuwa kwa mwakalinga leo naona kama unamsapoti mwakipesile. mwakipisile ni mtu asiye na rafiki always, ni mtu mwenye hasira sana. ninakumbuka siku ya kupiga kura za maoni katika kanisa moja hapo mbugani zilizomfanya mwakyembe kuwa mgombea kwa tiketi ya CCM. mwakipesile alimshambulia kwa maneno moja kwa moja mwakyembe. hawa watu wanachanzo chao cha ugomvi wao. wote wanajifanya 'nibasisya' sasa hakuna mdogo kwa mwenzie. halafu hawa wengine madiwani ni wapambe wa kambi hizo mbili. maana ukipatana na mwakipesile ni moja kwa moja unakosana na mwakyembe. na ukipatana na mwakyembe tayari ni adui wa mwakipesile. ninakumbuka VIZURI kuna watu waliweka sherehe za kukosa uwaziri kwa mwakyembe. Hawa watu kupatana hawawezi kabisa. wakipatana nani atakuwa mdogo kwa mwenzie? hakuna anayekubali kuwa mdogo.Nyani haoni kundule, kama Mwakipesile hapatikani na mbunge yeyote wa mkoa wa Mbeya, je yeye Dr. Mwakyembe mbona na yeye hapatani na diwani yeyote wa wilaya ya Kyela? Mbona hapatani na kiongozi yetyote wa CCM wa wilaya ya Kyela. Hawa jamaa wote wawili wanaturudisha nyuma shauri ya ujinga wao usio na mwisho.
Baada ya kuitangazia dunia yote kwamba alitaka kuuwa, sasa anaanza kuruka na kusema ni uwongo? Amejua polisi wamegundua nini na anaanza kujiandaa kabla ya report. Kama ni uongo kwanini alienda kununua kisu na kuwapa wapambe ili wakitumie kama ushahidi wa kutaka kuuwa kwa kisu? Mbona alitumia magazeti ya MENGI kuitangazia dunia nzima kwamba alitaka kuuwa?
mzee kuna mjadala mwingine kule. maana mumeunda kikundi kidogo cha kutetea ufisadi na injinia. najua nako mtanipinga tu. halafu utakimbilia kusema huyu ndogo ninamfahamu ni mbishi. mwenzio enginia ameelewa(LOL). utamskia? japo hata wewe umeelewa tena kwa kuleta na citation hilo safi. sasa tukutane kwa mjadala wa mwakipesile. injinia tayari yuko kwa mwakipesile sasa we mdogo wake utamsaliti kweli? tutaona tu !!!.awu umeamua kugive thanks tu.Mhandisi,
Niliwaonya tangu mwanzo hamkuamini. Nilisema tangu mwanzo kuwa kijana ni MBISHI KAMA DAGAA, mlifikiri natania? Nilisema namfahamu kijana mlifikiri natania? Haya sasa hayo hapo MNAYAONA WENYEWE. Mie najitoa maana nilitaka tu kuwaonyesha kijana uwezo wake wa kubisha kuwa BLACK is black and WHITE is WHITE.
Ngoja nimfuate kwenye mijadala mingine anakotumia jina jingine.... hihiii 🙂
KASYABONE: Sawa mkuu, nakubaliana na wewe kuwa Mwakyembe ana DEGREE ya UANDISHI WA HABARI ya UDSM.
Enginner,Jile97,
Unajua mtu Limbukeni ndiye anaita wengine Limbukeni. Mwakalinga ana kosa gani kuamua kugombea ubunge Kyela?
Acheni ujinga wenu wa kusema kuna watu wanatumiwa, kama ni hivyo toa ushahidi. Wewe kuja kuandika hapa unatumiwa na nani?
Kyela tunataka hata watu wengine waje tu kugombea ili tupate kuchuja na kupata kiongozi bora na sio hawa wasanii, kila siku mafisadi tu huku watoto hawana hata madarasa ya kusomea.
Ufisadi umegeuka mtaji wa kisiasa. Kama mtu anataka kupigana na mafisadi basi aende akagombee kule kwa RA au kule kwa Lowassa.
Kyela ina matatizo yake mengi ambayo sasa hayatatuliwi kwasababu viongozi ni kugombana tu kila siku. Mbunge akija anaongea mafisadi tu hotuba nzima utafikiri Kyela haina matatizo mengine.
Ifike 2010 tutampiga chini tu na kama anafaa basi JK amteue kuwa mbunge wa taifa. Nyie mnaomtaka Mwakyembe muiteni kwenye majimbo yenu na ndio mtamjua Mwakyembe ni nani.
Hapa Kyela wote tulikuwa tunamuunga mkono lakini sasa kabaki na Wapambe tu. Anatukana kila mtu kwamba hajasoma, vijana wakimzomea anawaweka ndani polisi. Huyo jamaa yenu ameisha hapa Kyela na hata yeye anajua na ndio maana ya kelele zote hizo.
Kawatuma mpaka akina Kifukwe Uingereza kwenda kumtisha Mwakalinga asigombee lakini naona haijazaa matunda.
Mwisho wake ulihitimishwa siku ile alipotunga uwongo wa kwamba alitaka kuchomwa kisu. Hapo ndipo hata wale wachache waliokuwa wanamtetea wakaamua kumtosa. Mbunge mwenye akili timamu hawezi kuja na uwongo kama huo. Kibaya imegundulika hata kisu wanachosema kilitaka kutumika, kumbe kilinunuliwa na Dr. mwenyewe pale Kyela mjini siku ya tukio.