Siasa za Mbeya 2005-2010

Yule mwandishi wa habari ya awali (NIPASHE) huenda analipwa na Dr. Mwakyembe na huyu wa TAZAMA TANZANIA (gazeti la Lowasa na Karamagi) huenda analipwa na Mwakalinga. Sasa hapo ndo wasomaji kuchambua machuya na mchele.
 
Nemesis;

unachekesha, Sio kwamba analipwa na mafisadi? imeshageuka kuwa analipwa na GAM? LOL

Mtageuza story kama mpendavyo, the truth shall prevail!!!


FP
 
engineer wa majungu ya ukweli mkuu,wanakyela wamesha mstukia kuwa ni mamluki katumwa na mafisadi na kapewa minoti kufa mtu.......

Jile habari yako hapo juu imenichekesha sana kwa kweli;sidhani kama "Engineer"kapewa hela yeyote na mafisadi maana angekuwa nazo lzm angekuja pale kijiweni kwetu Kyerucu kula bata na rafiki zake akina Kenne,Malwilo na Kambi!

Namtetea kwa hilo,hajapewa hela lkn huwa anajaziwa pikipiki yake mafuta ili awe anazunguka vijijini hasa kule Ipinda,Kasumulu,Ntaba,Butangali,Njisi,Matema,Kafundo,Mwaya na Kajunjumele kuona wana Kyela wanamuongelea vipi Mbunge wao!

"Engineer" njoo kesho hapa Baling'enyo tupate kubadilishana mawazo hasa nikimaliza safari ya kutoka kijijini kwetu Ilopa;jana nilikuona pale kibandani kwa Madaraka nahisi ulikuwa unaongea na kaka Maneno!
 
Mhandisi,
Na heshima zote lazima nikuambie kuwa Shalom na Masanilo ni watu wawili tofauti. Shalom ni Mnyakyusa na Masanilo ni Msukuma. Mengine yote nawaachieni wenyewe ila nilitaka kukusaidia kwa hilo tu.
Asante Sikonge,

Najua Masanilo na Shalom (mwekezaji wa Wazungu) ni tofauti ila mimi nawaweka pamoja kwasababu usanii wao unafanana ingawaje wa Shalom umezidi kipimo.

Masanilo kinachomsumbua zaidi ni ile Mkapa aliyosema Mijitu mingine ina wivu wa kijinga.

Hapa naenda vijijini kusambaza gazeti la Tazama. Pikipiki yangu imeshajaa mafuta. Huyu mwandishi mungu ampe uhai maana hawa mashemeji wa Mwakyembe (IPP) wamezidi kutuonea.
 

Baba Mkwe,

Nimeambiwa uko hapa mjini. Vipi msanii amekuita uje usaidie kuokoa boat lake? Mwiteni Shalom alete wazungu wake waje wasifie vikoba. Kwenye mkutano wao mmoja, walikutana na vijana wa vikoba. Mzungu mmoja akaanza " We are very impressed with your project and we wish we had ability to help you financially" Shalom akatafsiri " Tumefurahishwa sana na mradi wenu na tunaahidi tukifika nyumbani tutawachangia pesa nyingi kwa ajili ya mradi wenu" Vijana wakashangilia kweli kweli, huku pembeni Dr. akawa amefurahi kweli. Hawakujua kuna kijana pale kasoma Malawi na anaelewa Kiingereza.

Mimi niko busy sana kwasasa na muda wa kuja hapo Balimonye sina. Naona wewe ni wa kuja hata jina la guest ya ndugu yenu unalikosea. Hizo pesa za beer sisi ndio tunazitumbukiza kwa Mwakalinga kusaidia vijana wazunguke vijijini. Huu muda sio wa beer tena bali mabadiliko.

Vipi huko Kajunjumele? Dr. anafikiri ataweza kupambana na komandoo Majuni? Juzi anaimba nilimwachia Majuni milioni moja na nusu za ujenzi wa shule. Watu wakacheka na kuanza kuondoka, wakawa wanasema msanii huyu, hata kuongea na Majuni tu hawaongei kweli ataweza kumwachia pesa?

Karibu Kyela yetu, ungemwalika na Sikonge.Mimi namsubiri huyu mpiganaji Sikonge aje Kyela ndio nimwonyeshe viwanja vyote.
 
pindi watu wazima wanapotumia muda wao mwingi kukujadili, jua u have made a big impact in society.bravo Harrison, u have made it!
 

dah pole sana ndugu yangu kumbe unanaukabila pia? mimi sina kabila ndugu mimi ni mtanzania tu sio mnyakyusa wala mpare,
 
Huyo kijana angekuwa mtoto wa maskini, mpaka sasa angekuwa anasota rumande bila kosa.

Mbunge unaanza kuwatungia wananchi wako makosa makubwa kama hayo? Mbunge inatakiwa uwe unatetea wanyonge na wala sio kuwazulia wanyonge makosa ambayo hayapo.

Mbona uchaguzi uko mbali? Tunataka tuwapige chini wababaishaji.
 
dah pole sana ndugu yangu kumbe unanaukabila pia? mimi sina kabila ndugu mimi ni mtanzania tu sio mnyakyusa wala mpare,

Ningelikuwa na UKABILA si ningelikuwa kwenye mambo ya Tabora na Sikonge huko? Ila nipo hapa nikimkoma nyani wa Kinyakyusa. Sasa unaniita mie Mkabila, zinakutosha kweli wewe? Au neno FIKIRI limeondolewa kwenye ubongo wako?

NB: Masanilo, wahi Sikonge sasa mkuu maana haya Matonga kwa sasa yapo kibao. Pia Mahama na Nfulu ndiyo zimeiva kwa wingi. Ntalantu nazo msituni kwa wingi sana. Mapera na Mapapai yameisha na twajiandaa kwa Maembe mwezi ujao mwishoni. Ahhhh, maembe wewe acha. Asali aka "wuki" ndiyo kwa saana. Chai ya asali umeshakunywa mkuu? Ngoja nimalise maana Lorah atasema "si mkabila huyu?"
 

??????????????????????????????????"
 

Bambumbile,

Leo hii wametangaza uchunguzi tiyari umekamilika. Tusubiri tuu usiwe na haraka.
 
Mwanakatwe unatia huruma ndugu yetu. Karibu ukweli wote utajulikana, endelea kuwalaumu polisi wa Kyela. Uchunguzi huu umefanywa na RCO. Wajanja wa mjini tunajua wamegundua nini, siku hiyo nitalewa kimpumu ile mbaya. Wamefulia kweli kweli!

 
Mwanakatwe unatia huruma ndugu yetu. Karibu ukweli wote utajulikana, endelea kuwalaumu polisi wa Kyela. Uchunguzi huu umefanywa na RCO. Wajanja wa mjini tunajua wamegundua nini, siku hiyo nitalewa kimpumu ile mbaya. Wamefulia kweli kweli!

Hili nalo tunatakiwa kulijua? walevi wa chimpumu ovyo kabisa
 
Hili nalo tunatakiwa kulijua? walevi wa chimpumu ovyo kabisa

Na wewe ****** siku hiyo sijui uso wako utaficha wapi? Mijitu mingine kama Masanilo ina wivu wa kijinga.

Hapo RPC haongelei tena mauaji bali utekaji nyara.

Malafyale,
Siku wakitoa taarifa tu nitakutafuta nikupe beer Barimonye, pesa ya siku moja nitaipata tu hata kama itakuwa kwa kuuza kokoa mbichi.

Eti Engineer wa majungu ha haa haaaa!!! For Kyela Breaking News - Engineer is the man! Itabidi munipe mji tu au kata ila isiwe Ikolo maana kule wasanii wengi sana pia kuna mbunge mteka vijana, sitaki waniue miye! maana JF bado inanihitaji for Breaking News!
 

Engineer mpika majungu!

Engineer is an old lady in menopause
 
Umoja wa vijana wa CCM wilaya ya Kyela wametoa tamko kali kulaani kijana mwenzao Dan Mwakalinga kutekwa nyara na kisha kusingiziwa kwamba alitaka kumdhuru mbunge.

Wameomba uongozi wa polisi ukamilishe uchunguzi haraka na wahusika kuchukuliwa hatua mara moja.

Walipokea taarifa kutoka kata ya Ngusa kuelezea nini kilitokea siku hiyo. Taarifa hiyo ilitamka wazi kwamba tukio la kuuawa mbunge halikuwepo na ni usanii wa kisiasa ambao umeleta madhara makubwa kwa kijana mwenzao kuishia lupango kwa masaa karibu 24.

Nikilipata tamko lenyewe nitawarushia.
 
Sikonge/Engineer:
Mbona hamjibu maswali? Tunauliza, mworozeshe yale aliyoweza Mwakyembe, na yale aliyoshindwa. Kisha mtuonyeshe yale atakayoweza Mwakalinga.
Sisi wana Kyela tunataka maendeleo, si tu ya Kyela bali ya nchi nzima. Leteni data hapa, ni kipi kinamsukuma Mwakalinga kuwania ubunge? Ni yepi atayafanya kuliko Mwakyembe? Na yepi aliyoshindwa
Mwakyembe?. Maana tukijua hilo we will not give a damn to Mwakyembe and we will all go to Mwakalinga or any other aspirant. Jibu swali hili tuanzie
 
Sikonge/Engineer:
Mbona hamjibu maswali? Tunauliza, mworozeshe yale aliyoweza Mwakyembe, na yale aliyoshindwa. Kisha mtuonyeshe yale atakayoweza Mwakalinga.
Sisi wana Kyela tunataka maendeleo, si tu ya Kyela bali ya nchi nzima. Leteni data hapa, ni kipi kinamsukuma Mwakalinga kuwania ubunge? Ni yepi atayafanya kuliko Mwakyembe? Na yepi aliyoshindwa
Mwakyembe?. Maana tukijua hilo we will not give a damn to Mwakyembe and we will all go to Mwakalinga or any other aspirant. Jibu swali hili tuanzie hapo.....
 

Mkuu Nyumbu,

Mimi siko upande wowote lakini ninaamini hayo maswali yako yatajibiwa vizuri tu na hawa "wapiganaji" watakapokuwa wanajinadi mbele ya wapiga kura wa Kyela .... hapo ndipo itajulikana Mwakyembe aliahidi nini na amefanya nini; na vivyo wana-Kyela watapata fursa ya kumsikiliza Mwakalinga na ahadi zake .... then watapiga kura!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…