figganigga
Platinum Member
- Oct 17, 2010
- 28,008
- 63,988
Usajili wa Bajaji wapigwa marufuku Mkoani Mbeya na Waziri wa TAMISEMI Riziki Shemdoe alipokuwa akizungumza na vijana wa bodaboda, Bajaji na kumpa Maagizo Mkuu wa mkoa wa Mbeya kuunda Tume. Vilevile kasema Mgomo umesababishwa na Mkoa kutowashirikisha Bajaji kwenye maamuzi yao. Mwakilishi wa Bajaji kasema Viongozi walikuwa hawataki kuwasikiliza badala yake walikuwa wanatishwa kila wakiomba kusikilizwa.
Wakati huo huo amewaruhusu Bajaji kuendelea na kazi kwa muda wa wiki mbili huku akimtaka mkuu wa Mkoa kuwapanga Bajaji katika zone tofauti.
Waziri amesema Mkuu wa Mkoa alitekeleza agizo la Samia Suluhu aliye waagiza miji iwe misafi.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OWM–TAMISEMI), Prof. Riziki Shemdoe, ameelekeza kuundwa kwa timu itakayozunguka Jiji la Mbeya kufanya tathmini ya maeneo watakayotumia madereva wa bajaji, njia watakazotumia, njia za daladala pamoja na kupendekeza njia za usafiri zitakazowawezesha abiria kufika katika eneo la uwanja wa ndege wa zamani, ambako soko la wamachinga litajengwa.
Prof. Shemdoe amesema uundaji wa timu hiyo ni hatua ya kutatua mgogoro baina ya madereva wa bajaji na daladala uliopelekea kuibuka kwa mgomo wa madereva hao na kusababisha kusimama kwa huduma za usafiri jijini Mbeya, na kuongeza kuwa mgomo huo ulitokana na uongozi wa mkoa kutowashirikisha kikamilifu madereva wa bajaji katika kutekeleza maelekezo ya Samia Suluhu Hassan ya kuboresha usalama wa madereva hao.
Kumbuka Mei 21, 2026 LATRA ilisema, Mamlaka imewaelekeza Mawakala wanaotoa huduma za leseni za usafirishaji wa pikipiki za magurudumu mawili na matatu (Bodaboda na Bajaji) kwa niaba ya LATRA, kisajili kwa kusimamia misingi ya kisheria iliyopo kwenye leseni zao za uwakala katika utoaji wa huduma za leseni za bodaboda na bajaji.
Baada ya Bajaji kadhaa kusaajiliwa leoo wanapiga marufuku kusajili wakati kuna bajaji nyingi zinasubiriwa kusajiliwa. Inadaiwa Mbeya mjini ina Bajaji elfu sita tu.
MY TAKE
Haya ndo madhara ya kuingia madarakani bila kuchaguliwa. Hajui shida za wananchi.
Hapo atakuja Mwigulu atatue hilo tatizo halafu ashangiliwe.
CCM wanatengeneza tatizo halafu wanalitatua kisha wanasema tumesikia kilio cha Wananchi samia ni msikivu makofi kwake. 🤣 🤣🤣🤣🤣