Siasa za CHADEMA hatimaye zaanza kutuchosha wanachama

Siasa za CHADEMA hatimaye zaanza kutuchosha wanachama

Salaam,

Napenda kuisihi CC ya CHADEMA iitishe kikao cha dharula cha kujadili barua ya utetezi dhidi ya mashitaka yanayomkabili Zitto; na mwishowe imvue uanachama na hivyo kupoteza ubunge wake..
Kiongozi Unaongea tofauti na wajumbe wa Kamai kuu wanavyoliona swala hili,

"Bahati nzuri wamevuliwa uongozi siyo uanachama, binafsi nadhani viongozi wanatakiwa kutafakari na kudhibiti madhara zaidi kwa chama, wakishupaza shingo, lolote litakalotokea watakuwa ni sehemu ya lawama," Profesa Baregu alisema Dar es Salaam jana.
Source: November 2013 | KAPINGAZ
 
wana Jf hawa viongozi digitali wana matatizo sana. Lengo ni kupata atteantion ya wasiokuwa na uwezo wa kufuatilia haya mambo kwa undani.

Wilbroad Slaa amekuwa amekuwa maarufu sio kwa kuleta usumbufu kwenye chama, amekuwa maarufu kwa kuwasemea watanzania walio wengi. Hatuoni umimi kwa mtu kama Slaa pamoja na umaarufu wote huo na kuwa mwiba kwa CCM ya mafisadi. Vyama vya siasa kama iliyo serikali yenyewe bado vinahitaji maboresho makubwa kwenye mifumo yao ya usimamizi wa fedha. Maboresho hayo yanapaswa yasimamiwe na serikali kwani serikali ndio msimamizi wa rasilimali za taifa ikiwemo pesa za walipa kodi wanazopewa vyama kama ruzuku. Udhaifu wowote unaotokana na mifumo hautoshi kusema vyama vya siasa vinakula pesa za ruzuku. Naibu katibu mkuu wa chama badala ya kuongoza chama chako kuelekea kwenye mifumo bora ya usimamizi wa rasilimali wewe unakimbilia twitter na facebook kupayukapayuka hovyo. Hiki kizazi cha namna hii ni hatari kuliko mafisadi wazee waliopo CCM.
 
Naunga Mkono hoja.

Mtu anayekisaliti chama kwa manufaa ya MAGAMBA huyo siyo wa kucheka naye. Ni kufukuza tu.

MAGAMBA wamekuwa wakimkuwadia sana ili akamilishe mradi aliotumwa nao wa kuibomoa kama siyo kuiua kabisa CDM kabla ya 2013 kama MAGAMBA walivyokuwa wanajiapiza.

Chondechonde Kamati Kuu fanyeni haraka nadhani mnakumbuka alivyosababisha vijana wengine waliokuwa wapambanaji kufukuzwa kama Kafulila, Mwapamba, Shonza, (just to mention few).
 
sijui wanasubiri nini kumuondoa huyo mchumia tumbo.
 
Zzk anasikitisha. Itachukua miaka 1000 kigoma kutoa kiongozi wa kuaminiwa hapa nchini maana wote waliojaribu toka huko wameishia kujiporomosha wao wenyewe. Kuanzia Kaburu, Nsangugwako, Kafulila, Ntagazwa na sasa Zitto.
 
Siku zote jina la shujaa hutajwa mara nyingi kuliko majina yote Zitto ni shujaa ndo maana kila kukicha ni zitto tu hakuna habar nyingine
 
Mbona unawapa wenzio mtihani mkubwa hivyo? Unadhan ni kazi nyepes et? Waambie wajaribu waone, hapo walipo walihisi wana kigoma watamfukuza na badala yake wanampokea kifalme! Msiporuhusu demokrasia chadema itabaki ya maendeleo ya wachaga wachache tu
 
Sikubalieni na wewe kiongozi nafikiri mitandao hii ni sauti kwa wasio kuwa na sauti. Nafikiri ni suala la viongozi kusikiliza maoni kutoka pande zote maana hawa ndo wapiga kura wenyewe.Leo anaweza kuwa adui yetu lkn kesho akajua ukweli akawa upande wetu. Mimi nilikuwa na waCCM kindakindaki lkn leo ni CHADEMA damu baada ya kuwahubiria kwa muda mrefu.
Ahsante sn kwa kunielewa kiongozi.

kweli wewe ni GT
 
Kumbe ili uwe mwanachama wa chadema mwenye nidhamu lazima usihoji jambo lolote la msingi kwa uongozi?
Kama wewe ndiye mwanachama wa chadema mwenye nidhamu basi chama hakina jipya na ndio mlaana mtaendelea kuburuzwa na watu wachache kwa maslahi yao wachache,AIBU sana hii

Demokrasia bila mipaka....
 
mbwa mzee hafundishwi mbinu mpya wakuu...........makengeza na kikongwe waondoke la sivyo watasimamisha wanachama wote wabaki wenyewe tu
 
Salaam,

Napenda kuisihi CC ya CHADEMA iitishe kikao cha dharula cha kujadili barua ya utetezi dhidi ya mashitaka yanayomkabili Zitto; na mwishowe imvue uanachama na hivyo kupoteza ubunge wake.

Ni wazi CHADEMA imemvumilia huyu jamaa kwa muda mrefu licha ya harakati zake ambazo amekuwa akizifanya za kuzoofisha chama kwa miaka kadhaa. Sina sababu ya kurudia kuzitaja harakati hizo ambazo zinafahamika na kila mmoja.

Hapa naihasa tu CHADEMA ichukue maamuzi ya haraka sana ya kumvua uanachama ndugu Zitto, la sivyo ataendelea kuleta madhara ndani ya chama kama akiendelea kuchekewa.

Nilitarajia mtu ambaye ameshitakiwa hata kama ni kwa kuonewa, awe mtulivu ili kusubiri hatma yake. Badala yake huyu jamaa kwa kushirikiana na "washirika" wake, ameendelea na harakati zake haramu za kuleta mitafaruku na kutukana viongozi wa juu wa chama. Safari hii akifanya hivyo "mchana kweupee". Mshirika mkuu akiwa Albati Msando ambaye naye amekuwa akisambaza jumbe za kutukana na kubeza viongozi kwenye mitandao ya kijamii.

Nasema CC imtimue Zitto haraka sana. Madhara yake akiwa nje ni madogo kuliko "spoil" anayoifanya sasa akiwa ndani ya chama.

Wasalaam.


wadhani rahisi kihivyo,, labda chama kiwe mali ya MTEI,,,na mapoyoyo kama wewe, kama ni cha wanaCHADEMA basi taratibu lazima zifuatwe,,,kwani Zitto bado ni mwanachama na ana haki zaki zake.
 
zitto ninafiki na umaarufu wake umebaki kigoma ya dubai
 
zikishaisha kikao cha kk kitaitishwa na kujadili barua za utetezi wa wasaliti....na kutolea ufafanuzi hivyo siyo haraka kama unavyotaka tuamini...ila tunamfukuza..

Mnajichanganya tu na muda unavyoenda mtapingana muda sio mrefu!!!!!

Hili halikuwa dharura kweli???!!!!
 
ndungu makamanda wenzangu, nashangazwa sana kuona makamanda walio wengi wamekuwa wakipambana na hao tunaosema ni ccm wanaomtetea zzk, huoni tunavyozidi kurushiana nao maneno ndio tunazidi kufanya mgogoro uonekane mkubwa? Tena ugomvi wa mtu mmoja na maelefu ya watu ndani ya taasisi?.

Hatuoni kadri tunavyozidi kukinzana na hao maccm ndio tunaonyesha nikweli tunachuki na zzt kabwe?.

Pia kama nihaki yakila mmoja kutoa hisia zake hata kama ni kamanda mwenzetu tunamuita ni ccm?
Kwanini tusingejikita kwa hoja nyingine za kujenga kuliko kila siku kuruhu hawa watu kuzidi kuwazodoa viongozi wetu wa taafa mfano dr. Slaa. Si kweli kwamba malengo yetu nikuonekana nani kamanda wa kweli nani asiye, bali ni kuvuka mpaka tufike ikulu 2015. Na sikweli kwamba sisi makanda tu ndio tutakaolivusha hili gurudumu mpaka ikulu, bali hata kuwashawishi hao wasio nasi ili watupatie kura.

Tunavyozidi kumchafua zitto kwa matusi kuna baadhi wataamini makamanda tulikuwa na chuki na zitto ambapo tutawakosa waliokuwa njia panda?
Nashauri tusubili maamuzi ya cc na sio sisi kubaki washabiki kama wa simba na yanga. Kunawengine wengi watamfuata kaseja japo tutajifariji kuwa waondoke tu kumbe ni pigo kubwa kwetu ili hali mda kuelekea 2015 unakaribia.

Ndugu zangu tusipo vuka 2015 watu watakata tamaa na tutapoteza wengi maana sasa wengi wanamatumaini makubwa ya mabadiliko. Nimda mwaafaka kuonza wafuasi na si kuwapoteza kwa kuhendekeza mgogoro.
 
Back
Top Bottom