Salaam,
Napenda kuisihi CC ya CHADEMA iitishe kikao cha dharula cha kujadili barua ya utetezi dhidi ya mashitaka yanayomkabili Zitto; na mwishowe imvue uanachama na hivyo kupoteza ubunge wake.
Ni wazi CHADEMA imemvumilia huyu jamaa kwa muda mrefu licha ya harakati zake ambazo amekuwa akizifanya za kuzoofisha chama kwa miaka kadhaa. Sina sababu ya kurudia kuzitaja harakati hizo ambazo zinafahamika na kila mmoja.
Hapa naihasa tu CHADEMA ichukue maamuzi ya haraka sana ya kumvua uanachama ndugu Zitto, la sivyo ataendelea kuleta madhara ndani ya chama kama akiendelea kuchekewa.
Nilitarajia mtu ambaye ameshitakiwa hata kama ni kwa kuonewa, awe mtulivu ili kusubiri hatma yake. Badala yake huyu jamaa kwa kushirikiana na "washirika" wake, ameendelea na harakati zake haramu za kuleta mitafaruku na kutukana viongozi wa juu wa chama. Safari hii akifanya hivyo "mchana kweupee". Mshirika mkuu akiwa Albati Msando ambaye naye amekuwa akisambaza jumbe za kutukana na kubeza viongozi kwenye mitandao ya kijamii.
Nasema CC imtimue Zitto haraka sana. Madhara yake akiwa nje ni madogo kuliko "spoil" anayoifanya sasa akiwa ndani ya chama.
Wasalaam.