ZZK haeleweki, kwanini asitoe kauli kuhusu hawa CCM kuleta propaganda ya kuipotosha jamii.
Wajinga hawa tukiwaacha watu watadanganywa sana.
Dawa ni kupambana nao daima. Hii ni sawa na vita. Muhimu ni kujenga hoja dhidi ya propaganda.
Siyo kazi rahisi kama unavyowaza wewe,cc ya chadema ilishajua suala la Zitto ni kaa la moto si la kulichezea kizembe linaweza kuchoma chamaTaratiibu sumu za ZZK zinaanza kutuingia baadhi ya wanachama na kuanza kuamini huenda zzk katengenezewa zengwe ndani ya chama. Wote tunaona harakati za huyu mtu,kwa harakaharaka tunaweza kudharau lakin anazidi kuongeza wafuasi,kwa walioangalia habari ya star tv mtaungana na mimi kuwa zzk anazidi kuongeza iman ya wanachama juu yake. Suala hili hakika litakigharimu sana chama kwa kuleta mgawanyiko mkubwa wa chama usio walazima. Binafsi naweza kusema Huenda CC ya chama ilikurupuka kufanya maamuzi ndo maana ina kigugumizi kuweka hitimisho la sinema hii. Wanachama wanaelekea kuchoka kutokana na ukimya wa uongozi wa chama huku upande wa pili ukizidi kutumia nafasi hii kujiimarisha zaidi. Binafsi siasa za chadema zimeanza kunichosha maneno mengi bila vitendo.
Yule balozi wa gongo Tanzania alisema mjadala wa zitto umefungwa lakini akipanda kwenye majukwaa ana lopoka habari za Zitto
Siongezi neno,wala sipunguzi neno,maneno yako yamejaa busara za hali ya juu,wataweweseka sana na huyo zzk
mbwa mzee hafundishwi mbinu mpya wakuu...........makengeza na kikongwe waondoke la sivyo watasimamisha wanachama wote wabaki wenyewe tu
hatuna mwana chadema mwenye akili kama zako acha kujikomba wewe gamba.
ndungu makamanda wenzangu, nashangazwa sana kuona makamanda walio wengi wamekuwa wakipambana na hao tunaosema ni ccm wanaomtetea zzk, huoni tunavyozidi kurushiana nao maneno ndio tunazidi kufanya mgogoro uonekane mkubwa? Tena ugomvi wa mtu mmoja na maelefu ya watu ndani ya taasisi?.
Hatuoni kadri tunavyozidi kukinzana na hao maccm ndio tunaonyesha nikweli tunachuki na zzt kabwe?.
Pia kama nihaki yakila mmoja kutoa hisia zake hata kama ni kamanda mwenzetu tunamuita ni ccm?
Kwanini tusingejikita kwa hoja nyingine za kujenga kuliko kila siku kuruhu hawa watu kuzidi kuwazodoa viongozi wetu wa taafa mfano dr. Slaa. Si kweli kwamba malengo yetu nikuonekana nani kamanda wa kweli nani asiye, bali ni kuvuka mpaka tufike ikulu 2015. Na sikweli kwamba sisi makanda tu ndio tutakaolivusha hili gurudumu mpaka ikulu, bali hata kuwashawishi hao wasio nasi ili watupatie kura.
Tunavyozidi kumchafua zitto kwa matusi kuna baadhi wataamini makamanda tulikuwa na chuki na zitto ambapo tutawakosa waliokuwa njia panda?
Nashauri tusubili maamuzi ya cc na sio sisi kubaki washabiki kama wa simba na yanga. Kunawengine wengi watamfuata kaseja japo tutajifariji kuwa waondoke tu kumbe ni pigo kubwa kwetu ili hali mda kuelekea 2015 unakaribia.
Ndugu zangu tusipo vuka 2015 watu watakata tamaa na tutapoteza wengi maana sasa wengi wanamatumaini makubwa ya mabadiliko. Nimda mwaafaka kuonza wafuasi na si kuwapoteza kwa kuhendekeza mgogoro.
Uongozi wa Chadema unamuogopa Zito, huu ni ukweli tunaoanza kuuamini sisi wafuasi na wanachama wa Chadema. Uongozi wa Chadema ni waoga wa kufanya maamuzi kila linapokuja swala linalomhusu Zitto Kabwe Ikumbukwe ya kuwa vurugu za zito zilianza tangu mwaka 2007.
Mnafukuza viongozi wa mikoa, wilaya mpaka tawi lakini Zito mnaogopa kumfukuza. Kanuni na taratibu za chama zinazovunjwa na viongozi hao wa mkoa, wilaya mpaka tawi ndizo hizo hizo zinazovunjwa na Zito Zuberi Kabwe tena hadharani bila kificho. Hatua ya kumpoka wadhifa wake ndani ya chama ninyi mnaita maamuzi magumu wakati wapinzani wetu ccm wanafukuza mawaziri wake ndani ya serikali nao sijui waitaje? Kweli Zito ni mzito hata ndani ya chadema.
Dharau, kiburi na jeuri anayoonyesha zito kwa uongozi wa chadema naamini angekuwa ccm angekuwa ameshashika njia ya kutokea. Tukumbuke kiburi cha Sita aliishia kulia na kuomba msamaha ndani ya vikao vya chama. Lowasa ana nguvu ya fedha, siasa na amewahi kufukuzwa uwaziri mkuu lakini humsikii akisimama jukwaani, mitandaoni au popote pale akikashifu chama ama viongozi wake lkn zito anafanya hivyo bila kuchukuliwa hatua yeyote huku akisema hakuna wa kumfukuza chadema. Utetezi wa uongozi wa chama unadai kuwa unafuata taratibu za chama lkn walipomvua madaraka yake walidai kuna kifungu kinawaruhusu kufanya hivyo kwa dharula endapo wakiona jambo hilo kama litaadhiri chama, je yanayofanywa na kutamkwa na Zito Kabwe hayaathiri chama? kushirikiana na vibaraka wa ccm kama wakina mtela mwampamba katika mikutano yake hakuathiri chama?. Mbowe, Dr. Slaa, Mnyika, Lema, Msigwa, Mdee, Lisu na kamati kuu kwa ujumla ni vyema mkakiri kuwa Zito amewashinda wanachama tukajua tusimame katika mtazamo upi.​
Kushindwa kuchukua hatua kwa muda muafaka ni kushindwa kuwajibika pia.
Taratiibu sumu za ZZK zinaanza kutuingia baadhi ya wanachama na kuanza kuamini huenda zzk katengenezewa zengwe ndani ya chama.
Wote tunaona harakati za huyu mtu,kwa harakaharaka tunaweza kudharau lakin anazidi kuongeza wafuasi,kwa walioangalia habari ya star tv mtaungana na mimi kuwa zzk anazidi kuongeza iman ya wanachama juu yake.
Suala hili hakika litakigharimu sana chama kwa kuleta mgawanyiko mkubwa wa chama usio walazima.
Binafsi naweza kusema Huenda CC ya chama ilikurupuka kufanya maamuzi ndo maana ina kigugumizi kuweka hitimisho la sinema hii.
Wanachama wanaelekea kuchoka kutokana na ukimya wa uongozi wa chama huku upande wa pili ukizidi kutumia nafasi hii kujiimarisha zaidi.
Binafsi siasa za chadema zimeanza kunichosha maneno mengi bila vitendo.