Siasa ni mfumo wa maisha, hakuna namna mtanzania ataacha kujihusisha na siasa.Tuwaache waongee,wakosoe. Uzalendo na maslahi ya taifa yazingatiwe

masare

JF-Expert Member
Oct 12, 2010
1,231
1,363
Wanabodi
Nianze kwa kuchukua tafsiri ya neno Siasa kutoka Wikipedia Dictionary

Politics (from Ancient Greek πολιτικά (politiká) is the set of activities that are associated with making decisions in groups, or other forms of power relations among individuals, such as the distribution of resources or status.

Ukiangalia tafsiri hiyo utakubaliana kuwa Politics is a system of life. Yaani Siasa ni mfumo wa maisha. Siasa ndiyo inayoamua usome wapi,ule nini,uishi wapi,ulipe kodi kiasi gani,ulipwe pensheni kiasi gani n.k.

Ni ngumu kumwambia mtu asijihusishe na Siasa wakati mfumo wake wa maisha unaathiriwa moja kwa moja na Siasa.

Suala la Bandari ni mojawapo ya mambo ya kisiasa yanayomhusu mlipa kodi mtanzania hivyo kila mtu ana haki ya kulizungumzia na kutoa maoni yake regardless of any status.

Umeanza mtindo sikuhizi wa kuwataja viongozi wa dini pamoja na baadhi ya makundi kwenye jamiiyetu kwamba wasijihusishe na mambo ya siasa.Kiuhalisia ni ngumu kuwazuia wasijihusishe na Siasa kwasababu Siasa ndio maisha yenyewe.Utamzuiaje mtu asiongelee rasilimali za nchiyake...huo sio uzalendo.

Tuache watu waongee....demokrasia ichukue mkondo wake

MUNGU IBARIKI TANZANIA
 
Nakumbuka nikiwa shule tulijaribu kuhoji kuhusu ufundishaji mbovu na uvivu wa baadhi ya walimu, matokeo yake, tukaambiwa msilete siasa kwenye Elimu mtaangukia pua, ole wenu mjifanye much know!!!
 
Back
Top Bottom