Siasa na Pesa: Wananchi wengi wamechagua Pesa

Countrywide

JF-Expert Member
Mar 2, 2015
18,210
27,268
Mambo ni zaidi ya moto, Mama anaupiga mwingi sana. Nilijua na najua kuwa Mama Samia ana akili nyingi sana Ila sikujua kwa kiwango hiki. Ana IQ kubwa sana.

Kitendo cha kukataa mabaradhuli kuzunguka mtaani kupiga porojo za siasa ikiwa wananchi wake hawana Pesa ni kitendo cha kishujaa na kinapaswa kuigwa na maraisi wote duniani.

Watu hawataki porojo za siasa, wanataka pesa. Uchumi wa nchi ndio kila kitu, hizo porojo za siasa kwanza husababisha uvunjifu wa amani na hafa husababisha wawekezaji wasije.

Mama Samia shikilia hapo hapo, wananchi tulio wengi tunakuelewa sana. Mahitaji ya nchi hii sio katiba wala mikutano ya siasa, na Wala sio tume huru. Mahitaji yetu ni uchumi kukua.

Narudia tena wananchi hatuhitaji katiba, wala time huru wala mikutano ya siasa BALI tunahitaji uchumi kukua.

Mama Samia shikamoo, shikilia hapo hapo mama. Hawa walitaka kukujaribu bila kujua kuwa hujaribiwi.

Kazi iendelee, siasa fanyeni kwenye vikao vyenu hivyo vya saccos
 
Back
Top Bottom