vibertz
JF-Expert Member
- Mar 15, 2022
- 1,382
- 2,525
Kuna wimbi la mashabiki, wachambuzi na wadau wa soka wakihoji uhalali wa goli la tano. Kwa wenzetu walioendelea mambo kama haya yameshapitwa na wakati ila kwa nchi zetu za kimasikini bado tumeshindwa kuendana na teknolojia.
Watu tumepiga kelele sana humu juu ya uchache wa camera za Azam, lile tukio kwa vituo vilivyopiga hatua huwa wanajaribu kuangalia angle sahihi ya kuonesha position ya mpira kama ulivuka mstari au ulikuwa nje ya mstari ila Azam wana replay, replay tu pasipo kuzingatia angle sahihi inayoweza kuondoa utata na watu wote wakaondoka na jibu moja kuwa eidha mpira ulikuwa nje au mpira ulikuwa upo ndani.
Kuna matukio mengine ya mfano offside, Azam bado wanashindwa kututendea haki watazamaji wake kwa kufanya replay kwa kutumia angle sahihi kisha wakachora mstari wa offside position ili watazamaji waondoke na jibu moja kulingana na marejeo. Badala yake wataonesha marejeo isiyo na angle sahihi kisha mtazamaji apime kwa macho yake kama mchezaji kazidi au lah.
Tunaomba msimu unaokuja Azam muende na wakati, mmefanya makubwa katika kui brand ligi yetu na kuifanya ifatiliwe na watu wa mataifa tofauti tofauti hivyo ni wakati wa kwenda sambamba na ukuaji wa teknolojia, angalieni supersport, kukiwa na utata wa mpira kuvuka au kutovuka goal line wanavyofanya replay inayomaliza utata kabisa pale pale mchezoni. Unaona kabisa position ya mpira pale pale uliopo mstari tena tukio linachukuliwa kwa ukaribu kabisa.
Lakini tukio la jana kila mtu kaondoka na jibu lake, wengine goli wengine sio goli hiyo yote inatokana na Azam kushindwa kuondoa utata wa tukio.
Hii chini ni moja ya video inaonesha ule mpira uliingia ndani, lakini bado video haikuwa na kiwango cha kufuta utata kivile.
View attachment 2932460