Siamini katika Karma, Watu wengi wamewafanyia ubaya wengine na wanazidi kupasua anga

R-K-O

JF-Expert Member
Jun 27, 2023
482
2,138
Karma limekuwa neno maarufu Sana likitumika kumaanisha usimfanyie mwenzako ubaya, maana na wewe utalipwa ubaya. (Malipo hapahapa Duniani)

Binafsi siamini katika hili, nahisi ni imani tu iliwekwa ili kupunguza uovu, ila kiuhalisia mambo ni tofauti

Nakumbuka kulikuwa na wababe wale waonezi mashuleni, ni kweli baadhi yao maisha yamewapiga lakini pia wapo wengi tu wana afya nzuri, kazi nzuri, familia, n.k.

Matajiri wapo wengi wametajirika kwa dhulma, wengine yamewakuta ila wapo wengi pia ambao ni vizazi sasa mambo yapo fresh kabisa

Wahusika wengine ni sisi wenyewe tunaojijua kila kitu tunajijua tuliwahi kuwafanyia ubaya wengine lakini mambo yanakwenda sawia.
 
Haujui undani wa mtu kwa kuwa tu unaona evil people wakikenua kenua meno kwenye media pamoja na mabaya yote waliofanya usifikirie kwamba wako happy na wana amani, wengi wao wana maisha ya shida siyo material things lkn kiroho na hawana furaha maishani mwao hata usingizi hawalali vizuri na ndiyo maana kila siku unawaona wakipambana kujaribu kubakia relevant unafikiri ni kwa nini?

Angalia mtu kama uhuru kenyata unafikiri ana amani moyoni mwake? Ulishajiuliza anahangaikia nini kama alishakuwa tayari raisi kwa miaka 10 na utajiri usioelezeka? Kwa nini raisi mstaafu anakimbizana na polisi leo hii ambao alikuwa anawa command?

Karma is real …
 
Mbona jibu unalo, Wanapasua ili na ww uwafatishe njia zao.

Fedha zina siri sana sana sana, ili kuzipata fedha lazima uchague pande either hasi au chanya vinginevo ukijitaidi sana utishia kupata pesa tu.

Kingine familia ziko tofauti tofauti, malezi tofauti na sheri tofauti pia na impact yake hua tofauti, wengine mafanikia yao au kuanguka kwao ni kwaajili ya ya wazazi wake tu na si yeye
 
Karma limekuwa neno maarufu Sana likitumika kumaanisha usimfanyie mwenzako ubaya, maana na wewe utalipwa ubaya. (Malipo hapahapa Duniani)

Binafsi siamini katika hili, nahisi ni imani tu iliwekwa ili kupunguza uovu, ila kiuhalisia mambo ni tofauti

Nakumbuka kulikuwa na wababe wale waonezi mashuleni, ni kweli baadhi yao maisha yamewapiga lakini pia wapo wengi tu wana afya nzuri, kazi nzuri, familia, n.k.

Matajiri wapo wengi wametajirika kwa dhulma, wengine yamewakuta ila wapo wengi pia ambao ni vizazi sasa mambo yapo fresh kabisa

Wahusika wengine ni sisi wenyewe tunaojijua kila kitu tunajijua tuliwahi kuwafanyia ubaya wengine lakini mambo yanakwenda sawia .
Mi nnaichukulia katika namna ya tofauti.

Nachukulia kwamba ile itikadi ya mtu na mantiki zake anavyoendesha maisha yake ndivyo seli zilizopo mwilini mwake zinaiga.

Nnaiweka kiafya zaidi. So karma ina matokeo katika afya ya mtu binafsi.

Mfano, mtu ambaye atafanya lolote, liwe baya liwe zuri ili ajikusanyie hela mingi. Yena haswa kwa kuwawekea wengine mazingira magumu ya kuzitumia hizo pesa eti kisa yeye ni mjanja na mwerevu. Basi ana hatari ya kupatwa na kisukari.

Why?

Kwa sababu seli za mwili wake zitaiga mtindo huo. Ubongo ambao ni mwerevu utajikusanyia sukari yote na kuiweka kwenye damu. Kisha utaongoza mifumo kuzuia misuli na ogani nyingine sisitumie sukari kikamilifu. Huo ndio utaitwa ugonjwa wa kisukari.

Mtu hatapatwa na kisukari kama katika utafutaji wake wa pesa ni fair, kila mwenye uhitaji na haki anapata nafasi ya kutumia sukari/pesa ki usawa na uhitaji. Afya itamtawala kijamii na kimwili.

So anayepiga na kumuonea kila aliye mdogo kwake, basi na seli za mwilini mwake zitaiga na kupigana kila mara. Afya yake itakuwa hivyo.

Basi hii ndio nadharia yangu ya karma.
 
Karma limekuwa neno maarufu Sana likitumika kumaanisha usimfanyie mwenzako ubaya, maana na wewe utalipwa ubaya. (Malipo hapahapa Duniani)

Binafsi siamini katika hili, nahisi ni imani tu iliwekwa ili kupunguza uovu, ila kiuhalisia mambo ni tofauti

Nakumbuka kulikuwa na wababe wale waonezi mashuleni, ni kweli baadhi yao maisha yamewapiga lakini pia wapo wengi tu wana afya nzuri, kazi nzuri, familia, n.k.

Matajiri wapo wengi wametajirika kwa dhulma, wengine yamewakuta ila wapo wengi pia ambao ni vizazi sasa mambo yapo fresh kabisa

Wahusika wengine ni sisi wenyewe tunaojijua kila kitu tunajijua tuliwahi kuwafanyia ubaya wengine lakini mambo yanakwenda sawia.
Duniani malipano, usipolipia hapa duniani lazima utalipia baada ya kifo.
 
Unachukua mda gani !. Karma ijalishi leo au kesho.
Nenda pale znz wanazifikisha haraka karma kuliko tanganyika ndio maana raisi wa anaogopa kufanya ujinga huko.
Muulize marehemu huyu
IMG_0126.jpg
 
Karma limekuwa neno maarufu Sana likitumika kumaanisha usimfanyie mwenzako ubaya, maana na wewe utalipwa ubaya. (Malipo hapahapa Duniani)

Binafsi siamini katika hili, nahisi ni imani tu iliwekwa ili kupunguza uovu, ila kiuhalisia mambo ni tofauti

Nakumbuka kulikuwa na wababe wale waonezi mashuleni, ni kweli baadhi yao maisha yamewapiga lakini pia wapo wengi tu wana afya nzuri, kazi nzuri, familia, n.k.

Matajiri wapo wengi wametajirika kwa dhulma, wengine yamewakuta ila wapo wengi pia ambao ni vizazi sasa mambo yapo fresh kabisa

Wahusika wengine ni sisi wenyewe tunaojijua kila kitu tunajijua tuliwahi kuwafanyia ubaya wengine lakini mambo yanakwenda sawia.
Pascal Mayalla jibu hili...
 
Karma ipo na mimi nimeishuhudia ikiwakuta watu yale yale waliofanyia wenzao yaliwakuta wao.Kuhusu matajiri wala usidanganyike hakuna atakayekuonesha anachopitia hata siku moja ila uhalisia anaujua wenyewe.Ndio maana unaweza sikia mwingine kajiua,kaanguka kafa ghafla,kafilisiwa nk.Karma ipo na inafanya kazi kwa wakati wake!
 
Mkuu Proved , asante kunistua.
Karma limekuwa neno maarufu Sana likitumika kumaanisha usimfanyie mwenzako ubaya, maana na wewe utalipwa ubaya. (Malipo hapahapa Duniani)
True
Binafsi siamini katika hili, nahisi ni imani tu
Sii kweli karma is real!.
iliwekwa ili kupunguza uovu, ila kiuhalisia mambo ni tofauti
Kilichowekwa kupunguza tuu uovu ni dini!
Nakumbuka kulikuwa na wababe wale waonezi mashuleni, ni kweli baadhi yao maisha yamewapiga lakini pia wapo wengi tu wana afya nzuri, kazi nzuri, familia, n.k.
Ni kweli
Matajiri wapo wengi wametajirika kwa dhulma, wengine yamewakuta ila wapo wengi pia ambao ni vizazi sasa mambo yapo fresh kabisa
Pia ni kweli
Wahusika wengine ni sisi wenyewe tunaojijua kila kitu tunajijua tuliwahi kuwafanyia ubaya wengine lakini mambo yanakwenda sawia.
Ni kweli,
Kwa kuanzia karibu mitaa hii "The Power of 'Karma'- Ndio Hukumu Pekee ya Haki Kamili Hapa Duniani!, Unahukumiwa kwa Matendo Yako!
Kuhusu karma
  1. Karma is real na malipo ni hapa hapa duniani!.
  2. Karma is reversible, unaweza kufanya uovu, halafu ukafanya wema mkubwa kuliko ule uovu, hivyo unakuwa umeifuta ile bad karma na unabarikiwa!.
  3. Karma is transferable, ukifanya uovu halafu ukafa bila kulipa deni la karma, deni hilo linahamia kwa uzao wako up to 4 generations!.
  4. Karma is multiplied three folds, unaweza kufanya wema mdogo ukalipwa wema mkubwa three folds!, na unaweza kufanya ubaya mdogo tuu, lakini ukapigwa mapigo ya karma makubwa ajabu.
P
 
Ndio maana wachawi wanakua wema sana
 
Tatizo karma tunaitarajia iwe kama switch yani ukiwasha taa iwake na ukizime na taa nayo izime.

Karma ina njia nyingi ya kutokea. Yule unaehisi ana enjoy utajiri baada ya kudhulumu unaweza kuta ana madhila makubwa kuliko hata fukara asie na kitu.
 
Mi nnaichukulia katika namna ya tofauti.

Nachukulia kwamba ile itikadi ya mtu na mantiki zake anavyoendesha maisha yake ndivyo seli zilizopo mwilini mwake zinaiga.

Nnaiweka kiafya zaidi. So karma ina matokeo katika afya ya mtu binafsi.

Mfano, mtu ambaye atafanya lolote, liwe baya liwe zuri ili ajikusanyie hela mingi. Yena haswa kwa kuwawekea wengine mazingira magumu ya kuzitumia hizo pesa eti kisa yeye ni mjanja na mwerevu. Basi ana hatari ya kupatwa na kisukari.

Why?

Kwa sababu seli za mwili wake zitaiga mtindo huo. Ubongo ambao ni mwerevu utajikusanyia sukari yote na kuiweka kwenye damu. Kisha utaongoza mifumo kuzuia misuli na ogani nyingine sisitumie sukari kikamilifu. Huo ndio utaitwa ugonjwa wa kisukari.

Mtu hatapatwa na kisukari kama katika utafutaji wake wa pesa ni fair, kila mwenye uhitaji na haki anapata nafasi ya kutumia sukari/pesa ki usawa na uhitaji. Afya itamtawala kijamii na kimwili.

So anayepiga na kumuonea kila aliye mdogo kwake, basi na seli za mwilini mwake zitaiga na kupigana kila mara. Afya yake itakuwa hivyo.

Basi hii ndio nadharia yangu ya karma.

Ngoja niisome Taratibu.
Watu wenye kuwaza beyond jf bado wapo.
 
Karma limekuwa neno maarufu Sana likitumika kumaanisha usimfanyie mwenzako ubaya, maana na wewe utalipwa ubaya. (Malipo hapahapa Duniani)

Binafsi siamini katika hili, nahisi ni imani tu iliwekwa ili kupunguza uovu, ila kiuhalisia mambo ni tofauti

Nakumbuka kulikuwa na wababe wale waonezi mashuleni, ni kweli baadhi yao maisha yamewapiga lakini pia wapo wengi tu wana afya nzuri, kazi nzuri, familia, n.k.

Matajiri wapo wengi wametajirika kwa dhulma, wengine yamewakuta ila wapo wengi pia ambao ni vizazi sasa mambo yapo fresh kabisa

Wahusika wengine ni sisi wenyewe tunaojijua kila kitu tunajijua tuliwahi kuwafanyia ubaya wengine lakini mambo yanakwenda sawia.
Waswahili hawakukosea kabisa kusema siku za mwizi ni 40.
 
Karma is real Bro, ni swala la muda tu utakuja hapa kushuhudia, afu pia ina apply kulingana na intention, mtu anaweza akatenda jambo baya lakini intention yake haikuwa imekusudia uovu na mwingnie anaweza tenda mema ila intentionally amekusudia uovu, naweza kusema karma haitokei kulingana na kitendo ulichofanya bali hutokea kulingana na dhamira uliyonayo juu ya kitendo fulani.

Kuna watu wanaonekana wamefanikiwa sana kwa mtazamo wa macho lakini uhalisia wanaujua wenyewe.
 
Back
Top Bottom