KUNA “KARMA" HALAFU IPO “FATE"

Manyanza

JF-Expert Member
Nov 4, 2010
9,529
14,424
imeandikwa na Luqman Maloto
Source: Facebook page ya Luqman Maloto

KIFO cha Dk John Magufuli na kuingia madarakani kwa Rais Samia Suluhu Hassan ni Karma au Fate? Nimeanza na swali.
Karma tafsiri yake ni kuwa yanayomtokea binadamu ni matunda ya matendo yake ya nyuma. Fate ina maana kwamba yote yalishapangwa. Kila hatua ambayo mja huipiga ilishaamuliwa kabla hajazaliwa.
Ni ufafanuzi; kwamba mja hana uchaguzi mbele ya Fate (hatima). Kwamba umwonavyo mja na maisha yake, ndivyo alivyopangiwa kuishi kabla hajazaliwa. Anafuata rasimu iliyoandikwa kwa ajili yake.
Anavyoishi binadamu leo ni matokeo ya aliyoyatenda jana. Hiyo ndio Karma. Mantiki ni kuwa mja anaweza kuamua kesho yake iweje kulingana na matendo yake ya leo.
Baada ya ufafanuzi, sasa tafsiri wewe kuhusu kuondoka kwa Magufuli na kuingia kwa Samia. Je, ni Karma au Fate? Halafu mtafute Mungu ndani ya maneno hayo mawili. Dini na imani yako usiviweke mbali.
Seif Sharif Hamad aliyegombea urais wa Zanzibar mara sita bila mafanikio. Akawa analalamika anadhulumiwa. Alipokufa akasifiwa na kila mtu kwamba alikuwa nguzo ya amani na maridhiano katika siasa za Zanzibar. Kifo cha Seif, mazishi na mazingira yake ni Karma au Fate?
Raila Amolo Odinga, anayesifika kwa kuchonga barabara ya siasa na demokrasia Kenya, ameshindwa majaribio ya urais mara tano. Je, hiyo unaiweka kwenye kundi gani? Fate au Karma?
Tuachane na siasa; mtazame Mama Patrick, aliyeuza pombe za kienyeji ili mwanaye asome. Akauza mpaka nguo zake za kuvaa na samani za ndani, kukusanya fedha za ada ya mwanaye.
Patrick akahitimu chuo. Akampata mke na watoto. Patrick akasema hiyo ndio familia yake. Mama Patrick maisha yakawa magumu. Njaa ikamtesa. Matibabu hakupata. Mwanaye hakujali uwepo wa Mama aliyeyapambania maisha yake. Mama Patrick akafa na kinyongo.
Kisha, watoto wa Patrick wakakua. Wakasoma. Maisha yakawa mazuri tu. Siku za likizo Patrick na mkewe wanapelekewa wajukuu. Wanaishi uzee wenye raha.
Itafute Karma na Fate ndani ya Patrick na Mama yake. Je, iliandikwa Mama Patrick aishi kwa maumivu, alee kwa jasho halafu afe na kihoro? Je, kuna binadamu wameandikiwa maumivu maisha yao yote? Usimsahau Mungu. Yupo. Mimi naamini. Nawe amini!
Ni Karma? Kosa la Mama Patrick ni nini katika kuhakikisha mwanaye anakuwa mwanaume mwenye maisha bora? Malipo yake ni kutelekezwa? Mbona Patrick yeye uzeeni ana furaha, wanaye wanaishi naye vizuri? Karma ipo wapi? Ikiwa utashika Fate, je, kuna ambao wameandikiwa hatima nzuri hata kama walitelekeza wazazi?
Yule jambazi aliyeua na kupora mali za wengine. Ukafika wakati akaacha ujambazi. Mali alizopora akazifanya mtaji wa biashara. Akawa tajiri. Akamwelekea na Mungu. Akaitwa mchamungu. Mtoa sadaka na zaka. Akaishi vizuri. Alipokufa, alizikwa kwa heshima zote. Karma ilijificha wapi kwake?
Unapodaiwa, roho inakuwa juu kwa sababu ya uaminifu wako. Nafsi haitulii mpaka ulipe. Wewe unaowadai hawakulipi. Wanakudhulumu. Unajilalamikia mwenyewe: “Mbona mimi nadhulumiwa wakati sidhulumu cha wengine?” Karma ipo wapi? Kama ni Fate, je, wewe hatima yako ni kudhulumiwa na wengine?
Vipi Ben Saanane aliyepotezwa? Kama ni Karma, je, naye aliwahi kumpoteza mtu? Waliompoteza malipo yao nini? Ikiwa utasema kupotezwa kwa Ben ni Fate, je, aliandikiwa aishi na apotezwe akiwa kijana mdogo? Mungu aliumba waja ili wapotezwe na wengine?
Dhambi ya Azory Gwanda ni nini mpaka apotezwe ili tuseme Karma haikopeshi? Familia yake itavuna nini kama fidia? Waliohusika na kupotea kwake, nao wameshapotezwa au wanaendelea kudunda?
Yatafakari maisha na kila nukta ya mshale wa saa, oanisha na matukio ya siku na hata siku. Wangapi wanalia kwa uonevu? Kipi kinawapata wanaoonea wenzao?
Sina na wala sishawishi itikadi za kipagani kama Karl Max, ila dunia imekuwa na visa vingi vya ubabe. Na hatuoni wababe wakilipa gharama ya matendo yao. Wanaishi vizuri. Wanastarehe na familia zao.
Wazungu waliomfunga Nelson Mandela na wenzake 13 Afrika Kusini kwa miongo mitatu kasoro, waliondoka duniani na wakazikwa kwa heshima. Karma ipo wapi? Utasema ni Fate; kwa hiyo kuna watu waliandikiwa mwisho mzuri hata kama walitesa wenzao?
Mamia ya watoto waliouawa Soweto, Afrika Kusini, Juni 16, 1976, mbona wauaji hawakulipa gharama? Mwanafunzi wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT), Akwilina Akwilini, alipigwa risasi akiwa kwenye daladala. Bila hatia. Damu ya Akwilina ilikosa nguzo za haki mbele ya vyombo vya sheria. Aliyempiga risasi yupo salama.
Tupo kwenye nchi ambayo hakimu anatafsiri uamuzi wa kesi kwa pesa. Kuna waliofungwa kwa uonevu kwa sababu wenye fedha waliamua. Kisha, hakimu aliyetoa hukumu ya kikatili kwa hongo, muda unafika anastaafu. Anapewa kiinua mgongo. Aende akale akijipongeza kwa hukumu zake zilizojengwa kwa ushawishi wa rushwa. Halafu aliyeonewa anaendelea kusota jela.
Ukiielewa Karma, utaelewa kuwa ni ile ngano ya “malipo ni duniani”. Shughulisha ubongo kiduchu; hakimu aliyemhukumu kwa uonevu maskini dhidi ya tajiri. Maskini akapoteza ardhi yake. Hakimu analipwa mshahara na haki anauza ndani ya hukumu. Anapostaafu, analipwa stahiki na kwenda kustarehe na wajukuu.
Malipo duniani; huyo hakimu kalipwa nini, wakati muda wake ulipowadia alikufa na siku ya mazishi wasifu mrefu ulisomwa, ukimpamba kama mwanafamilia bora na mwenye mafanikio?
Ya hakimu tuseme ni Fate? Halafu tukubaliane kuwa kuna waja wameandikiwa kudhulumu haki za wengine, kutesa na kukatisha maisha ya wenzao, kisha wao mwisho wao uwe mzuri. Kwani dunia ina maana gani?
Mwaka 1944, majaji Wazungu, kwa sababu za kibaguzi, walimhukumu kifo mtoto mweusi, George Stinney Jr, aliyekuwa na umri wa miaka 14. George akanyongwa kwa kiti cha umeme.
George alipoteza maisha kwa dhuluma ya uhai wake. Majaji waliomhukumu George, walistaafu. Wakatunukiwa vyeti na fedha za mafao ya ustaafu. Miaka 70 baadaye, yaani mwaka 2014, Mahakama Marekani ilieleza kuwa hukumu ya George ya mwaka 1944, ilikuwa batili. Wakati huo, majaji wote waliomhukumu walikuwa wameshakufa. Na walizikwa kwa heshima.
Kuna mtu alimlawiti mke wa mfanyakazi wake. Mwenye mke akaja nyumbani kwangu kunililia yaliyomkuta. Miaka inapita. Agano la malipo duniani halijatimia. Je, mnataka kusema sina subira?
Huyohuyo aliyemlawiti mke wa mwenzake, alimlawiti pia kijana mmoja kisa hawara. Kijana aliyelawitiwa akaja nyumbani kwangu analia usiku. Alikuwa anatafuta maficho. Huyo mlawiti hivi sasa ni mbunge. Je, mnataka kunilaumu kuwa nampangia Mungu jinsi ya kufanya kazi?
Dunia ina maajabu hii. Kuna watenda dhambi jua halizami wanajikuta wameshalipa gharama ya matendo yao. Wengine miaka inakatika mpaka dhambi inapoteza maana ndio inagundulika. Na mtenda dhambi wala hakutani na Karma.
Wapo viumbe kosa moja wanakamatwa na wanakutana na adhabu. Wengine wanatenda makosa mpaka ile dhambi inageuka utaratibu wa maisha yao na hawakamatwi. Je, waliosema za mwizi arobaini walitumia vipimo gani? Mpaka hapo bado unaamini Karma au Fate?
Mfanyabiashara aliyemhujumu mwenzake, akaanguka na kufilisika. Mhujumu akaendelea kupeta. Utajiri ukashamiri. Namjua rafiki aliyekuwa na duka kubwa la nguo, leo anafanya kazi ngumu za kubeba zege sehemu za ujenzi. Aliyemsababishia anguko yupo vizuri. Ameshakuwa mfanyabishara mkubwa.
Viongozi wa dini wanazini na kondoo wao mpaka wanajirekodi video. Waumini nao wanaongezeka. Yupo aliyeshirikiana na muumini wake mwanamke kudhulumu nyumba ya mume. Kisha, “Mtu wa Mungu" akampa na mimba huyo mwanamke. Mume akapoteza mali, mke na akashuhudia mtoto asiye wake akizaliwa ndani ya ndoa yake.
Ni dunia ambayo viongozi wa kiroho wanavuna utajiri kwa kukusanya sadaka kutoka kwa kondoo maskini. Nyumba za ibada zimegeuzwa uwekezaji, mahubiri biashara, dua ni bidhaa inayouzwa. Je, Mungu ameruhusu jina lake lichezewe?
Kuna mambo yanatokea dunia ya leo na sayari haitikisiki, mpaka unahisi watu wa Lutu kwenye miji ya Sodoma na Gomora, walionewa kugeuzwa miamba ya chumvi. Hivi kweli kwa yanayoendelea ulimwengu tunaoishi, tuna usafi upi mbele ya kizazi cha Nuhu kilichoangamizwa?
Mimi ni mlowezi wa Dar es Salaam. Mzunguko wangu wa maisha hauniweki mbali na mizungu ya jiji. Nawajua matapeli wanaoliza watu kila uchwao kwa uganga feki. Na polisi ni wapambe wa matapeli hao.
Miaka inapita, matapeli wanajenga mahoteli na apartments na wanaimbwa kwenye nyimbo mbalimbali za wasanii. Karma ina subira sana eeh? Tuamini Fate? Kwamba wao hatima yao ni kula bata mpaka mwisho kwa maumivu ya wenzao waliowatapeli?
Mara nyingi maisha hayakupi matokeo kama methali ya Kiswahili “baada ya dhiki faraja". Wengine dhiki ipo kwenye damu na ngozi. Wanaishi nayo maisha yote. Wanapambana mchana na usiku, bila kuvuna faraja.
Maisha si kama filamu kwamba mwishoni jambazi lazima auawe, afungwe jela au akutane na joto ya jiwe mtaani. Kisha, aliyedhulumiwa anaibuka shujaa. Filamu huandikwa kwa matamanio ya mwandishi (binadamu). Huumba matukio na kutengeneza mwisho wenye faraja.
Ingekuwa maisha ya kila siku ni kama filamu, kusingekuwa na utapeli wala wizi, dhuluma na mauaji. Maana waandishi wa filamu hutengeneza mwisho wenye kuumiza kwa watenda maovu. Watu wabaya wangeogopa ubaya kuwarudia. Tatizo maisha ya kawaida hayatoi ahadi kuwa ukitenda uovu lazima ukurudie.
Rais wa 33 wa Marekani, Harry Truman, aliamrisha nyuklia kwenye miji ya Hiroshima na Nagasaki, Japan. Watu takriban 215,000 walipoteza maisha. Maelfu walipata ulemavu. Mbona hakuiona Karma? Alikufa taratibu akiwa na umri wa miaka 88. Natamani unielewe!
Wanasiasa wanasababisha machafuko, raia wasio na hatia ndio wanakufa. Kisha, wanasiasa wanaketi mezani kumaliza vita na kugawana mkate. Waliokufa hawana fidia. Kuna viongozi wengi sio halali lakini wanadunda. Wapo wanasiasa wananuka damu na haiwadhuru.
Ni Karma ni Fate, wewe chagua kuamini kipi. Mimi ni mtazamaji tu.
 
Hayati magufuli alifariki kifo cha kawaida tu. Sote tunajua alikuwa na ugonjwa wa moyo isingekuwa hivyo tungekuwa naye hadi leo hii.
Soma mpaka mwisho uelewe na hapo wewe nadhani hujaelewa huo vizuri mfano wa kifo cha Magufuli , je ndio riziki ya Rais Samia ilipangwa kupitia kifo cha Magufuli?
 
Mkuu hongera sana kwa uandishi mzuri na wenye kufikirisha!
 
nimei copy Facebook Mkuumjana humu kulikuwa na mada ya Karma leo katika kupita facebook nikaikuta hii ndio nikaamua share nanyi.
 
Unaakili kuliko mimi kheeeee 🥰🥰🥰 good work bro
 
Karma means action (Matendo) - ukiwa unatenda mema basi tegemea kuvuna mema na ukiwa unatenda mabaya tegemea mabaya kuambatana nawe.

Fate - "Hatma"......Kila mwanadamu hana hatma yake.

Kuhusu kifo cha Magufuli naweza kusema ni karma ndiyo iliyofanya kazi. Kwa sababu aliamua kutetea wanyonge kwa maneno pamoja na kwa vitendo (action=karma). Kitendo ambacho hakiku wapendeza mabeberu pamoja na mafisadi.

Alizuia wizi wa rasilimali za Taifa kwa vitendo(action=karma), kitendo ambacho kiliwaudhi mabeberu na kuamua kukatisha uhai wake.

Kuhusu mama ni katiba ndio iliyomuweka madarakani ayo mambo ya fate na kuachia wewe? 🤔
 
Karma is the most patient gangster ever
Gangster? Karma is a bitch inaweza ikakunufaisha au ikakupoteza inategemea unaitumiaje kwa manufaa ya nani?

Jambazi anaeua akwapue pesa ili akamlipie matibabu mama yake asife, unadhani ameitumiaje karma?

Mwanasiasa anaeiba fedha za umma matrillion ya dollar ili ajilimbikizie mali kwa manufaa ya yeye na kitukuu chake, ameitumiaje karma?
 
Mkuu karma, kama hutojali naomba uniachie ID yangu please bado naipenda, siyo amri lakini ni ombi
 
Write your reply... Naomba tafsiri za KARMA na FATE kwa kiswahili labda nitaelewa kitu
 
Karma tafsiri yake ni kuwa yanayomtokea binadamu ni matunda ya matendo yake ya nyuma.

Fate ina maana kwamba yote yalishapangwa. Kila hatua ambayo mja huipiga ilishaamuliwa kabla hajazaliwa
 
imeandikwa na Luqman Maloto
Source: Facebook page ya Luqman Maloto

KIFO cha Dk John Magufuli na kuingia madarakani kwa Rais Samia Suluhu Hassan ni Karma au Fate? Nimeanza na swali.
Karma tafsiri yake ni kuwa yanayomtokea binadamu ni matunda ya matendo yake ya nyuma. Fate ina maana kwamba yote yalishapangwa. Kila hatua ambayo mja huipiga ilishaamuliwa kabla hajazaliwa.
Ni ufafanuzi; kwamba mja hana uchaguzi mbele ya Fate (hatima). Kwamba umwonavyo mja na maisha yake, ndivyo alivyopangiwa kuishi kabla hajazaliwa. Anafuata rasimu iliyoandikwa kwa ajili yake.
Anavyoishi binadamu leo ni matokeo ya aliyoyatenda jana. Hiyo ndio Karma. Mantiki ni kuwa mja anaweza kuamua kesho yake iweje kulingana na matendo yake ya leo.
Baada ya ufafanuzi, sasa tafsiri wewe kuhusu kuondoka kwa Magufuli na kuingia kwa Samia. Je, ni Karma au Fate? Halafu mtafute Mungu ndani ya maneno hayo mawili. Dini na imani yako usiviweke mbali.
Seif Sharif Hamad aliyegombea urais wa Zanzibar mara sita bila mafanikio. Akawa analalamika anadhulumiwa. Alipokufa akasifiwa na kila mtu kwamba alikuwa nguzo ya amani na maridhiano katika siasa za Zanzibar. Kifo cha Seif, mazishi na mazingira yake ni Karma au Fate?
Raila Amolo Odinga, anayesifika kwa kuchonga barabara ya siasa na demokrasia Kenya, ameshindwa majaribio ya urais mara tano. Je, hiyo unaiweka kwenye kundi gani? Fate au Karma?
Tuachane na siasa; mtazame Mama Patrick, aliyeuza pombe za kienyeji ili mwanaye asome. Akauza mpaka nguo zake za kuvaa na samani za ndani, kukusanya fedha za ada ya mwanaye.
Patrick akahitimu chuo. Akampata mke na watoto. Patrick akasema hiyo ndio familia yake. Mama Patrick maisha yakawa magumu. Njaa ikamtesa. Matibabu hakupata. Mwanaye hakujali uwepo wa Mama aliyeyapambania maisha yake. Mama Patrick akafa na kinyongo.
Kisha, watoto wa Patrick wakakua. Wakasoma. Maisha yakawa mazuri tu. Siku za likizo Patrick na mkewe wanapelekewa wajukuu. Wanaishi uzee wenye raha.
Itafute Karma na Fate ndani ya Patrick na Mama yake. Je, iliandikwa Mama Patrick aishi kwa maumivu, alee kwa jasho halafu afe na kihoro? Je, kuna binadamu wameandikiwa maumivu maisha yao yote? Usimsahau Mungu. Yupo. Mimi naamini. Nawe amini!
Ni Karma? Kosa la Mama Patrick ni nini katika kuhakikisha mwanaye anakuwa mwanaume mwenye maisha bora? Malipo yake ni kutelekezwa? Mbona Patrick yeye uzeeni ana furaha, wanaye wanaishi naye vizuri? Karma ipo wapi? Ikiwa utashika Fate, je, kuna ambao wameandikiwa hatima nzuri hata kama walitelekeza wazazi?
Yule jambazi aliyeua na kupora mali za wengine. Ukafika wakati akaacha ujambazi. Mali alizopora akazifanya mtaji wa biashara. Akawa tajiri. Akamwelekea na Mungu. Akaitwa mchamungu. Mtoa sadaka na zaka. Akaishi vizuri. Alipokufa, alizikwa kwa heshima zote. Karma ilijificha wapi kwake?
Unapodaiwa, roho inakuwa juu kwa sababu ya uaminifu wako. Nafsi haitulii mpaka ulipe. Wewe unaowadai hawakulipi. Wanakudhulumu. Unajilalamikia mwenyewe: “Mbona mimi nadhulumiwa wakati sidhulumu cha wengine?” Karma ipo wapi? Kama ni Fate, je, wewe hatima yako ni kudhulumiwa na wengine?
Vipi Ben Saanane aliyepotezwa? Kama ni Karma, je, naye aliwahi kumpoteza mtu? Waliompoteza malipo yao nini? Ikiwa utasema kupotezwa kwa Ben ni Fate, je, aliandikiwa aishi na apotezwe akiwa kijana mdogo? Mungu aliumba waja ili wapotezwe na wengine?
Dhambi ya Azory Gwanda ni nini mpaka apotezwe ili tuseme Karma haikopeshi? Familia yake itavuna nini kama fidia? Waliohusika na kupotea kwake, nao wameshapotezwa au wanaendelea kudunda?
Yatafakari maisha na kila nukta ya mshale wa saa, oanisha na matukio ya siku na hata siku. Wangapi wanalia kwa uonevu? Kipi kinawapata wanaoonea wenzao?
Sina na wala sishawishi itikadi za kipagani kama Karl Max, ila dunia imekuwa na visa vingi vya ubabe. Na hatuoni wababe wakilipa gharama ya matendo yao. Wanaishi vizuri. Wanastarehe na familia zao.
Wazungu waliomfunga Nelson Mandela na wenzake 13 Afrika Kusini kwa miongo mitatu kasoro, waliondoka duniani na wakazikwa kwa heshima. Karma ipo wapi? Utasema ni Fate; kwa hiyo kuna watu waliandikiwa mwisho mzuri hata kama walitesa wenzao?
Mamia ya watoto waliouawa Soweto, Afrika Kusini, Juni 16, 1976, mbona wauaji hawakulipa gharama? Mwanafunzi wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT), Akwilina Akwilini, alipigwa risasi akiwa kwenye daladala. Bila hatia. Damu ya Akwilina ilikosa nguzo za haki mbele ya vyombo vya sheria. Aliyempiga risasi yupo salama.
Tupo kwenye nchi ambayo hakimu anatafsiri uamuzi wa kesi kwa pesa. Kuna waliofungwa kwa uonevu kwa sababu wenye fedha waliamua. Kisha, hakimu aliyetoa hukumu ya kikatili kwa hongo, muda unafika anastaafu. Anapewa kiinua mgongo. Aende akale akijipongeza kwa hukumu zake zilizojengwa kwa ushawishi wa rushwa. Halafu aliyeonewa anaendelea kusota jela.
Ukiielewa Karma, utaelewa kuwa ni ile ngano ya “malipo ni duniani”. Shughulisha ubongo kiduchu; hakimu aliyemhukumu kwa uonevu maskini dhidi ya tajiri. Maskini akapoteza ardhi yake. Hakimu analipwa mshahara na haki anauza ndani ya hukumu. Anapostaafu, analipwa stahiki na kwenda kustarehe na wajukuu.
Malipo duniani; huyo hakimu kalipwa nini, wakati muda wake ulipowadia alikufa na siku ya mazishi wasifu mrefu ulisomwa, ukimpamba kama mwanafamilia bora na mwenye mafanikio?
Ya hakimu tuseme ni Fate? Halafu tukubaliane kuwa kuna waja wameandikiwa kudhulumu haki za wengine, kutesa na kukatisha maisha ya wenzao, kisha wao mwisho wao uwe mzuri. Kwani dunia ina maana gani?
Mwaka 1944, majaji Wazungu, kwa sababu za kibaguzi, walimhukumu kifo mtoto mweusi, George Stinney Jr, aliyekuwa na umri wa miaka 14. George akanyongwa kwa kiti cha umeme.
George alipoteza maisha kwa dhuluma ya uhai wake. Majaji waliomhukumu George, walistaafu. Wakatunukiwa vyeti na fedha za mafao ya ustaafu. Miaka 70 baadaye, yaani mwaka 2014, Mahakama Marekani ilieleza kuwa hukumu ya George ya mwaka 1944, ilikuwa batili. Wakati huo, majaji wote waliomhukumu walikuwa wameshakufa. Na walizikwa kwa heshima.
Kuna mtu alimlawiti mke wa mfanyakazi wake. Mwenye mke akaja nyumbani kwangu kunililia yaliyomkuta. Miaka inapita. Agano la malipo duniani halijatimia. Je, mnataka kusema sina subira?
Huyohuyo aliyemlawiti mke wa mwenzake, alimlawiti pia kijana mmoja kisa hawara. Kijana aliyelawitiwa akaja nyumbani kwangu analia usiku. Alikuwa anatafuta maficho. Huyo mlawiti hivi sasa ni mbunge. Je, mnataka kunilaumu kuwa nampangia Mungu jinsi ya kufanya kazi?
Dunia ina maajabu hii. Kuna watenda dhambi jua halizami wanajikuta wameshalipa gharama ya matendo yao. Wengine miaka inakatika mpaka dhambi inapoteza maana ndio inagundulika. Na mtenda dhambi wala hakutani na Karma.
Wapo viumbe kosa moja wanakamatwa na wanakutana na adhabu. Wengine wanatenda makosa mpaka ile dhambi inageuka utaratibu wa maisha yao na hawakamatwi. Je, waliosema za mwizi arobaini walitumia vipimo gani? Mpaka hapo bado unaamini Karma au Fate?
Mfanyabiashara aliyemhujumu mwenzake, akaanguka na kufilisika. Mhujumu akaendelea kupeta. Utajiri ukashamiri. Namjua rafiki aliyekuwa na duka kubwa la nguo, leo anafanya kazi ngumu za kubeba zege sehemu za ujenzi. Aliyemsababishia anguko yupo vizuri. Ameshakuwa mfanyabishara mkubwa.
Viongozi wa dini wanazini na kondoo wao mpaka wanajirekodi video. Waumini nao wanaongezeka. Yupo aliyeshirikiana na muumini wake mwanamke kudhulumu nyumba ya mume. Kisha, “Mtu wa Mungu" akampa na mimba huyo mwanamke. Mume akapoteza mali, mke na akashuhudia mtoto asiye wake akizaliwa ndani ya ndoa yake.
Ni dunia ambayo viongozi wa kiroho wanavuna utajiri kwa kukusanya sadaka kutoka kwa kondoo maskini. Nyumba za ibada zimegeuzwa uwekezaji, mahubiri biashara, dua ni bidhaa inayouzwa. Je, Mungu ameruhusu jina lake lichezewe?
Kuna mambo yanatokea dunia ya leo na sayari haitikisiki, mpaka unahisi watu wa Lutu kwenye miji ya Sodoma na Gomora, walionewa kugeuzwa miamba ya chumvi. Hivi kweli kwa yanayoendelea ulimwengu tunaoishi, tuna usafi upi mbele ya kizazi cha Nuhu kilichoangamizwa?
Mimi ni mlowezi wa Dar es Salaam. Mzunguko wangu wa maisha hauniweki mbali na mizungu ya jiji. Nawajua matapeli wanaoliza watu kila uchwao kwa uganga feki. Na polisi ni wapambe wa matapeli hao.
Miaka inapita, matapeli wanajenga mahoteli na apartments na wanaimbwa kwenye nyimbo mbalimbali za wasanii. Karma ina subira sana eeh? Tuamini Fate? Kwamba wao hatima yao ni kula bata mpaka mwisho kwa maumivu ya wenzao waliowatapeli?
Mara nyingi maisha hayakupi matokeo kama methali ya Kiswahili “baada ya dhiki faraja". Wengine dhiki ipo kwenye damu na ngozi. Wanaishi nayo maisha yote. Wanapambana mchana na usiku, bila kuvuna faraja.
Maisha si kama filamu kwamba mwishoni jambazi lazima auawe, afungwe jela au akutane na joto ya jiwe mtaani. Kisha, aliyedhulumiwa anaibuka shujaa. Filamu huandikwa kwa matamanio ya mwandishi (binadamu). Huumba matukio na kutengeneza mwisho wenye faraja.
Ingekuwa maisha ya kila siku ni kama filamu, kusingekuwa na utapeli wala wizi, dhuluma na mauaji. Maana waandishi wa filamu hutengeneza mwisho wenye kuumiza kwa watenda maovu. Watu wabaya wangeogopa ubaya kuwarudia. Tatizo maisha ya kawaida hayatoi ahadi kuwa ukitenda uovu lazima ukurudie.
Rais wa 33 wa Marekani, Harry Truman, aliamrisha nyuklia kwenye miji ya Hiroshima na Nagasaki, Japan. Watu takriban 215,000 walipoteza maisha. Maelfu walipata ulemavu. Mbona hakuiona Karma? Alikufa taratibu akiwa na umri wa miaka 88. Natamani unielewe!
Wanasiasa wanasababisha machafuko, raia wasio na hatia ndio wanakufa. Kisha, wanasiasa wanaketi mezani kumaliza vita na kugawana mkate. Waliokufa hawana fidia. Kuna viongozi wengi sio halali lakini wanadunda. Wapo wanasiasa wananuka damu na haiwadhuru.
Ni Karma ni Fate, wewe chagua kuamini kipi. Mimi ni mtazamaji tu.
Inawezekana Kuna fate za namna mbili, Ile unayoweza ku-control na usiyoweza ku-control...mfano umejitafuta na kujipata na ukajua kusudi lako au unachokitaka katika maisha basi ni rahisi ku-control fate yako,ila Kuna namna unaweza kupitia aina Fulani ya maisha pasipo kujua( uncontrolled fate) kumbe ndo unaelekea kwenye fate yako na hapa ndo utasikia watu wanasema; "Ni Kwa Neema tu na Wala sio Kwa uwezo wangu" pale Mtu mambo yake yanapomwendea vizuri pengine pasipo kutarajia, au utasikia wanalalamika mikosi pale mambo yanapowakalia vibaya!
Kuhusu Karma,yes karma is real! Karma is timeless! Usipolipwa wewe kitalipwa Kizazi chako. Na nafikiri lengo la karma ni kutenda haki! "Whether we bring our enemies to justice or justice to our enemies, justice will be done" George W. Bush.
 
Back
Top Bottom