idriss
JF-Expert Member
- Mar 11, 2014
- 720
- 366
Okay naweza share experience yangu ingawa sitakua na exact details sababu nilikua kijana mduchu sana.Mbona kila anaeulizwa inafanyikaje hajibu!!! anabakia ooh.. uchawi ooh.. ushirikina
Nakumbuka Home Msimbazi st Kariakoo days back tulikua na mdrasa eneo la Uwani (Watoto wa Kariakoo, Ilala, Magoma wanazielewa hizi Madrasa za Vibarazani na Uwani)
Nakumbuka kipindi Madrasa tupo likizo walikuja watu kukadiria 10 hadi 15 wakivalia makanzu sambamba na Ustadh wetu , wameshika mijitabu asaa na makoro koro mengine yalionikodelesha macho kodo kodo.
Hao wakaingia zao madrasa.
Mara paulizwa : Enhee maalim Tia nia hao waizi liwapate Lipi?
Hilo jibu sasaa : Maalim Hao tumshitakie Allaah nati zilegee wende mbio kama gari lisilo sukani.
Baada ya makubaliano.
Kukaanza rindima sauti za visomo na chanting Qur'an si Qur'an yaani nlikua nasikia zogo tuu kwa kitambo kirefu asaa mpaka nikauchapa usingizi na Ushilawadu wangu.
Kustuka zamaani nimelazwa Chumbani kwangu na Kadadaa wetu wa Kazi[emoji23]
Nlipoamka mbio mpaka uwani mie tena[emoji85].
Kuingia Madrasa nikakuta sahani Ina sindano, Uzi mweusi, mbegu za mahindi, mtama, maharagwe yaani takribani zote za nafaka, Tura,manyoa sijui hata ya nini, mara fundo za vitambaa, ubani yaani tafrani.
Yale majitabu sikuyakuta.
Nilipouliza Kadadaa aniambia palikua pasomwa al badir kuna mtu alishtaki ameibiwa millioni Kumi na palitangazwa siku saba hakuna aliyejitokeza (ilikua miaka ya tisini).
Nilipokuja kukuwa nikasikia mambo hayo hayo so ni mule Mulee. [emoji3]