Rev. Kishoka
JF-Expert Member
- Mar 7, 2006
- 4,526
- 1,529
...
Si kipapai, kafara au malipo kwa kufuru ya ufisadi, bali ni barabara nyembamba na mbovu!
Mungu aziweke mahali pema roho za wote waliopoteza masha kwa ajali hizi na awape nguvu na afya walio majeruhi.
Rev. Kishoka,
Nakubaliana na mengine yote uliyoyandika isipokuwa hilo la kupanua barabara, je utapanua kama ile barabara ya Morogoro mpaka Mbeya ili iwe na lane ngapi? Je ni economically feasible kufanya hivyo? Tuna pesa za kufanya hivyo wakati robo tatu ya nchi yetu haina barabara za maana? Je hata tukipanua tutapunguza ajali? Ukiangalia barabara nzuri TZ ndio zinaongoza kwa ajali, yaani ile ya Dar mpaka Arusha na ya Dar mpaka Mbeya. Uk
Nafikiri muhimu kwa TZ ni alama barabarani, sheria za kubana madereva wanaokimbiza magari, ubora wa magari, ubora wa barabara kwamba zisiwe na mashimo ambayo yanaweza kusababisha ajali na elimu ya kutosha kwa madereva na watumiaji wengine wa barabara.
Nakubaliana nawe mchungaji wa kondoo wa bwana. Tatizo ni kuwa hawa jamaa wanapokuwa bungeni akili zao zinakwenda likizo. Labda wanaweza kujifunza katika hilo.
Lakini usishangae vilevile kusikia wanapendekeza bungeni kila mbunge apewe mkopo wa helikopta ili kuepuka ajali za barabarani. Hao ndio wabunge wetu.
mwanamalundi mbona hili limeshapendekezwa kuwa zitumike Dar kuwasafirisha viongozi kutoka uwanja wa ndege nk!
Talking about priorities!
Yaani tunahitaji watu kama 5 wengine wenye mtazamo kama wako, we are free to go ! maneno mazuri, yasiyo na siasa, viongozi wanakosolewa when needed, KWA KWELI NAKUPONGEZA KWA DHATI !
Pongezi zangu kwako haimaniishi serikali isikosolewe pale inapokosea, bali siasa ndio zisihusishwe na kila kitu !
Shukrani !
Kada, nami namshukuru sana ndugu Mtanzania kwa msimamo wake mzuri katika maswala ya usalama mabarabarani,(nikiwa katibu nitampa cheyo cha kusimamia hilo kama alivyo omba awali!! lol).
Kwenye wekundu hapo juu, tatizo siasa zimejipenyeza almost katika kila nyanja ya maisha ya Mtanzania... angalia na ikiwezekana toa mfano wa vitu ambavyo kama matukio ya kulalamikiwa havina links na siasa..
SteveD.
makamba ni kiongozi wa ccm na sio serikali ! tofautisheni vitu vingine bana !
kila kitu ccm mweeh !
siasa na wanasiasa ndio wanafanya maamuzi yote yakuhusu nchi na for now kila kitu kinatazamwa hivyo!
Kada, sikuelewi unaposema nitofautishe CCM na serikali. Wanaotengeneza sera (i.e., policies) ni akina nani??? kwa nini kikwete alipitia CCM ili kuingia ikulu??? Kikwete anatekeleza ilani ipi?? ni nani anatunza mafaili ya hiyo ilani??? Kada usinitie majaribuni, nikaanza kuhoji uelewa wako. Hata hivyo siamini kama ulichoandika hapo juu, ndicho ulichotaka kumaanisha. Naheshimu michango yako.
Mwafrika, the two are synchronized. You can never never, never separate them. Labda kuna watu wanafikiri bado tupo primary school.
Rev. Kishoka said:bali ni ubovu wa barabara zetu ulioandamana na sheria mbovu, ulafi wa wenye magari na kukosekana kwa nidhamu kwa madereva ambayo ungeambatana na mafunzo bora.
Sio hilo tu, vile vile magari mengi ambayo yako barabarani Tanzania hayastahili kuwepo barabarani. Serikali imejisahau kiasi kwamba njia kuu za usafiri wa uhakika kwa raia (Mizigo yao Mazao n.k.) imeachwa ifanywe kiholela pasipo uthibiti wa kutosha.