Si rahisi watu kufanana namna ya kufikiri na kutoa maoni! 'Critics' lazima ziwepo ili kufikia maendeleo endelevu!

Lanlady

JF-Expert Member
Feb 27, 2019
1,423
4,730
Kwamba kwenye nchi hii haitakiwi kuwa na maoni tofauti?
Kwamba kila mwenye maoni tofauti ni mpinzani wa maendeleo?

Basi watafukuzwa wengi!
Screenshot_20220823-083500_1.jpg
 
Enzi za Mwendazeke ukienda tu against na matakwa ya Serikali yake unapotezwa au unakula risasi hadharani.
Leo hii hadi viongozi wa Serikali wanaikosoa Serikali hiyo hiyo wanayotumikia bado mnalalamika? Kipindi kile mbona mlikuwa hamfungui midomo, badala yake mkakazana kuita watu wasaliti na wenye kutumiwa na mabeberu? Naunga mkono huyo jamaa kufukuzwa kazi mara moja, it's a serious misconduct na ni kinyume cha collective responsibility. Kama anaona mwajiri wake hafanyi vizuri angejiuzulu kwanza ndo aanze kutema cheche zake akiwa upinzani au raia huru asiyefungamana na mwajiri yeyote.
 
Kama anaona mwajiri wake hafanyi vizuri angejiuzulu kwanza ndo aanze kutema cheche zake akiwa upinzani au raia huru asiyefungamana na mwajiri yeyote.
Ni nani alijiuzulu enzi hizo ulizotaja?
Hata waliokuwa kinyume chake, wamekuja kukiri baadae

Ukiwa kiongozi ni afadhali sana upate watu wanaokukosoa hadharani, kuliko wanaokusubiri utoke au usiwepo kabisa duniani!

Tujifunze katika mema na si mabaya! Kukubali kukosolewa na kutoa ufafanuzi wa kina, ni kuonesha ukomavu!
 
Nilikuwa Twitter matusi kama yote,watu wanashindwa kukosoa kwa staha.
 
Back
Top Bottom