Si ni kasahau kubeba daftari la muandiko............aiseeeeeee eeeeeeeeeee

Si ni kasahau kubeba daftari la muandiko............aiseeeeeee eeeeeeeeeee

Mkuu.

Umenikumbusha mwalimu wangu wa Hisabati darasa la Tatu. Alitoa swali akasema "anayejua apite afanye ubaoni". Mtu mzima nikajipitisha, dah! nikashindwa kulifanya. Nilistukia bonge la kofi, akasema "nimesoma wanaojua, kama haujui kakae"

Niliumia sana rohoni. Alinifanya kuwa muoga wa kujaribu mambo.

Kuna wakati hata kuwatongoza wasichana nilikuwa naogopa. Aliniathiri kiakili.
Hahahahahahahahah uuuuui mungu wangu weeee hahahahahahahahahaha sipati picha mwenzenu
 
Ili sikika sauti ya mwanafunzi akisema jamani mwalimu(ke)......... anakuja, baada ya dakika kama mbili hivi daras lote(lanneB) lilikuwa kimya maana huyo mwalimu aliye semekana anakuja darasani kwakweli alisifika kwa kutembeze mkong'oto na hata kama ulikuwa umeshindikana lazima unyooke na wazazi wengi walipenda kuwakabidhi watoto wao kwa huyu Mwl maana hakika alikuwa anajua kuchunga kondoo wake zaidi ya Paloma anavyo mchunga sosoliso.

Ilipita nusu saa Mwl mwenyewe aliyesemekana anakuja aonekani, daaa kila mtu akasema bora asije tuu maana mtiti wake huyu ni bora ukutane na rungu la Paw siyo yule Mwl.. daaaaa tukaendelea kupiga story huku tukijua leo huyu Mwl kaona tupumzike maana alikuwa na vipindi vitatu kwa wiki na hakikosi hata kimoja.

Mara tulisikia mtu akiseama toeni madaftari yenu ya muandiko, daaa watu tukaanza kutafuta madaftari yetu tuweke juu ya meza japo dawati tulikuwa tumekalia watu wanne na lisingetosha kila mtu kutandika daftari lake pale, daaa wakati wenzangu wameshatoa madaftari yao, kwakweli mimi niliendelea kulitafuta bila mafanikio kwakweli nilihisi kizunguzungu kabisa maana nilijua leo nageuzwa kitoweo. Niliendelea kutafuta huku nikiwa kwenye mfuko wangu wa sport kwakweli kumbe daftari nililisahau nyumbani ooooooooooh jasho lilianza kunitoka asubuhi.........

Hile nainua kichwa kujiuliza nitafanya nini leo kwakweli nilikutana uso kwa uso na Mwl wangu wa muandiko na akaanza kuniliza Ruttashobolwa naomba unioneshe tulipo andika jana daaaaaaaaa niliaanza kutetemeka kama alivyo tetemeka Arushaone alipo fumaniwa na Lady doctor,akaniuliza tena daftari liko wapi? Ni kamwambia Mwl samahani nimelisahau,weeeeeeeeeeeee................alisisema unaniambia nini? “kwa hiyo leo somo langu hutoandika” nikamwambia nitaandika kwenye karatasi, akasema leo nitakufundisha jinsi ya kuwa makini na kutunza kumbu kumbu.

Aliniambia vua shati leo ndio litakuwa daftari lako, alaf akani hamisha kutoka kwenye dawati maana kwenyewe nilikuwa nimekalia kalio mmoja akanipeleka nikakae kwenye sakafu, nikavua shati huku watu wote kimya akaanza kuandika ubaoni na mimi naendelea kuandika kwenye shati na kila baada ya dakika anakuja kuangalia kama nina andika baada ya kumaliza kuandika tukaambiwa tupange mstari ili tusahishiwe daaaa nikapanga mstari na shati langu huku wenzangu wakitaka kuvunjika mbavu.

Ilipofika zamu yangu nikajua hawezi kuweka wino kwenye shati langu, kwakweli sikuamini kuona anasahihisha juu ya shati langu na akaniambia “kama una matatizo ya kusahau shati lako ndilo litakuwa daftari. Kwakweli tangu siku hiyo huyu mwal nilimuona kama simba na nilikuwa na beba daftari lake hata kama hana kipindi na ilinibidi niwe na beba madaftari yote kila siku.

Sikutegemea huyu Mwl kuja kuwa rafiki yangu na nilipo kuwa nikikutana nae baada ya kumaliza la saba aliniita na kuanza kunihoji unaendeleaje na masomo, kwakweli nilitokea kuanza kumkubali sana na kila likizo nilikuwa lazima niende kwake kumsalimu maana alinifunza kuwa makini na kujali.

Pongezi nyingi ziwafikie walimu wote, Nyinyi ni wa Muhimu sana.

Hapo kwenye red yametukuta saana na sasa ninayaona sana kwa wanafunzi looh.

Hapo kwenye blue kwa kweli kaka nimecheka saaana but na kahuzuni kidogo kamenishika

Kwenye green nimejikuta nikitoa machozi....sipati picha mama nyumbani alikupokeaje na shati lina mix ya blue and red colours.

All in all nimejifuza na ki ukweli huwa nawakumbuka sana walimu walionitoa ujinga. BIG UP sana WALIMU
 
umenikumbusha mwalimu wangu wa French wakati niko secondary....... Naye alikuwa kauzu ka nini, hadi nilitamani kutoingia kwenye pindi lake.....! Ila sasa najuta kwanini nilikuwa nampuuzia!!!!!!!!

Ha ha haa umenikumbusha mwalimu wangu wa FRENCH FORM II. Daah R.I.P Madam. Yaani yeye vipindi vyake vilikuwa vya mwisho then break ya chai.

Alikuwa anakija class na mfuko wa maandazi a.k.a viholonzo. Na camera yake..Atafudisha je ma pelle zakeee dkk 20, 60 zinazo baki zoote tunapiga picha na kununua maandazi. Anafunga mlango kabisa asibambwe.

Tena anahamasisha mbaya....maana usiponunua break time ukagombanie kwa wachuuzi. Viholonzo vikiisha anaanza le photooo yaani ile form two kwenda three robo tatu ya darasa lilikimbia FRENCH.

Kwake ilikuwa pesa mbele
 
Mkuu darasa la nne bado mlikua na somo la muandiko? Sisi muandiko ilikua darasa la 1 na la 2. Kuendelea mbele ilikua masomo ka siasa, sayansi kimu, jiografia, sayansi kilimo, hisabati nk. Anyway mimi ilinitokea STD VII nilisahau daftari la kiswahili halafu ticha mnoko balaa, wakati mtu anachapwa wengine mnaambiwa msogee mbali damu zisiturukie.
 
hahahaha mkuu asante kwa kunikumbusha nime edit hapo, daaa mwalimu wako alikuwa na mikwara sana. hahahaha umeniacha hoi eti damu zisiwarukie
 
Ha ha haa umenikumbusha mwalimu wangu wa FRENCH FORM II. Daah R.I.P Madam. Yaani yeye vipindi vyake vilikuwa vya mwisho then break ya chai.

Alikuwa anakija class na mfuko wa maandazi a.k.a viholonzo. Na camera yake..Atafudisha je ma pelle zakeee dkk 20, 60 zinazo baki zoote tunapiga picha na kununua maandazi. Anafunga mlango kabisa asibambwe.

Tena anahamasisha mbaya....maana usiponunua break time ukagombanie kwa wachuuzi. Viholonzo vikiisha anaanza le photooo yaani ile form two kwenda three robo tatu ya darasa lilikimbia FRENCH.

Kwake ilikuwa pesa mbele

hahahhahahahahahahaha umenikumbusha chips za miambili
 
Hapo kwenye red yametukuta saana na sasa ninayaona sana kwa wanafunzi looh.

Hapo kwenye blue kwa kweli kaka nimecheka saaana but na kahuzuni kidogo kamenishika

Kwenye green nimejikuta nikitoa machozi....sipati picha mama nyumbani alikupokeaje na shati lina mix ya blue and red colours.

All in all nimejifuza na ki ukweli huwa nawakumbuka sana walimu walionitoa ujinga. BIG UP sana WALIMU
hahahahaha
hahahahaha kwakweli sikuwai kukutana na mwl anaye fatilia kama huyu, unaweza kuomba kuhamishwa shule.
lakini mwisho wa siku walimu ni wa muhimu sana kwakweli nikimkumbuka huyu mwl kwakweli nasema kama angefundisha kipindi hiki hakika wanafunzi wange nyooka.
 
Wangenyooka au wangempeleka mahakmani kwa child abuse....siku hzi maadili hakuna kabisa na ukijaribu tu ku m discipline mwanafunzi utakomaje?
 
lol! huyu mwalimu kiboko!
maskini mwenyewe ukajua leo unarudi home na michirizi ya bakora...........kumbeeeee
 
hhahahaaa!!hako kauzembe kakushau
bado unako maana uanasahau mpaka familia yako
siku hizi! Lady doctor hivi ulishamkaguaga shem wako kweli?!!
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom