Leak
Platinum Member
- Feb 22, 2012
- 52,944
- 43,609
Ili sikika sauti ya mwanafunzi akisema jamani mwalimu(ke)......... anakuja, baada ya dakika kama mbili hivi daras lote lilikuwa kimya maana huyo mwalimu aliye semekana anakuja darasani kwakweli alisifika kwa kutembeze mkong'oto na hata kama ulikuwa umeshindikana lazima unyooke na wazazi wengi walipenda kuwakabidhi watoto wao kwa huyu Mwl maana hakika alikuwa anajua kuchunga kondoo wake zaidi ya Paloma anavyo mchunga sosoliso.
Ilipita nusu saa Mwl mwenyewe aliyesemekana anakuja aonekani, daaa kila mtu akasema bora asije tuu maana mtiti wake huyu ni bora ukutane na rungu la Paw siyo yule Mwl.. daaaaa tukaendelea kupiga story huku tukijua leo huyu Mwl kaona tupumzike maana alikuwa na vipindi vitatu kwa wiki na hakikosi hata kimoja.
Mara tulisikia mtu akiseama toeni madaftari yenu ya muandiko, daaa watu tukaanza kutafuta madaftari yetu tuweke juu ya meza japo dawati tulikuwa tumekalia watu wanne na lisingetosha kila mtu kutandika daftari lake pale, daaa wakati wenzangu wameshatoa madaftari yao, kwakweli mimi niliendelea kulitafuta bila mafanikio kwakweli nilihisi kizunguzungu kabisa maana nilijua leo nageuzwa kitoweo. Niliendelea kutafuta huku nikiwa kwenye mfuko wangu wa sport kwakweli kumbe daftari nililisahau nyumbani ooooooooooh jasho lilianza kunitoka asubuhi.........
Hile nainua kichwa kujiuliza nitafanya nini leo kwakweli nilikutana uso kwa uso na Mwl wangu wa muandiko na akaanza kuniliza Ruttashobolwa naomba unioneshe tulipo andika jana daaaaaaaaa niliaanza kutetemeka kama alivyo tetemeka Arushaone alipo fumaniwa na Lady doctor,akaniuliza tena daftari liko wapi? Ni kamwambia Mwl samahani nimelisahau,weeeeeeeeeeeee................alisisema unaniambia nini? "kwa hiyo leo somo langu hutoandika" nikamwambia nitaandika kwenye karatasi, akasema leo nitakufundisha jinsi ya kuwa makini na kutunza kumbu kumbu.
Aliniambia vua shati leo ndio litakuwa daftari lako, alaf akani hamisha kutoka kwenye dawati maana kwenyewe nilikuwa nimekalia kalio mmoja akanipeleka nikakae kwenye sakafu, nikavua shati huku watu wote kimya akaanza kuandika ubaoni na mimi naendelea kuandika kwenye shati na kila baada ya dakika anakuja kuangalia kama nina andika baada ya kumaliza kuandika tukaambiwa tupange mstari ili tusahishiwe daaaa nikapanga mstari na shati langu huku wenzangu wakitaka kuvunjika mbavu.
Ilipofika zamu yangu nikajua hawezi kuweka wino kwenye shati langu, kwakweli sikuamini kuona anasahihisha juu ya shati langu na akaniambia "kama una matatizo ya kusahau shati lako ndilo litakuwa daftari. Kwakweli tangu siku hiyo huyu mwal nilimuona kama simba na nilikuwa na beba daftari lake hata kama hana kipindi na ilinibidi niwe na beba madaftari yote kila siku.
Sikutegemea huyu Mwl kuja kuwa rafiki yangu na nilipo kuwa nikikutana nae baada ya kumaliza la saba aliniita na kuanza kunihoji unaendeleaje na masomo, kwakweli nilitokea kuanza kumkubali sana na kila likizo nilikuwa lazima niende kwake kumsalimu maana alinifunza kuwa makini na kujali.
Pongezi nyingi ziwafikie walimu wote, Nyinyi ni wa Muhimu sana.