Si Matakwa ya watawala kutuletea katiba mpya. Ni maagizo ya Wananchi

Fundi Madirisha

Senior Member
Jun 30, 2020
184
988
Si kazi ya watawala kuleta katiba ya wananchi, labda atokee mtawala mmoja akawa ni mwenye kutumia busara na hekima za kupitiliza kitu ambacho Afrika hakipo kabisa. Katiba mpya nyingi Afrika ni matokeo ya matukio mabaya ndio watawala huona na kukubali yaishe. Je, tunataka kwenda huko tulikozoea?

Hizi sababu za tujenge uchumi kwanza ni visingizio tu na katiba haijawahi kua kipaumbele kwa watawala bali ni mashinikizo ya wananchi na wanaharakati. Kwahiyo siyo jambo rahisi hivyo kama ambavyo wengi tunadhani na ndiyo maana gharama tunaziona, wengine wako magereza kwa tuhuma za ugaidi zisizoendana na ugaidi. Gharama ya kupata katiba mpya si ndogo kwa Afrika.

Niwadokeze hawa wapinzani wetu wanaopiga kelele kisha wakakaa kimya, katiba mpya siyo lelemama. Haiandikwi kwa watu kuvaa T-shirts zilizoandikwa katiba mpya vifuani au kuandika sana mitandaoni, ni matendo, ni mashinikizo kwa watawala wasioitaka na tayari wameonesha kua siyo kipaumbele kwao. Kuna gharama za kudai katiba mpya na ni lazima muwe tayari kwa hilo, anayopitia Mhe Mbowe ni kawaida na yalitarajiwa na wengi.
 
Back
Top Bottom