Si kila shari ni laana, kuna shari nyingine ni kheri

Suphian Juma

Senior Member
Apr 2, 2019
133
546
SI KILA SHARI NI LAANA, KUNA SHARI ZINGINE NI KHERI.

Nikiwa nasoma Shule ya Msingi na kwa muda mwingi baada ya kumaliza darasa la saba nilikuwa najishughulisha na biashara ya mbuzi na kuku kijijini kwetu Minyughe Mkoani Singida.

Kabla sijaenda kidato cha kwanza, nilipanga kisirisiri kutoroka nyumbani Singida kwenda Mjini Arusha kutafuta maisha kufuatia kasumba ya wakati huo kwamba wasomi wengi wa Sekondari hawana maisha bora kulinganisha na maisha ya wazamiaji wa mijini.

Bila kujua nikanunua mbuzi wawili wa wizi kwa mfanyabiashara mwenzangu. Mwizi aliyeniuzia alitoweka pasipojulikana. NIKAKAMATWA. Serikali ya Kijiji kwa kujua rekodi yangu nzuri ya kijamii na heshima ya Familia yangu ikaamuru kesi kurudishwa mahakama ya familia.

Baada ya mazungumzo ya familia mbili ikanibidi niwarudishe mbuzi kwa mmiliki bila faini. Mtaji wangu na hela za nauli zikaisha na safari ikakoma hapo.

Nikiwa nataka kuanza upya biashara, cha ajabu wiki iliyofuata matokeo ya darasa la Saba yakatoka na nikawa nimefaulu vizuri sana. Nikajiunga na Elimu ya Sekondari, na hivyo mawazo ya kutafuta kazi Mjini yakafa kifo cha kudumu.

Laiti nisingelipata janga hilo, huenda hadi leo nisingelikuwa hata na Elimu ya Sekondari wala Chuo Kikuu.

Mungu ana makundi yake katika kila mapito yako.

KUNA SHARI NI KHERI.

Suphian Juma Nkuwi.

FB_IMG_1694191049191.jpg
 
Back
Top Bottom