Si kila anaeenda dukani anatafuta pesa, Wengine wanaenda sababu wamechoka kukaa nyumbani, auze asiuze bado atakuja na gari na kula vizuri

R-K-O

JF-Expert Member
Jun 27, 2023
482
2,138
Katika sehemu nilizowahi kufanya biashara nimewahi kukutana na haya,

Sehemu ya kwanza kulikuwa na frem laki 3, mmama flani akaja akaweka vi choclate na vineti vya mbu yani hata wateja kwenda pale ni nadra, ila kila siku anakuja na gari yake ya apha na ananunua chakula kwa order ugali kuku, ikifika saa 11 jioni huyo anaondoka, ile sehem mara nyingi wenzake wanakuja wanapiga stori anawapa soda bure kabisa.

Sehemu ya pili jamaa flani anapiga kazi shirika la serikali alimpa mtaji mchepuko wake, huo mtaji akanunulia mabox ya nyembe za kunyolea nywele / ndevu pamoja na mabox ya vijiti vya kusafishia masikio, yani hapo dukani anaweza kufungua saa tatu na nusu ikifika saa tano huyo kaenda kwenye misele anawaambia maduka ya karibu wamuangalizie, hapo anarudi jioni, kwa mbali alijitahidi kuweka mdada hapo ofisini ila yeye kama kawa ikifika saa tano ni mwendo wa bata. akija mchana basi kaleta rafiki zake hapo kuwaonyesha duka lake kisha wanaondoka.

Mwengine kuna dogo alikuwa na miaka 22 hivi alilipiwa frem na mshua wake kipindi kamaliza chuo kama sio six nadhani, akaweka vinguo vichache tu , huyu dogo kwenda dukani ni saa nne, dukani kaweka play station na tv kubwa basi hapa marafiki zake wakija wanacheza sana, internet alikuwa analipia laki na nusu kila mwezi ya vodacom ihaina kikomo.

Sinza naskia ndio kufuru, ukiachan na aina ya watu kama niliowataja juu yapo makundi ya watakatisha fedha na wanaofanya shughuli haramu madukani.

  • a. ) watakatisha fedha - hawa wanaingiza pesa kwa njia zinazokiuka sheria aidha ujambazi, kuuza madawa, kudalalisha malaya, n.k, wameweka maduka haya yawe ya kutakatisha fedha hizo za shughuli za kando zionekane zimepatikana kihalali, mtu anakuwa mlipa kodi halali kabisa inaonekana pesa zake anapata kwa duka au maduka yake, kwa siku hata asipouza anatoa risiti feki kwamba kauza

  • b) waliogeuza maduka kufanyia shughuli haramu - mtu anatumia duka directly dukani hapo hapo ama indirectly kuuza bangi, unga, kudalalisha malaya, n.k. Sinza ni sehemu ina vijana wengi walau wenye uwezo wenye maisha ya mjini mjini wapo wanaopenda kutumia madawa, hapa mtu anaweza kutumia duka liwe stoo, mtu akihitaji anampelekea mzigo au kama kawa mteja wa mara kwa mara anamwambia awe anakuja dukani moja kwa moja, wengine haya maduka inakua vituo vya kununulia malaya, mwenye duka ndio dalali anachukua mgao wake. Ikifika jioni wenye hayo maduka wanapitia hesabu.

 
Katika sehemu mbili nilizowahi kufanya biashara nimewahi kukutana na haya,

Sehemu ya kwanza kulikuwa na frem laki 3, mmama flani akaja akaweka vi choclate na vineti vya mbu yani hata wateja kwenda pale ni nadra, ila kila siku anakuja na gari yake ya apha na ananunua chakula kwa order hizi kuku, ikifika saa 11 jioni huyo anaondoka, pale mara nyingi wenzake wanakuja wanapiga stori.

Sehemu ya pili kuna mchepuko wa mfanyabiashara flani alipewa mtaji, huo mtaji akanunulia mabox ya nyembe za kunyolea nywele / ndevy pamoja na mabox ya vijiti vya kusafishia masikio, yani hapo dukani anaweza kufungua saa tatu ikifika saa tano huyo kaenda kwenye misele anawaambia maduka ya karibu wamuangalizie anarudi jioni, sana sana alijitahisi kuweka tu mdada wa hapo ofisini ila yeye kama kawa ikifika saa tano ni mwendo wa bata. akija mchana basi kaleta rafiki zake hapo kuwaonyesha duka lake kisha wanaondoka.

Mwengine kuna dogo aliliiwa frem na mshua wake kipindi kamaliza form 6 wakati anasubiri kwenda chuo, huyu dogo kwenda dukani ni saa tano, dukani kaweka play station na tv kubwa hapa marafiki zake wakija wanacheza sana hadi jioni, internet ya vodacom ile isio na kikomo alikuwa nayo laki na nusu kila mwezi, duka lilikuwa na vinguo vichache tu.
Hio ndio tofauti ya mtoto wa Kibopa na hustler wa mtaa!
 
Halafu wana sifa moja, wenzao wakija watasifia sana biashara zao yani
Nakosaga majibu sana, kuna duka moja linaitwa "PATRICIA" karibu na wedding Lydia. Hilo duka tuliendaga shop mwezi February ila ajabu hadi leo mzigo tulioacha ni ule ule. Tusharudi more than once. Sasa unajiuliza ile biashara ina survive vipi kama haili hela za mtu tu 🤣?
 
Tofauti ni kwamba frame za sinza kuna plan B....trust me Sinz a is mine....najua kila angle,mtu..mikimbizano etc..!
Nakosaga majibu sana, kuna duka moja linaitwa "PATRICIA" karibu na wedding Lydia. Hilo duka tuliendaga shop mwezi February ila ajabu hadi leo mzigo tulioacha ni ule ule. Tusharudi more than once. Sasa unajiuliza ile biashara ina survive vipi kama haili hela za mtu tu 🤣?
 
Nakosaga majibu sana, kuna duka moja linaitwa "PATRICIA" karibu na wedding Lydia. Hilo duka tuliendaga shop mwezi February ila ajabu hadi leo mzigo tulioacha ni ule ule. Tusharudi more than once. Sasa unajiuliza ile biashara ina survive vipi kama haili hela za mtu tu 🤣?
Kutakuwa na jamaa wake ana kamshahara si haba ka kumpa 30 ya kila siku ila kamfungulia duka ili nae asiboreke kukaa nyumbani, hawezi kabisa kuumiza kichwa kwenye biashara wakati anajua kuna 30 ya kila siku.
 
🤣🤣🤣🤣🤣Dah ndio asibadili nguo na viatu hio ni biashara au ukichaa
Huyo nina uhakika kabisa hata Tin Namba na leseni sio zake na kama ni zake basi aliletewa hakuzitafuta yeye wala hajui jinsi ya kuzipata.

Trust me brother, aina hii ya watu ni sifuri kabisa kuhusu kujiongeza, hata kusema kuna wanafunzi wengi wanapita hio sehemu aweke auze hata kalamu, hilo wazo hana kabisa
 
Huyo nina uhakika kabisa hata Tin Namba na leseni sio zake na kama ni zake basi aliletewa hakuzitafuta yeye wala hajui jinsi ya kuzipata.

Trust me brother, aina hii ya watu ni sifuri kabisa kuhusu kujiongeza, hata kusema kuna wanafunzi wengi wanapita hio sehemu aweke auze hata kalamu, hilo wazo hana kabisa
Mkuu ni duka classique, nguo za 50 hadi laki 3🤣
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom