Shutuma za Diamond Platnumz dhidi ya Forbes, sasa naanza kuamini maneno ya Vijiweni kuwa Bakheresa ni tajiri zaidi ya MO

WINGER_TEREZA

JF-Expert Member
Jul 31, 2015
242
450
Habari, Jana msanii tajika sana nchini Tanzania, Afrika Mashariki na kati na pengine kuliko wote kusini mwa jangwa la Sahara Naseeb Abdul, maarufu kama Diamond Platnumz, alisaini dili kubwa na moja kati ya recording label kubwa ya muziki dunia, Warner Music Group, kuhusu usambazaji wa kazi za muziki wake na Wasanii walio katika label yake ya WCB WASAFI.

Muda mfupi baada ya Diamond kusaini mkataba huo alitumia page za mitandao ya kijamii ya Instagram na Twitter kutoa shutuma kwa kampuni kubwa ya Kimarekani inayojihusisha na tafiti za kubaini watu wenye ukwasi (UTAJIRI), FORBES, kuwa hawakufanya tathimini vizuri juu ya ukwasi aliona kupitia ile list waliyoitoa last week inayonesha Wasanii matajiri zaidi barani Afrika ambapo kwenye list hiyo Naseeb hayumo hata kwenye top 20!

Sio mara ya kwanza hawa FORBES kulalamikiwa na baadhi ya watu juu ya takwimu zao kwa mfano ni mwaka jana tu rapper Mkubwa toka "STATE", Kanye West, alilalamika na kuwapa makavu hao FORBES kwa kumkadilia kiduchu juu ya utajiri wake kitu achapo kilizua gumzo sana Dunia nzima na ikapelekea kwa hao FORBES kuingia chimbo kumkadilia tena Kanye na hatimaye wakamtangaza kuwa yuko katika orodha ya Ma-rapper billionares sambamba na Jay Z, P.Diddy na Dr Dree.

Kwa huku kwetu Tanzania, kila mwaka FORBES wamekuwa wakitoa orodha ya watu matajiri zaidi nchini na kwa mara zote wamekuwa wakimtaja Mtendaji Mkuu wa Makampuni ya Mohammed Enterprises (METL), Mohammed Dewji - Mo, kuwa ndiye billionaire kinara hapa kwetu na pengine ndiye billionare kijana kuliko wote Afrika. Hii imekuwa ikipingwa na baadhi ya watu hasa katika "vijiwe vya kahawa" kwani wengine wanaamini kuwa mmiliki wa Makampuni ya Said Salim Bakhresa (SSB Group of Companies) - Saidi Bakheresa kuwa ndiye mwenye pesa nyingi kuliko wote hapa Tanzania kwani ana mali zisizo amishika zinazo onekana na kujilikana na kila mtu tofauti na huyo MO.

Kwa scenerio hizo, nami kama naanza kuamini hayo maneno ya Vijiweni kuwa Bakhresa ndiyo tajiri namba moja hapa kwetu Tz kwani kila mtu anaziona mali zake kama Wiwanda vyake kila kona hapa nchini na kwa DSM Mfano ni pale Buguruni, Mwandege, Uwekezaji Mkubwa pale Chamazi - Azam complex, kuleze Zanzibar ana uwekezaji mkubwa sana sitaweza kutaja wote ila chukulia mfano wa Hotel Verde na ule Mji wa kitalii wa Fumba. Ana mradi mkubwa wa uzalishaji wa miwa pale Bagamoyo ambapo itapelekea kuanzishwa kwa kiwanda kikubwa cha sukari nchini. Pia bidhaa za Azam zimekuwa nambari moja katika nchi nyingi za Afrika na ni nadra sana kwa Mtanzania wa kawaida kupita siku bila kutumia bidhaa hata moja ya Azam hasa za Vyakula na Vinywaji!.

Mwisho napenda kuhitimisha kuwa pengine Diamond yuko sahihi kuwa Forbes memkadilia vibaya na pia Forbs wamemkadilia vibaya Bakhera (kwa Bakhersa nina asilimia kubwa hii ni kutokana na hulka yake ya kutopenda kuweka mambo yake hadharani na huwa hapendi kujionesha wala kuonekana onekana tofauti na MO au matajiri wengine tunao wajua).

Nawasilisha na asanteni.
 
Bakheresa ndio tajiri wa ukweli wala sina mashaka na hilo na naamini ni tajiri mkubwa nchi hii ndio maana hata JPM aliwavuruga wote mpaka huyo Mo na Manji lakini alijaribu kidogo kwa Bakheresa nadhani aliambiwa mzee huyu msimguse mambo yatayumba JPM mwenyewe akaenda akawapokonya wale jamaa Bagamoyo akampa Bahkresa ardhi kubwa kwa ajili ya sukari na JPM unamjuwa alikuwa hana msalie mtume Manji aliona cha moto na Mo alipata shughuli.
 
Bakheresa ndio tajiri wa ukweli wala sina mashaka na hilo na naamini ni tajiri mkubwa nchi hii ndio maana hata JPM aliwavuruga wote mpaka huyo Mo na Manji lakini alijaribu kidogo kwa Bakheresa nadhani aliambiwa mzee huyu msimguse mambo yatayumba JPM mwenyewe akaenda akawapokonya wale jamaa Bagamoyo akampa Bahkresa ardhi kubwa kwa ajili ya sukari na JPM unamjuwa alikuwa hana msalie mtume Manji aliona cha moto na Mo alipata shughuli.
Kweli Mkuu nami naungana na wewe kuwa SSB ndio tajiri wa ukweli na hakuna uongozi uliowahi mtikisa yule Mzee.
 
Nimegundua Diamond ana akili fupi sana au anatafuta kick tu. Hauwezi kuja na kuanza kuisema Forbes wakati wewe mwenyewe unajijua hauna utajiri wa kujilinganisha na Davido au Wazkid. Utajiri wa mtu huwa unapimwa na thamani ya Asset, Cash au Shares ambazo anazo kwenye kampuni. Sasa Diamond Asset ngapi hapa mjini au Shares ngapi? Ni ujinga tu.
 
Bakheresa ndio tajiri wa ukweli wala sina mashaka na hilo na naamini ni tajiri mkubwa nchi hii ndio maana hata JPM aliwavuruga wote mpaka huyo Mo na Manji lakini alijaribu kidogo kwa Bakheresa nadhani aliambiwa mzee huyu msimguse mambo yatayumba JPM mwenyewe akaenda akawapokonya wale jamaa Bagamoyo akampa Bahkresa ardhi kubwa kwa ajili ya sukari na JPM unamjuwa alikuwa hana msalie mtume Manji aliona cha moto na Mo alipata shughuli.
Hiyo ni dhana iliyopotoka.
 
Unajua nani anayeshikilia soko la kusafirisha korosho za Tanzania nje na nani ana kibali pekee cha kuingiza bidhaa za lg pamoja na pikipiki boxer, halafu next time ukikurupuka na kusema sijui bakhresa anamiliki shamba la miwa ukiwa unaelekea Tanga na kuona yale mashamba ya mkonge unayaangalia hadi unalala ukiamka hujamaliza ujiulize ni nani/...maana kwa uwezao wako wa kuchambua hoja hata nikikuambia ukafuatilie walipaji wakubwa wa kodi TRA kati ya MO na BAKHRESA bado ntakuchosha. Mo ni Tajiri bahili kuliko bakhresa ujue tu mwenzio ndo anaongoza kuajili watu wengi Afrika mashariki na kati baada ya serikali yako
 
MO yupo kwenye kundi la vijana matajiri Afrika na sio tajiri kwa ujumla ukilinganisha na Bakhresa.
 
unajua nani anayeshikilia soko la kusafirisha korosho za Tanzania nje na nani ana kibali pekee cha kuingiza bidhaa za lg pamoja na pikipiki boxer.....halafu next time ukikurupuka na kusema sijui bakhresa anamiliki shamba la miwa ukiwa unaelekea Tanga na kuona yale mashamba ya mkonge unayaangalia hadi unalala ukiamka hujamaliza ujiulize ni nani/...maana kwa uwezao wako wa kuchambua hoja hata nikikuambia ukafuatilie walipaji wakubwa wa kodi TRA kati ya MO na BAKHRESA bado ntakuchosha…… mo ni Tajiri bahili kuliko bakhresa ujue tu mwenzio ndo anaongoza kuajili watu wengi Afrika mashariki na kati baada ya serikali yako
Mkuu, huyo mleta thread ni kati ya wale vijana wanaoangalia vitu juu juu na kuleta mabishano yasomaana! Anadhani anavyoona magari ya Bakhresa yanavyopita road na ile mibango anaamini ndo utajiri! Anadhani kuimiliki Azam media, kuwa na kiwanja Chamanzi na kumiliki timu ndio utajiri. Hamjui MO vizuri huyu!
 
Back
Top Bottom