Shutuma za Diamond Platnumz dhidi ya Forbes, sasa naanza kuamini maneno ya Vijiweni kuwa Bakheresa ni tajiri zaidi ya MO

Habari, Jana msanii tajika sana nchini Tanzania, Afrika Mashariki na kati na pengine kuliko wote kusini mwa jangwa la Sahara Naseeb Abdul, maarufu kama Diamond Platnumz, alisaini dili kubwa na moja kati ya recording label kubwa ya muziki dunia, Warner Music Group, kuhusu usambazaji wa kazi za muziki wake na Wasanii walio katika label yake ya WCB WASAFI.

Muda mfupi baada ya Diamond kusaini mkataba huo alitumia page za mitandao ya kijamii ya Instagram na Twitter kutoa shutuma kwa kampuni kubwa ya Kimarekani inayojihusisha na tafiti za kubaini watu wenye ukwasi (UTAJIRI), FORBES, kuwa hawakufanya tathimini vizuri juu ya ukwasi aliona kupitia ile list waliyoitoa last week inayonesha Wasanii matajiri zaidi barani Afrika ambapo kwenye list hiyo Naseeb hayumo hata kwenye top 20!

Sio mara ya kwanza hawa FORBES kulalamikiwa na baadhi ya watu juu ya takwimu zao kwa mfano ni mwaka jana tu rapper Mkubwa toka "STATE", Kanye West, alilalamika na kuwapa makavu hao FORBES kwa kumkadilia kiduchu juu ya utajiri wake kitu achapo kilizua gumzo sana Dunia nzima na ikapelekea kwa hao FORBES kuingia chimbo kumkadilia tena Kanye na hatimaye wakamtangaza kuwa yuko katika orodha ya Ma-rapper billionares sambamba na Jay Z, P.Diddy na Dr Dree.

Kwa huku kwetu Tanzania, kila mwaka FORBES wamekuwa wakitoa orodha ya watu matajiri zaidi nchini na kwa mara zote wamekuwa wakimtaja Mtendaji Mkuu wa Makampuni ya Mohammed Enterprises (METL), Mohammed Dewji - Mo, kuwa ndiye billionaire kinara hapa kwetu na pengine ndiye billionare kijana kuliko wote Afrika. Hii imekuwa ikipingwa na baadhi ya watu hasa katika "vijiwe vya kahawa" kwani wengine wanaamini kuwa mmiliki wa Makampuni ya Said Salim Bakhresa (SSB Group of Companies) - Saidi Bakheresa kuwa ndiye mwenye pesa nyingi kuliko wote hapa Tanzania kwani ana mali zisizo amishika zinazo onekana na kujilikana na kila mtu tofauti na huyo MO.

Kwa scenerio hizo, nami kama naanza kuamini hayo maneno ya Vijiweni kuwa Bakhresa ndiyo tajiri namba moja hapa kwetu Tz kwani kila mtu anaziona mali zake kama Wiwanda vyake kila kona hapa nchini na kwa DSM Mfano ni pale Buguruni, Mwandege, Uwekezaji Mkubwa pale Chamazi - Azam complex, kuleze Zanzibar ana uwekezaji mkubwa sana sitaweza kutaja wote ila chukulia mfano wa Hotel Verde na ule Mji wa kitalii wa Fumba. Ana mradi mkubwa wa uzalishaji wa miwa pale Bagamoyo ambapo itapelekea kuanzishwa kwa kiwanda kikubwa cha sukari nchini. Pia bidhaa za Azam zimekuwa nambari moja katika nchi nyingi za Afrika na ni nadra sana kwa Mtanzania wa kawaida kupita siku bila kutumia bidhaa hata moja ya Azam hasa za Vyakula na Vinywaji!.

Mwisho napenda kuhitimisha kuwa pengine Diamond yuko sahihi kuwa Forbes memkadilia vibaya na pia Forbs wamemkadilia vibaya Bakhera (kwa Bakhersa nina asilimia kubwa hii ni kutokana na hulka yake ya kutopenda kuweka mambo yake hadharani na huwa hapendi kujionesha wala kuonekana onekana tofauti na MO au matajiri wengine tunao wajua).

Nawasilisha na asanteni.
Mkuu ni kusahihishe kidogo kweli bakhresa ni matajiri Mara dufu kuliko moo,,
Inawezekana ikawa ni moja Kati ya ya kampuni zenye ukwasi wa kutisha barani africa lakini tofauti ni kwamba bakhresa ni group of company .
Na Forbes wanakadiria utajiri wa MTU mmoja mmoja..
 
Jamani hayo ni makadilio tu mapovu ya nini sasa,mbona akina Harmonize & king kibamia wameuchuna hawana muda wa kujilinganisha na mafreemasons
 
Mkuu ni kusahihishe kidogo kweli bakhresa ni matajiri Mara dufu kuliko moo,,
Inawezekana ikawa ni moja Kati ya ya kampuni zenye ukwasi wa kutisha barani africa lakini tofauti ni kwamba bakhresa ni group of company .
Na Forbes wanakadiria utajiri wa MTU mmoja mmoja..
una akili kweli wewe...unajua ellon musk ana kampuni ngapi ndani yake au unajua google ni part ya Alphabet company...hivi leo kijiwe kizima ndo mmeazimana simu kuja kucomment humu nn
 
Dhana ya Diamond ni kuwa Forbes walipaswa kumfuata na kuwapatia full details toka kwake labda angewatajia hizo assets, Cash na liabilites na hapo sio lazima Diamond awe juu ya Davido

Alitakiwa kuwa kimya bcz hizi report zinatoka kila mara alichotakiwa ni kuwapa invatation waje hao forbes then anawapa full details za utajiri wake baada ya hapo nexr report wana toa report iliyo na utajiri wake current na sio kuandika huu upuuzi ambao hata wanamziki wezake wanamcheka….
 
Bakheresa ndio tajiri wa ukweli wala sina mashaka na hilo na naamini ni tajiri mkubwa nchi hii ndio maana hata JPM aliwavuruga wote mpaka huyo Mo na Manji lakini alijaribu kidogo kwa Bakheresa nadhani aliambiwa mzee huyu msimguse mambo yatayumba JPM mwenyewe akaenda akawapokonya wale jamaa Bagamoyo akampa Bahkresa ardhi kubwa kwa ajili ya sukari na JPM unamjuwa alikuwa hana msalie mtume Manji aliona cha moto na Mo alipata shughuli.
Sasa mbona Bakharesa halii kutotajwa kama Mondi? Hivi tajiri/mwenye fedha huwa anajisifu?
 
Nimegundua Diamond ana akili fupi sana au anatafuta kick tu. Hauwezi kuja na kuanza kuisema Forbes wakati wewe mwenyewe unajijua hauna utajiri wa kujilinganisha na Davido au Wazkid. Utajiri wa mtu huwa unapimwa na thamani ya Asset, Cash au Shares ambazo anazo kwenye kampuni. Sasa Diamond Asset ngapi hapa mjini au Shares ngapi? Ni ujinga tu.
Haka kajamaa, eti hana akir!
 
una akili kweli wewe...unajua ellon musk ana kampuni ngapi ndani yake au unajua google ni part ya Alphabet company...hivi leo kijiwe kizima ndo mmeazimana simu kuja kucomment humu nn
Mimi ntakuelewesha vizuri tu ambapo hujaelewa sitakutukana Wala nn mkuu,,
Hata metl ya moo ina makampuni mengi tu umo ndani lakini owner ni moo dewji,,
Bakhresa group of companies Kuna kampuni nyingi Sana humo ndani zinazomilikiwa na wanafamilia wa familia moja ya bakhresa,,mzee bakhresa mwenyewe siku nyingi tu alishakaa pembeni makampuni yanasimamiwa na wanae mkuu sijui ka unajua hilo ..
Kuna kampuni nyingne zipo chini ya yusuphu zingine Aboubakar na wanafamilia wengne nazani utakua umenielewa mkuu.
 
Hata lugha yake sio nzuri hauwezi ukasema stupid nadhani kosa ni Manager wake hakufanya kazi yake au Diamond hakumuhusisha manager wake katika hili
 
Nimegundua Diamond ana akili fupi sana au anatafuta kick tu. Hauwezi kuja na kuanza kuisema Forbes wakati wewe mwenyewe unajijua hauna utajiri wa kujilinganisha na Davido au Wazkid. Utajiri wa mtu huwa unapimwa na thamani ya Asset, Cash au Shares ambazo anazo kwenye kampuni. Sasa Diamond Asset ngapi hapa mjini au Shares ngapi? Ni ujinga tu.
Vichwa panzi uta wajua hao forbes ni nani hadi wasi semwe ni sawa na gazeti la nipashe tu .tofaut yao ni wako America na ni famouse ..sasa wasi semwe wana mchango gani kwa taifa
 
unajua maana ya managing director na executive director.....Unajitukana mwenyewe kwa uwezo wako wa kufikili...mkurugenzi mkuu na mmiliki wa makampuni ya azam bado ni baba hao wengine ni wakurugenzi watendaji...hivi mnadhani google ni ya kusearch xvideo tu kaka na sio mambo ya maendeleo_???????
Mimi ntakuelewesha vizuri tu ambapo hujaelewa sitakutukana Wala nn mkuu,,
Hata metl ya moo ina makampuni mengi tu umo ndani lakini owner ni moo dewji,,
Bakhresa group of companies Kuna kampuni nyingi Sana humo ndani zinazomilikiwa na wanafamilia wa familia moja ya bakhresa,,mzee bakhresa mwenyewe siku nyingi tu alishakaa pembeni makampuni yanasimamiwa na wanae mkuu sijui ka unajua hilo ..
Kuna kampuni nyingne zipo chini ya yusuphu zingine Aboubakar na wanafamilia wengne nazani utakua umenielewa mkuu.
 
unajua maana ya managing director na executive director.....Unajitukana mwenyewe kwa uwezo wako wa kufikili...mkurugenzi mkuu na mmiliki wa makampuni ya azam bado ni baba hao wengine ni wakurugenzi watendaji...hivi mnadhani google ni ya kusearch xvideo tu kaka na sio mambo ya maendeleo_???????
nikutarifu tu mkuu mkurugenz mkuu wa Azam group of companies sio mzee bakhresa Tena mkuu,,..ni Aboubakar Saeed Salim bakhresa mtoto mkubwa wa mzee ebu nakuomba na we ugoogle Kama ulivyoniambia Mimi kuangalia x ,mzee Alishachana na Ivo vitu,,..na ndani ya hayo makampuni zipo kampuni nyingi tu msimamizi na mwenye share nyingi ni yusuph bakhresa ,nyngne zinasmamiwa na wanadungu wengne wa mzee bakhresa ,,so hizo Mali zimetapanywa kwa watu mbali mbali kwenye familia chini ya mwamvuli mmoja wa Azam group of company elewa mkuu,,
Hatupo apa kushindan nan mshindi tunaeleweshana tu mkuu.
Nadhani umenielewa mkuu
 
unajua maana ya managing director na executive director.....Unajitukana mwenyewe kwa uwezo wako wa kufikili...mkurugenzi mkuu na mmiliki wa makampuni ya azam bado ni baba hao wengine ni wakurugenzi watendaji...hivi mnadhani google ni ya kusearch xvideo tu kaka na sio mambo ya maendeleo_???????
Taratibu mkuu
 
Hata kama hawajasema ukweli kwani wamempora hela zake,kwani amevunjiwa heshma?
Hebu atulie tupambane na Tanesco na mafundi wao waliokosa uwezo wa kuchokonoa sehemu ndogo mtandao ukakaa sawa
 
Taratibu mkuu
Hakuna anachoelewa huyo mkuu matusi tu ndo yamemjaa..
Bado Hadi Leo anadhani mkurugenzi mkuu wa Azam group of companies ni mzee bakhresa,,
wakati mzee Alishachana na Ivo vitu kitambo tu toka mwanae mkubwa Aboubakar alivyorudi kutoka masomoni marekani.
akapewa cheo Cha mkurugenzi mkuu wa makampuni yote ya bakhresa ,so as for now Aboubakar ndio boss mkubwa,Ila zile ni Mali za family kila mtu Ana Chaka zake kapewa anaendeleza.
 
Hiyo list ya fobes kuna wasanii hawajulikani vyanzo vyao vya mapato kweli mtu unaamini msanii wa Nigeria anaitwa M.I au akothee ni bilionea
 
Hata kama hawajasema ukweli kwani wamempora hela zake,kwani amevunjiwa heshma?
Hebu atulie tupambane na Tanesco na mafundi wao waliokosa uwezo wa kuchokonoa sehemu ndogo mtandao ukakaa sawa
Diamond anaweza kua ha jasoma Ila inawezekana ana washauri wazuri au kujichanganya kwake na watu waliondelea kwenye sector ya biashara kumemfungua mnoo mawili matatu anapata.
Mkuu wasanii naongelea big artist dunian uko ambako ndugu yetu huyu anaenda Sana kujichanganya wanategemea Sana endorsement kujiongezea kipato na kuendelea kua wakubwa na matajiri.
So mtu akikukadiria wewe utajiri wako ni $mil5 means hata deal zako utakazopata itabdi ziendane na ukwasi wako means hapo mtu kaja Sana labda $100000.
huwez kupata deal itayozidi kiwango cha utajiri wako.
ndo maana wasanii wenye akili wanakua wakali Sana ukiwakadiria padogo.
Ukiskia Jay z kapata deal ya $mil.5
Moja ya vigezo vikubwa wanavyoangalia wat kuekeza kwako ni thamani yako currently.

Kama Jay z ana utajiri wa $bilion huwez kwenda na $100000 ukawekeze kwake lazma ujipange.
Na hicho ndio kinafanya diamond awe mkali.
Yale matoleo ya Forbes Yana maana kubwa Sana mkuu zile ndo reference zenyewe waheshmiwa wanaztumia if they need to invest to someone or in some bussness.
 
Wale akina zari na wema pamoja na uzee wao walikuwa wanamfundisha lugha na uchumi lakini sasa mtupu hivi kawekeza wapi na nini maana utajiri unapimwa kwa rasilimali ulizowekeza
 
Back
Top Bottom