15H4C9M1
Japokuwa kuna mtu hapo kaongea kiushabiki kiukweli hizo shule sio za watu maskini hata kwa standards za dunia ya kwanza, shule kama IST hata the median (typical) household in America(has a net worth of less than $15,000, excluding home equity) hawawezi ku-afford. Hizo shule zinawalenga senior expatriate officials ambao pia hata wao hulipiwa na ofisi zao kwa asilimia kubwa na watoto wa wafanyabiashara wakubwa nchini .
Na wanafunzi wanaomaliza hizo shule wengi wao wanakwenda kusoma vyuo vya America au ulaya maana ukimaliza IB Diploma ktk hizo shule ni rahisi sana kujiunga na chuo chochote kile hapa ulimwenguni hasa hasa ukiwa umefanya vizuri. Pia, kuhusu kusoma hapa nchini hutokea mara moja moja sana maana elimu ya vyuo vya Afrika Mashariki ni hovyo sana atleast Afrika kusini kwa hapa Afrika na kwenyewe kuna vyuo viwili vya maana kidogo (UCT na Pretoria). Kuna Rafiki yangu alimaliza IB diploma IST alisoma chuo kikuu cha Dar es Salaam japokuwa alipata chou kikuu cha Chicago aliamua kubaki hapa hapa.
Kuhusu kazi baadhi yao pia tupo nao maofisini hapa hapa bongo wengine wakimaliza vyuo hurudi mfano kuna mmoja nipo nae ofisini ni mchumi mwenzangu alimaliza Princeton University mwaka 2010 ktk kampuni ya mafuta na gesi na wengi sana wapo ktk auditing firms kama business analysts wawili wapo Delloitte mmoja kamaliza Harvard University (Econ 16') na mwingine kamaliza Yale University. Wote hao wamesoma IST au ISM pia almost wote ambao niliokutana nao makazini wamesoma Ivy league schools au vyuo vikubwa ulimwenguni maana yangu hapa wanakuwa na nafasi kubwa ya kufanya kazi mahala ppte duniani kwa reputation ya chuo alichosoma ukilinganisha na chuo kikuu cha Dar es Salaam au Nairobi au Makelele.
Kama una mfuko mpana ni shule nzuri sana kumsomesha mwanao zinampa exposure na platform nzuri ya kuwa global citizen tofauti na mtu wa style yangu niliyepita ktk mazingira ya kimaskini kidato cha kwanza mpaka cha sita ada elfu 70 kwa mwaka.😀