Shule zenye ada ndefu zaidi Tanzania

BoManganese

JF-Expert Member
Jun 10, 2017
979
2,671
SHULE KUMI GHALI ZAIDI TANZANIA.

International School of Tanganyika (IST)

— Hii ndio shule ghali zaidi nchini. Iko jijini Dar Es Salaam na hufuata Mtaala wa IB. IST hutoza ada kuanzia shilingi za Kitanzania milioni 34 kwa chekechea hadi shilingi milioni 71 kwa sekondari, kwa mwaka.

2. Braeburn International School
—Hii ni shule ya kimataifa ambayo iko Dar Es Salaam na Arusha. Hufuata mfumo wa IB na ada yake kwa mwaka ni kuanzia shilingi za Kitanzania milioni 20 kwa shule ya msingi hadi shilingi milioni 43 kwa sekondari.

3. Dar Es Salaam International Academy (DIA)
—Hii ni shule ya tatu kwa kuwa na ada ghali zaidi nchini. Iko Dar Es Salaam na hufuata Mtaala wa IB. Ada yake kwa mwaka ni kuanzia Shilingi za Kitanzania milioni 23 kwa shule ya msingi hadi shilingi milioni 40 kwa sekondari.

4. Iringa International School (ISS)
— Iko mkoani Iringa na hufuata mitaala miwili ya IB na ule wa Cambridge. Hutoza ada kati ya Shilingi za Kitanzania milioni 17 kwa Chekechea hadi milioni 27 kwa sekondari.

5. Saint Constantine International School
—Inapatikana mkoani Arusha na hufuata Mtaala wa Cambridge. Ada yake ni kati ya Shilingi za Kitanzania milioni 8 kwa Chekechea hadi shilingi za Kitanzania milioni 23 kwa sekondari.

6. Kennedys House Schools
—Shule za Kennedys ziko maeneo mengi duniani. Nchini Tanzania iko katika mkoa wa Arusha wakiendesha Chekechea na Shule ya Msingi. Ada zao huanzia Shilingi za Kitanzania milioni milioni 8 kwa Chekechea hadi milioni 22 kwa Shule ya Msingi. Shule hii hufuata Mtaala wa Cambridge.

7. Haven of Peace Academy (HOPAC)
—HOPAC ipo katika Jiji la Dar Es Salaam. Hufuata Mtaala wa Cambridge na hutoza ada kati ya shilingi za Kitanzania milioni 16 hadi 22 kwa mwaka.

8. Aga Khan Primary & Secondary School
—Shule hii iko katika Jiji la Dar Es Salaam, na hufuata Mtaala wa IB kama ilivyo ISM. Hutoza ada kuanzia Shilingi za Kitanzania milioni 7 hadi milioni 20.

9. Internation School Moshi (ISM)/ UWC East Africa
— Hii ndio shule ghali zaidi katika mkoa wa Kilimanjaro. Hutoza ada kuanzia shilingi za Kitanzania milioni 16 kwa chekechea hadi shilingi za Kitanzania milioni 41 kwa wale wa kidato cha tano na sita. Shule hii hufuata Mtaala wa International Baccalaureate (IB).

10.Morogoro International School (MIS)
—Hii inapatikana mkoani Morogoro na hufuata mtaala wa Cambridge. MIS hutoza kuanzia Shilingi za Kitanzania milioni 6.4 kwa chekechea hadi shilingi za Kitanzania milioni 18 kwa sekondari. Hii ni ada peke yake, mbali na fedha ya usajili na boarding kwa wale wanaolala shuleni.

SOURCE: SWAHILI TIMES



Sent using Jamii Forums mobile app
 
na ujuwe kuwa huko wanabebwabebwa tu kwa kuwa wazazi wanazo huwezi kukuta ufaulu mkubwa kama wanao itafuta elimu kwa udi na uvumba
ACHA wivu we ndo maana tunabakia kuwa maskini sababu ya kusema vitu ambavyo hata ushahidi hauna ukiulizwa unachosema una ushahidi nacho utabaki kutoa macho acha unaa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
ACHA wivu we ndo maana tunabakia kuwa maskini sababu ya kusema vitu ambavyo hata ushahidi hauna ukiulizwa unachosema una ushahidi nacho utabaki kutoa macho acha unaa

Sent using Jamii Forums mobile app
yaani wewe hunielewi nachokisema huko huwezi kukuta michujo kama inayofanyiwa huku kwenye shule unazoziona zinafaulisha sana kwa taarifa yako mfano shule iliyokuwa ya kwanza mwaka huu mmiliki anashule mbili vilaza wote kawahamishia shule nyingine ya kwake hapo kabakisha krimu tupu kwanini wasiwe wa kwanza sasa kule mtu analipa milioni 50 halfu umhamishie kwa mabwege nani atakubali acha ujinga kunguru wewe
 
Back
Top Bottom