Shule zangu 3 bora za serikali mkoa wa Dar es Salaam

Foffana

JF-Expert Member
Oct 29, 2022
635
1,239
Habari zenu wadau wa jukwaa la Elimu
Siku ya leo nimeona niwaletee Shule 3 bora za serikali katika mkoa wa Dar es salaam.

Kama ndugu au mtoto wako ikitokea amepangiwa shule ya kata na unataka kumuhamisha nashauri uwapeleke shule hizi

Shule hizi zinaongoza kwa kufanya vizuri katika mitihani mbali mbali ya kitaifa na isiyo ya kitaifa

Shule hizi zimebarikiwa kuwa na walimu bora sana na wazoefu pia na mazingira mazurii ya kujisomeas
shule hizo ni

1.Dar es salaam secondary school
Hii inapatikana mtaa wa sikukuu na Gerezani inapakana na uwanja wa Jakaya M. Kikwete youth park kidongo chekundu

Ni moja kati ya shule ambazo ziko underrated kitaifa lakini in reality ni moja kati ya shule nzuri sanaaa

Ina masomo yote ya sanaa,biashara na sayansi

Shule ni ya kutwa na ni O level peke yake na haiimbwi sana midomoni mwa watu lakini hizo shule kongwe zote za Dar hakuna inayoipata hiyo shule

Kitaaluma wako vizuri pia unaweza fuatilia matokeo yao ya NECTA

Hongera kwa uongozi wa shule husika hongera kwa walimu pia

Screenshot_20240730_170313_Chrome.jpg
 
No 2 Azania secondary school

Al maarufu walijulikana kama Aza boy Hii nayo ni shule nzuri sana katika mkoa huu wa Dar es salaam Ni shule ambayo ina historia nzuri pia katika kutoa vipanga katika taifa letu
Pia imejaaliwa kuwa na walimu wengi na bora sana ufaulu wao ukichagizwa na commitment yao wanafunzi kwani tulikuwa tunakutana nao sanaa pale mchikichini kwa logman,mudy physics, mgote so hata uwe kilaza pale wenzako watakuinfluence ili ule msuli.
Kitaaluma wako vizuri sana japokuwa hatuioni hata top 20 lakini wanafunzi wao kiujumla wanafanya vizuri sana
images.jpeg
 
Wale wenzangu na mimi wa Round about, hatuna shida.
Shule yangu hapo ilishaweka rekodi ya kufunga kitasa kitaifa..
Anyway iliniwakilisha vzr,
Mimi mwenyewe nishawahi funga kitasa kitaifa..
Nika trend, Sema tuu sitaki makuu.
 
No 3 Jangwani Secondary school

Hii ni shule ya wasichana tupu ambayo inapakana na shule ya Azania.
Ni shule nzuri sana kwa wasichana kwa hapa Dar ukicompare na zingine zilokuwepo kama Kisutu na Zanaki(hii simshauri mtu asome).

Ni shule inayofanya vizuri kwa O level na A level ina walimu wazuri na wazoefu pia.Wanazingatia sana suala la taaluma pia wako very strict kwa wanafunzi wanaovunjsheria.

kuna kipindi walishuka kiperfomance kwa A level now wamekqa vizuri na wanauwasha sana ni moja kati ya shule ambazo kupata division one kwa O level ni ukatae mwenyewe tu
 
Hivi Dar es salaam school nayo ni shule Kongwe? Kweli nmezeeka.....

Azania kwa sasa hakuna kitu ni moja ya shule inaongoza kwa zero nyingi kuliko div 1....

Kwa hiyo hizo shule ulizotaja zinaizidi Pugu Sekondari kwa ubora sio? Au hujui kuwa Pugu ipo Dar es Salaam pia.
Ndiyo Pugu inazidiwa
 
No 3 Jangwani Secondary school

Hii ni shule ya wasichana tupu ambayo inapakana na shule ya Azania.
Ni shule nzuri sana kwa wasichana kwa hapa Dar ukicompare na zingine zilokuwepo kama Kisutu na Zanaki(hii simshauri mtu asome).

Ni shule inayofanya vizuri kwa O level na A level ina walimu wazuri na wazoefu pia.Wanazingatia sana suala la taaluma pia wako very strict kwa wanafunzi wanaovunjsheria.

kuna kipindi walishuka kiperfomance kwa A level now wamekqa vizuri na wanauwasha sana ni moja kati ya shule ambazo kupata division one kwa O level ni ukatae mwenyewe tu
Warukaa ukuta bado wapoo nakumbuka enzizile tunatoka tambaza kuwasarandia mlinzi anapewa hela unajua anafungua geti kumbe anaenda kumsukuma mdada ukutan unasikia huyooo unapkkeaa mzigo wakoo aisee adventure haziishi
 
No 2 Azania secondary school

Al maarufu walijulikana kama Aza boy Hii nayo ni shule nzuri sana katika mkoa huu wa Dar es salaam Ni shule ambayo ina historia nzuri pia katika kutoa vipanga katika taifa letu
Pia imejaaliwa kuwa na walimu wengi na bora sana ufaulu wao ukichagizwa na commitment yao wanafunzi kwani tulikuwa tunakutana nao sanaa pale mchikichini kwa logman,mudy physics, mgote so hata uwe kilaza pale wenzako watakuinfluence ili ule msuli.
Kitaaluma wako vizuri sana japokuwa hatuioni hata top 20 lakini wanafunzi wao kiujumla wanafanya vizuri sanaView attachment 3056962
Hivi axania wameanza collabo niliskia wanaleta na mabinti iwe mxt
 
Back
Top Bottom