A
Anonymous
Guest
Wadau, wakiwemo baadhi ya wazazi wa wanafunzi katika shule ya sekondari ya wasichana ya 'Competence Girls' Islamic Seminary ' iliyopo Wilaya ya Kigamboni, Mkoa wa Dar es Salaam wameendelea kutoa wito kwa mmliki wa shule hiyo kumuondoa mwalimu mkuu aliyeteuliwa hivi karibuni, kwa madai ya kwamba mwalimu huyo anadaiwa kuwa na historia ya ukiukwaji wa maadili katika shule nyingine ya sekondari iliyopo Wilaya ya Bagamoyo, Mkoa wa Pwani, (jina linahifadhiwa), ambapo inadaiwa aliondolewa kazini kufuatia tuhuma za mwenendo usiofaa unaomhusisha na mwanafunzi msichana.
Wadau hao wameendelea kudai kwamba mwalimu huyo tangu aanze kufanya kazi katika shule ya ya wasichana ya 'Competence' amelalamikiwa sana kuhusiana na mwenendo wake dhidi ya baadhi ya wanafunzi, ambapo baadhi ya wazazi wanadaiwa tayari kuhamisha watoto wao kutoka shule hiyo.
Wamesisitiza kuwa ni muhimu kwa uongozi wa shule kuchunguza kwa kina tuhuma hizo na kuchukua hatua stahiki kwa haraka ili kulinda usalama, ustawi na mazingira bora ya kujifunzia kwa wanafunzi, pamoja na kuzuia madhara yanayoweza kujitokeza endapo madai hayo yatabainika kuwa na ukweli.