Shule za vipaji maalumu

Habari,wadau wa Jf,
Nlikua nauliza je mtoto aliyepata 1 ya 9 ,na ana ufaulu wa
A-chemistry,B-physics na B- mathematics ,anaweza kuchaguliwa
Shule za vipaji maalumu(special schools) kidato Cha Tano?
Hata ingekuwa miaka 15 iliyopita asingechaguliwa.
 
Hiyo lebo ya "vipaji maalum" ndiyo sumu namba moja. Serikali iweke level ground kwa shule zote iache watoto wapambane wenyewe, siyo kutenga kuwa wengine wana vipaji maalum na wengine hawana vipaji. Ile system aliyokuwa ametengeza Nyerere ya kuwa na michepuo ya biashara, kilimo, ufundi, ualimu, na zetu sisi tuliokuwa kwenye michepuo ya kijeshi wakati huo ndiyo iliyokuwa system nzuri. Serikali ilitakiwa iongeze michepuo kama michezo, Muziki na vipaji kama hivyo na kuwaacha watoto wenyewe ndio waamue wanataka kwenda kwenye shule ipi.

Kuwepo kwa hizo shule za vipaji maalum leo ni kama zimeweka matabaka miongoni mwa watoto ambapo wale ambao hawakuingia vipaji maalumu wanajiona kama hawafai.
 
Lazima tugroom brains za kutusaidia baadae.

Wale vijana wa vipaj maalum wa zamani ndiyo wanaotusaidia siku hizi katika vyuo vyetu vikuu kama lecturers.

Kuwa na shule za vipaji maalum ni muhimu hasa kwa Mataifa machanga haya yanayohitaji brains za kutupigisha hatua kwa kasi.
 
Back
Top Bottom