Daisy Llilies
JF-Expert Member
- Apr 19, 2019
- 1,017
- 2,154
Waziri wa TAMISEMI Selemani Jafo amemuagiza Mkurugenzi wa halmashauri ya Kisarawe kuisajili shule mpya ya wasichana Kisarawe kwa jina la mkuu wa wilaya hiyo, Joketi Mwegelo.
Jokate amepokea taarifa hiyo kwa hisia na kusema hiyo ni heshima kubwa ambayo kuifikia amevumilia mengi ikiwemo baadhi ya watu kujaribu kumbeza na kumvua utu wake.
"Nilipoteuliwa wapo walibeza na wengine kujaribu kunivua utu wangu. Niliwaelewa lakini. Pwani wanasema Aso Mtu Ana Mungu. Namshukuru Mungu wangu kwa kunitetea. Mhe Waziri Jafo kamuelekeza DED kuisajili hii shule ya kihistoria Kisarawe na iitwe Jokate Mwegelo Girls Secondary School", Ameandika mkuu huyo wa wilaya aliyepata pia kuwa mshindi wa pili kwenye mashindano ya Miss Tanzania mwaka 2006.