Shule ya Sekondari ya Jokate yakabiliwa na uhaba wa maji

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Feb 7, 2022
2,302
5,441
Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Jokate Mwegelo iliyopo Kata ya Kibuta Wilaya ya Kisarawe mkoani Pwani inakabiliwa na kikwazo cha maji, hali inayosababisha wanafunzi kutumia muda mwingi wa kujisomea wenyewe kupata huduma hiyo.

Aidha, shule hiyo pia ina uhitaji wa uzio kutokana na mazingira iliyopo ili kuweka ulinzi kwa watoto wa kike wanaosoma katika shule hiyo.

Kutokana na hali hiyo uongozi wa shule pamoja na wanafunzi wameiomba Serikali kuangalia kati na kutafuta namna ya kutatua kero hizo ili kuwalinda wanafunzi na madhara yanayoweza kujitokeza.

Wakizungumzia vikwazo vya shule hiyo, mkuu wa shule pamoja na wanatunzi wameieleza kuwa,shule hiyo ina mazingira rafiki ya kujisomea, lakini kutokana na suala la uzio na vyanzo vichache vya maji Serikali inatakiwa kuingilia kati kuvitatua.

Mkuu wa shule hiyo, Mariam Mpunga alisema, Sekondari ya Wasichana Jokate Mwegelo licha ya kuwa na mazingira mazuri ya kujisomea kwa wanafunzi wa kike suala la kujenga uzio na kuongeza vyanzo vya maji ni vitu vya muhimu.

Kwa mujibu wa Ofisa elimu huyo Serikali inatambua vikwazo hivyo na iko kwenye mikakati ya kushughukiwa, na kwamba Mkurugenzi wa Halmashauri ameahidi kupeleka matenki kwa ajili ya kuvunia maji wakati utaratibu wa maji ya DAWASA ukiendelea.

Shule ya Sekondari Jokate Mwegelo ilianzishwa mwaka 2020 kufuatia ndoto ya viongozi ya kuhakikisha wanafunzi wa kike wanaondokana na kikwazo cha kukatisha malengo yao kielimu kutokana na umbali wa shule ambao umekuwa ukisababisha baadhi yao kupata ujauzito.


Chanzo: Majira
 
Kwani yeye Jokate Mwegelo anasemaje? Nasubiria tu kadi yake ya mwaliko ili nije kuchangia kwenye Harambee ya ujenzi wa huo uzio na pia uchimbaji wa kisima kirefu cha maji ili hayo matatizo yanayo wakabili watoto wetu yaishe kabisa.
 
Jokate kachangisha harambee mpaka shule imejengwa.

Niki wa pili anashindwa nini kuendeleza harambee za kuchimba visima vya maji ama kupambana na dawasco
 
Back
Top Bottom