KERO Shule ya Sekondari Buhanda: Wanafunzi wanarudishwa nyumbani kisa madawati hayatoshi

KERO Shule ya Sekondari Buhanda: Wanafunzi wanarudishwa nyumbani kisa madawati hayatoshi

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Mkoa wa Kigoma, Jimbo la Kigoma Mjini – Wanafunzi waliokuwa wameanza kidato cha kwanza hivi karibuni katika Shule ya Sekondari Buhanda baadhi yao wamerudishwa nyumbani baada ya kushindwa kupeleka madawati. Tatizo hilo limetokana na uhaba mkubwa wa madawati, jambo linalozidisha changamoto kwa wazazi na watoto wanaoanza masomo.

Baadhi ya walimu wameripotiwa kuwataka wazazi walipishe shilingi 40,000 ili mwanafunzi apate dawati, au kuwalazimisha kurudi nyumbani hadi watakapoleta madawati shuleni. Hali hii imesababisha hasira na wasiwasi miongoni mwa wazazi ambao wanasema ni kero kubwa kwa familia zao na elimu ya watoto wao.

Uhaba huu unaashiria changamoto kubwa ya miundombinu shuleni, ingawa hivi karibuni viongozi wa juu wa mkoa walitembelea shule hiyo. Madarasa yapo, lakini madawati hayatoshi, jambo linalozuia wanafunzi kuanza masomo kama ilivyopangwa. Taarifa hii inajitokeza wakati elimu nchini ikisisitizwa kuwa haki ya msingi ya kila mtoto.
 
Hiyo shule ni mpya? Kama sio, Zitto Kabwe alikuwa anafanya nini?
 
Mkoa wa Kigoma, Jimbo la Kigoma Mjini, Wanafunzi wanaoanza form one wanarudishwa nyumbani na kushindwa kupokelewa kuanza masomi kisa shule haina madawati.

Hili ni janga mfano Shule ya Secondary BUHANDA, Walimu wanawafukuza Wazazi mpaka watakapopeleka madawati ndio wanapokelewa, la sivyo wawalipe Walimu kiasi cha Shilingi 40,000 ili wapewe dawati.
Inasikitisha sana sana sana
 
Muwasiliane na afisa elimu mkishindwa mtafuteni baba levo
 
hiyo ni taharuki inazushwa na kuletwa na watu wasio wazalendo wanaharakati wanaotumwa na mabeberu.(hivi ndivyo wanasiasa watakavo jibu).
 
Sisiemu ni janga la taifa ,viongozi wana misafara ya magari zaidi ya 150 na helcopter juu mbili za ulinzi lakini jambo dogo la madawati linawashinda wakati tuna miti ya mbao kibao.
 
Back
Top Bottom