Shule ya Msingi Lomakaa Wilaya ya Siha Hatarini Kufungwa

Shule ya Msingi Lomakaa Wilaya ya Siha Hatarini Kufungwa

kisinja

JF-Expert Member
Joined
Sep 30, 2013
Posts
243
Reaction score
297
Dunia iko katika karne ya 21 ambapo maendeleo ya sayansi na Teknolojia kwa sasa yanapewa nafasi kubwa katika kuchagiza maendeleo ya Nchi mbalibali duniani. Tunatambua juhudi kubwa zinazofanywa na Serikali ya awamu ya sita Chini ya Mhe. Rais Dr. Samia Suluhu Hassan katika kuboresha huduma za KIjamii nchini. Hata hivyo Katika Shule ya Msingi Lomakaa Wilaya ya Siha Mkoani Kilimanjaro hali ni tofauti ambapo hali ya choo cha wanafunzi na waalimu ni mbaya sana kufikia hatua ambayo inaweza kupelekea shule hiyo kufungwa kama jinsi ambavyo taarifa zimekuwa zikisambaa kutokana na kuwa na choo chakavu cha zamani ambacho hata hivyo kimejaa.

Hivi karibuni kumeitishwa mkutano wa wananchi na kupelekea kuomba wananchi kuchanga fedha kiasi cha Shilingi milioni Nane kwa lengo la kujenga choo kipya. Wananchi wamejitoa kwa kiasi chake, hata hivyo kutokana na hali ya uchumi na kutokuwa na uwezo mkubwa wa wananchi, zoezi hilo halijafanikiwa kwani bado fedha hazijapatikana.

Swali la msingi nalojiuliza, je ni kweli Halmashauri ya Siha chini ya mkurugenzi Mnasi imeshindwa kabisa kujenga choo cha shilingi milioni 8? kiasi cha kupelekea wananchi kutembeza bakuli kuomba msaada? Wananchi wanapoona viongozi wao wanaishi vizuri na kutembelea magari ya kifahari barabarani huku wakishindwa kutenga bajeti ya milioni nane kujenga choo wawaeleweje? mbunge wetu Mollel yupo? DC YUPO? RC yupo? kweli milioni 8 kwa Serikali ni tatizo hata kufikia kuomba michango wananchi ambao ndio hao hao wamelipa kodi zao tayari?

Tunaomba sana viongozi wetu lliangalie hili na kuwasaidia watoto wa watanzania ambao kwa sasa wanapitia changamoto ya kukosa sehemu nzuri ya kujisitiri. Kero hii ni ya muda mrefu kwa zaidi ya miaka miwili sasa na haijatatuliwa. Tatizo hili lilianza tangu Mwaka 2017 Mkuu wa Wilaya akiwa ndugu Onesmo Buswelu hadi leo choo hakijakamilika. IMAGINE!

Chukueni Hatua sasa
 
Back
Top Bottom