Shule ya Msingi Lengatei Yatengewa Milioni 145 Ujenzi wa Madarasa 6 & Matundu 8 ya Vyoo

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,909
945

JIMBO LA KITETO: SHULE YA MSINGI KONGWE YA LENGATEI YATENGEWA MILIONI 145,772,640 UJENZI WA MADARASA 6 & MATUNDU 8 YA VYOO

Ndugu Wananchi Wenzangu wa Lengatei natambua uchakavu wa Madarasa na Miundombinu ya Shule yetu Kongwe ya Msingi Lengatei iliyoanzishwa 1970 ndani ya Jimbo la Kiteto kwani nimetembelea na kujionea mwenyewe ubovu wa majengo ya Madarasa na Miundombinu yote kwa Ujumla katika shule yetu Kongwe ya Lengatei.

Nachukua fursa hii adhimu kuwafahamisha kuwa Bajeti ya Mwaka 2023/2024 ya Wizara ya TAMISEMI tulipitisha tarehe 18/4/2023 Shule Yetu ya Lengatei ni kati ya Shule Kongwe iliyokuwa imepangiwa pesa kwaajili ya Ujenzi wa Madarasa Matatu mpya (3) yenye thamani ya Shilingi Milioni 60,000,000 na Matundu ya Vyoo 8 yenye thamani ya Shilingi 14,400,000

Napenda kuwafahamisha kuwa Shule yetu ya Lengatei, pamoja na kupata pesa kwenye bajeti ya 2023/2024 nimepeleka tena Maombi Maalum kwa Waziri wa TAMISEMI Mhe. Angellah Kairuki kuhusu kupata pesa zingine kwaajili ya Shule ya Msingi Lengatei. Tuvute Subra yajayo yanafurahisha zaidi"

Kwa dhati kabisa niwapongeze wananchi wa Lengatei kwa kuendelea kufuatilia kwa karibu suala la Shule ya Msingi Lengatei kwani mara kadhaa Nimepokea simu nyingi za wananchi mbalimbali wakinitaka niendelee kutafuta fedha kwaajili ya ukarabati wa Shule hii kongwe.

Mpaka sasa tumefikia hatua nzuri na napenda kutoa taarifa kwamba tulipeleka maombi maalum ya ziada ya madarasa 5 kwaajili ya Shule yetu Kongwe ya Lengatei na LAKINI habari njema ni kuwa Shule yetu ya Lengatei Kongwe imepangiwa madarasa matatu ( 3) ya ziada yenye thamani ya shilling Milioni 71,372,640

Kwahiyo, kwa ujumla kwa mwaka huu Shule yetu ya Lengatei itapata Madarasa 6 na Vyoo matundu 8 yenye thamani ya jumla ya 145,772,640

Nawaomba tuendelea kumuombea Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama yetu mpendwa Dkt. Samia Suluhu Hassan na wasaidizi wake wote Serikalini kwa moyo wa kuendelea kutafuta pesa kwaajili ya miradi ya kuboresha Miundombinu ya Shule zetu kwaajili ya Watoto wetu na kushughulikia changamoto za wananchi katika Wilaya yetu.

Ahadi za CCM zinaendelea kutekelezwa kwa ufanisi na kasi kubwa zaidi.

Kiteto yetu inaendelea Kung'ara !

Mungu Ibariki Kiteto !
Mungu Ibariki Tanzania !
Mungu ambariki Mhe. Rais wetu Mpendwa Mama yetu Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Imetolewa na Ofisi ya Mbunge
Mhe. Edward Ole Lekaita Kisau
Mbunge wa Jimbo la Kiteto

Tarehe 26. 8. 2023

Kazi Iendelee
 

Attachments

  • WhatsApp Image 2023-08-27 at 09.57.41.jpeg
    WhatsApp Image 2023-08-27 at 09.57.41.jpeg
    68.7 KB · Views: 3
Back
Top Bottom