Shule ya Bendel Memorial Moshi wanachapa sana watoto

Shule ya Bendel Memorial Moshi wanachapa sana watoto

Mi nakumbuka niligoma kuchapwa mbele ya staff nzima eti mwalimu mmoja anachapa viboko 30,nikawaambia kama mnanifukuza shule nifukuzeni kuchapwa sichapwi ,halaf nilikuwa hata sijafanya kosa la kuchapwa viboko vingi vile kisa sketi fupi na sketi yenyewe ndefu nilichofanya nikaenda kuikata iwe fupi

hahahhahahh, hapo tu mie hoi hahahahahha.
 
Mi naona hiyo Shule haina utaratibu mzuri ,kama hata mrinzi wa Shule amepewa mamulaka ya kuchapa viboko au kutoa adhabu kwa mwanafunzi hapo kuna tatzo kubwa sana,binafisi Mimi kama mzazi siwez kukubali mtoto wangu asome Shule ambazo hata mrinzi amepewa authorities ya kutoa adhabu kwa wanafunzi,kwa sababu mrinzi wa Shule sio mlezi ,hana mkadirio wa kutoa adhabu,
 
Ningetamani Walimu wote wangekuwa kama mimi coz mimi sina time na mtoto wa mtu hata nikitoa zoezi wakaandika kumi tu hao wananitosha.

Mimi sina muda wa kuhangaika kumpa adhabu ya aina yoyote ile mtoto wa mtu hata akiwa mtoro wa kila mara coz si serikali wala wazazi wa watoto wa siku hizi hawana shukrani kwa walimu hata kidogo

Mimi najali vipindi vyangu, maandalio, maazimio, nukuu na zana tu basi.

Kinachoniuma ni kitu kimoja tu kuwa tunazidi kutengeneza kizazi cha wafuasi wa Chama chetu cha kijani (wajinga).
 
Yep! Nadhani mtu kama Evelyn Salt karukia mjadala kwa upondo. Mimi nimeleta swali na kuonyesha kutofahamu kwangu hatua ya kiasi hiki. Suala la viboko limekuwa ni mjadala mkubwa wizarani na haiwezekani kuliacha, lakini pia nafahamu watoto wa mawaziri hawaguswi na viboko hivyo.

Ktk msg yangu ni kiwango. Viboko kutolewa na mlinzi wa shule!!! Nonsense! Hizi siyo enzi za kudhani kuna mtu anakusaidia kulea mtoto. Kuna walawiti kibao mtaani. I like your comment, hata kama hutaki mwanao alelewe kama yai, hustahili kumfanya ni ngoma ya burudani.
Ndugu yangu,katika shule za Kikatoliki kila mtumishi ni Mlezi.Na hili ndilo jambo linaloziweka shule hizi kuwa tofauti na zingne.Watoto wanafundishwa kuheshimu kila myu kuanzia mfagizi mpaka Mwalimu mkuu.Kila mtumishi anapewa jukumu la ulezi pasipo ubaguzi wa Kielimu!

Nimejisikia vibaya sana pale unapodai mlinzi kumchapa mwanao it's nonsense.Ndugu yangu,nikutaarifu tu huyu mlinzi au hata angekua mpishi anaweza kuwa mlezi mzuri wa nidhamu kuliko mtu mwenye doctorate.Nidhamu haipimwi by education level.Otherwise,wasiliana na Mwalimu mkuu kuhusu aina ya adhabu watowazo na sio kuchagua nani ana hadhi ya kumgusa mwanao.Ukionesha aina hii ya dharau katika shule za kikatoliki wanaweza mfukuza mwanao ili ukamuadhibu mwenyewe ambae unadhani una hio hadhi!

Nimeshauri by experience,nimesoma kwanzia nursery mpk F4 kwa hizi shule na nimeendelea kuwa katika System ya Kanisa hili kwa miaka Mingi.Kila la kheri katika kumsaidia kijana wetu kufikia mafanikio yake!
 
Kama mtoto wako anafaulu na hana madhara ya dhahiri unayoyaona zaidi ya mashitaka,wachunguze watoto hao kama ni watukutu.Mimi ni mzazi ila mtu anayemkanya mtoto wangu hata kwa kiboko kwa kumfunza,zawadi yake ni kinywaji anachopenda!

Je, wewe ukikosea unastahili adhabu ya viboko? Kama wewe hustahili adhabu hiyo unapokosea, kwa nini iwe sawa kwa mtoto?
 
We ndo umewaza mchunguzi ni housemaid mi nimemjibu kama mzazi
Sina watoto wa kunichosha mtoto wangu ndo kwanza hata mwaka hajafikisha na sidhani kama atakuja kunichosha make hakunaga tembo anaechoshwa na mkonga wake
back to topic, nlivomwambia huyu hata mzazi mwingine ntamwambia pia, shule nnayofundisha wanakujaga wazazi na malalamiko haya haya mara mtoto siju kapewa adhabu, mara kachapwa utakuta mtoto mwenyewe hata sie walimu anatuchosha ni basi tu tunakomaa nae kutimiza majukumu, yap tunalea watu hatulei mayai, mie kama mwalimu adhabu na viboko ni part ya kumfundisha na sio kumkomoa mtoto wa mtu, hivo kama unaona mwanao anaonewa, anachapwa sana beba peleka wasikochapwa ambako hakuna old way of teaching
Hatimaye wamekuzalisha duuh..! Asante huyo mume aliyekutia...na kukuwekea....mimba
 
Waitie polisi hao walimu, kuchapa mtoto ni mbaya sana sana maana atakuwa zuzu au jambazi!
 
Hawa walimu wanaochapa wanafunzi hovyo wanapaswa kutiwa adabu!!

Hizi adhabu za kikoloni za kuchapa binadamu viboko inabidi zikome kabisa.

Kwanini uchape binadamu viboko???

This is so insane.... sijui walitoa wapi hili wazo!
 
Mimi ni muumini kamili na kwa moyo wote na adhabu ya fimbo,nasema hivi kwa sababu ninazozijua mwenyewe.kipindi nasoma shule ya msingi nilikuwa mkorofi mpaka nikavunja rekodi ya kuwa mwanafunzi mkorofi kuliko wote tena ktk umri mdogo kipindi hiko darasa la tatu.

Ila siku ya siku walimu kwa kushirikiana na mama yangu mzazi walinionyesha jinsi ambavyo ukikosa nidham kwa kuelekezwa utakavyoipewa kwa shuruti.toka siku hiyo nikawa wa kwanza kufika shule,nikawa muhamasisha usafi na heshima kwa walimu.well ilinipa kuheshimika sana nakumbuka baada ya adhabu ile mpaka namaliza msingi mwalim mkuu hakuwahi kunichapa tena.

Waafrika lazima tuendane na mazingira yetu,siku hizi tunasikia wanafunzi wamejaza matusi kwenye paper za mitihani wakiwatukana walim zao hili la kudekezana inaweza kuwa ndiyo sababu.elimu ya 2000 kurudi nyuma huu ujinga haukuwepo.mimi watoto wangu shule watachapwa na nikijua sababu ya kuchapwa kwao nitawaongezea adhabu.
 
Mtoto apigwe ila sio kwa kupitiliza, pia kosa lingine sio la kupigwa ni kuambiwa....sasa hadi mlinzi anapiga watoto?? V

Viboko vinauma jaman mnaosem wapigwe tu mnamaana gani???? Mimi mwenyew niliacha MADRASA kwa ajili ya kipondo niliona alhamdu kuijua tu inanitosha
 
Back
Top Bottom