Shule ya Bendel Memorial Moshi wanachapa sana watoto

Shule ya Bendel Memorial Moshi wanachapa sana watoto

kuchapa mwanafunzi sio kumfundisha mm sijawaichapwa tangu darasa la tano mpaka namaliza form six nanipo vizuri tu academically na ki-discipline pia....niliachana na shule za kuchapa chapa tangu la tano,kama uyo dogo anamoyo wakujisomea bila kushinikizwa basi inafaa akahamishwa shule lakini kuna wale wanafunzi kushika kitabu necta hadi necta shule hizo zinawafaa tena sana tu.
 
ni kweli naamini watumishi wa hizo shule ni timamu sasa kama kijana anavunja kanuni na ni mbishi mjeuri, mkaidi ,hakuna jinsi wapigwe tu hata waziri mkuu amekwisha litolea ufafanuzi jambo hili

Yaani we kwa akili yako unawezaje kunukuu akili ya waziri mkuu kama pinda? Hiyo siyo aibu kwa mtu unayeweza kusoma na kuandika?

Sorry, niko Dodoma kupunguza wenye akili ndogo kwenye msafara wa kwenda ikulu maana naona wengine munakabidhi ubongo kwa kila neno la mwanasiasa.
 
We ndo umewaza mchunguzi ni housemaid mi nimemjibu kama mzazi
Sina watoto wa kunichosha mtoto wangu ndo kwanza hata mwaka hajafikisha na sidhani kama atakuja kunichosha make hakunaga tembo anaechoshwa na mkonga wake
back to topic, nlivomwambia huyu hata mzazi mwingine ntamwambia pia, shule nnayofundisha wanakujaga wazazi na malalamiko haya haya mara mtoto siju kapewa adhabu, mara kachapwa utakuta mtoto mwenyewe hata sie walimu anatuchosha ni basi tu tunakomaa nae kutimiza majukumu, yap tunalea watu hatulei mayai, mie kama mwalimu adhabu na viboko ni part ya kumfundisha na sio kumkomoa mtoto wa mtu, hivo kama unaona mwanao anaonewa, anachapwa sana beba peleka wasikochapwa ambako hakuna old way of teaching
Kazi ya viboko ni ku-reinforce tabia nzuri kwa mtoto na ku-discourage tabia isiyofaa.Ila viboko vinapozidi inakuwa ni tatizo kwa wanafunzi wenyewe.Kama madai ya mzazi ni kweli kwamba mpaka walinzi wanaruhusiwa kuchapa,basi hapo kuna tatizo.Punishment to students should be controlled/managed..sio kila mtu anapiga tu na kuchapa viboko visivyo hata na idadi mpaka vya mgongo!NO!
 
Kwani wamemshikilia hapo? Mtoe mpeleke huko unakodhani ni sahihi

Naona signature yako umechukuwa maneno ya Pinda, siku hiyo alikuwa na kichwa chake au cha kwako?
Mtoa mada kaamua kunyamaza, nimechukuwa jukumunla kuwaelimisha, lakini naona kumbe TZ hajufaulu kufuta ujinga. Unataka tuhamishe watoto lakini tukuachie wanaotaka kuchapwa!

Yaani kabisa munaona kuchapa ni sehemu ya bonuses za waalimu. Disastrous!
 
Naona signature yako umechukuwa maneno ya Pinda, siku hiyo alikuwa na kichwa chake au cha kwako?
Mtoa mada kaamua kunyamaza, nimechukuwa jukumunla kuwaelimisha, lakini naona kumbe TZ hajufaulu kufuta ujinga. Unataka tuhamishe watoto lakini tukuachie wanaotaka kuchapwa!

Yaani kabisa munaona kuchapa ni sehemu ya bonuses za waalimu. Disastrous!

Yes.. Na ukiona hutaki mwanao achapwe muhamishe, elimu yetu iko free sana you can decide where to send your children! Na kuna shule maelfu kwa maelfu..
 
Mpeleke st jude arusha mkuu.pale mwalimu akikutwa na fimbo anafukuzwa.wanafunzi hawatandiwi na kudekezwa mwanzo mwisho
 
yani katika kuongea kwako kooooote point ni hii hapa, na naona unakubaliana na mie viboko vitumike pale inapobidi, kuponda kote na kuiita ni old way of teaching ni ukoloni but mwenyewe umeona kuna mahali matumizi ya viboko inabidi
hope mjadala ulikuwa hapo na conclusion tayari

sa mtu ku support nayo imekua shida? Basi pole mr educator msomi wa kamachumu.....mjadala umeisha

Tatizo sio fimbo tatizo ni fimbo kupita kiasi hasa mkishakuwa na stress za kutibuliwa na waume zenu asubuhi asubuhi hasira zote mnatka mzimalize kwa watoto hii sio sawa!!!
 
Mungu baba nisamehe ila huwa simuelewi mzazi anayechukia mtoto wake kuchapwa kiboko, hususani pale mtoto anapochapwa kwa lengo la kuwekwa kwenye mstari myoofu wa maisha yake ya kesho. Pole mzazi ila kama unahisi mtoto wako anaonewa basi fuata utaratibu ili uweze kumnusuru na kichapo hicho huenda anaonewa.
 
MWANANGU KARUDI LIKIZO ANASEMA SIR ALIWACHAPA WOTE NIKAMUULIZA KUMZUNGUKA KWA NN MCHAPWE AKASEMA WALIKUA WANAPIGA MAKELELE NA WALIPOULIZWA NAN ANAPIGA HAKUNA ALIEJIBU.NIKAMWAMBIA MWALIMU ALIKUA SAHIHI HATAKI MFICHE MAOVU na siku ingine nitamwaMBIA AKUONGEZEE.
MTOTO MWINGINE NAMSOMESHA(SIO WANGU JAPO NAISHI NAE )NA ALICHAPWA HAKUKUSANYA DAFTARI,siku ingine nikamwambia kajisomee akabaki anaqangalia tv nikamwambia ukichelewa shule hatuta elewana kweli asubuhi akachelewa shuleni AKAPEWA adhabu nyingine ,SIKU INGINE ALIPANGIWA BUSTANI YA SHULE AKAENDA then akapotea
MWISHO WA WIKI NIKAKAGUA DAFTARI SIKULIDHIKA JNNE ya wiki ya tatu NIKAAMUA KUPITIA SHULENI,NILIPOAMBIWA MATATIZO YAKE NIKAMWOMBA MWALIMU AMCHAPE MWALIMU ALIMCHAPA BAKORA TATU,SIKULIDHIKA NIKAMSHIKA MWENYEWE NIKAMPA BAKORA SABA,MBELE YA STAFU NIKAWAOMBA WALIMU NIKAWAPA NAMBA AKIWA MKAIDI NIAMBIWE TANGU NIFANYE TUKIO HILO AMETOKA KUWA WA 40 KATI YA WANAFUNZI 94 NA AMEKUWA WA 9 NDANI YA MWAKA MMOJA .
 
Kama unamjibu housemaid vile!
Ungehangaisha brain kidogo tu ungeona sababu ya mzazi huyu kuuliza. Tatizo nadhani umechoshwa na wanao na sasa unadhani kila mtoto ni yai na anastahili kubadilishwa.Una watoto au ngoma? Caning at our schools is a legacy of colonial rule and so, some of your type, appreciate it, bluffed by this old-type-way of teaching.
Sasa povu la nini mkuu? Simply ukiona mtoto wako anachapwa mhamishie shule nyingine that's all. As I were canned enough during primary&secondary I know how canning is Important in schools.
 
Sasa povu la nini mkuu? Simply ukiona mtoto wako anachapwa mhamishie shule nyingine that's all. As I were canned enough during primary&secondary I know how canning is Important in schools.
OooooH Once upon a time! Swali la mwaka 2015 leo hii ndo unarudi JF. Ulipokuwa haupo, ni mengi yalikupita. Jitahidi kujifunza yooote hapo katikati kabla hujarukia uzi huu. Kama ulichapwa sana miaka yako, hilo lilishapita. Miaka hii ni ile ya kusoma ukiwa na iphone 7 na headphones. kama mwalimu haelewi mtindo huo ni mzigio kwetu.

Mwalimu elewa kwamba mwaka jama Finland imeondoa mitihani mashuleni. Ulipofundishwa kutumia fimbo ni maiak ile ukiwa hulipwi pesa za likizo. Miaka hii yupo Rais makini. Fundisha kwa furaha!
 
Katika utaratibu wa kawaida, njia kuu mbili hutumika katika kubadilisha ama kuimarisha tabia ya mwanadamu (wakati mwingine hata kwa viumbe wengine). Njia hizo ni "punishment na reinorcement" . Ili kuweka nidhamu na kusaidia vijana kutumiza malengo yao, "punishment and reinforcement" hutumika pia shuleni. Tukumbuke kuwa reinforcement hutumika ili kuchochea ama kuimarisha tabia nzuri. Kwahiyo huwezi kutumia reinforcement (hata kama ni negative reinforcement) kama adhabu.

Adhabu ya viboko shuleni ni moja kati ya njia ya kurekebisha tabia kwa wanafunzi. Kwa utaratibu wa kawaida adhabu yoyote inayotekelezwa inapaswa izingatie yafuatayo.
1) Anayeadhibiwa (mwanafunzi) anapaswa ajue ni sababu gani zinasababisha aadhibiwe

2) Adhabu inapaswa kutekelezwa mara tu baada ya kosa kufanyika.( yani immediately)

3) Uzito wa adhabu unapaswa kuendana na uzit wa kosa

4) Mtekelezaji wa adhabu anapaswa kuwa na lengo jema na mwenye uelewa mzuri juu ya utekelezaji wa adhabu.

Turudi kwenye mada:

Mleta mada hakuna mahali aliweza kuthibitisha kuwa taarifa zake zilitoka kwenye vyanzo sahihi ambavyo no "bias-free" na kuwa ni za kweli. Kwa maelezo yake ni kuwa mtoto wake kalalamika, je malalamiko hayo ni ya kweli? Je ni kweli kuwa mlinzi naye anachapa wanafunzi? Je wanafunzi wanachapwa bila kosa? Je katika kosa gani wanachapwa viboko vingapi? Je walimu wa bendeli hawajui taratibu za kuadhibu?

Ninachokiona hapa ni wazazi kuwa na fikra kuwa watoto wao huonewa na walimu pindi tu wanapoadibiwa. Shule bila viboko ni vigumu mno ila inawezekana lakini kwa gharama kubwa sana. Ukweli ni kuwa ni nadra sana mwalimu kumuonea mwanafunzi kwani hakuna anufaikacho nacho zaidi ya kuumia yeye.

Wazazi wa miaka hii jitahidini kuwa mnawajibika kwa watoto wenu. Hizi tabia za kuwasikiliza kwa kila wanachosema ndio huzaa vijana hovyo na mwisho wa siku mnaanza kulalamika. Shule husaidia sana kuwaweka vijana katika mstari unaofaa. Msiwavunje moyo walimu kwani mwisho wa siku wakiacha kuadhibu maana yake ni kuwa watawarudishia mabomu yenu wenyewe baada tu ya miaka michache.
 
Mi nakumbuka niligoma kuchapwa mbele ya staff nzima eti mwalimu mmoja anachapa viboko 30,nikawaambia kama mnanifukuza shule nifukuzeni kuchapwa sichapwi ,halaf nilikuwa hata sijafanya kosa la kuchapwa viboko vingi vile kisa sketi fupi na sketi yenyewe ndefu nilichofanya nikaenda kuikata iwe fupi
 
Naomba ushauri toka kwenu wataalamu wa taaluma na ufundishaji kutokana na tabia niliyoisikia ktk shule hii. Nina mtoto ninayemsomesha ktk shule hii ya Bendel memorial iliyoko moshi eneo la soweto, ambayo inaendeshwa na shirika la kikatoliki. Kwa ujumla matokeo yao ya mitihani huwa ni mazuri.

Tatizo kubwa ni uhusiano kati ya waalimu na wanafunzi wa shule hii. Ni miaka miwili sasa, mtoto anaporudi hadithi anayoisimulia ni wingi wa viboko unaotokana na maamuzi ya mwalimu yeyote ktk maeneo ya shule. Mshauri wa wanafunzi, yaani Patron hana ushauri anaotoa zaidi ya viboko.

Nilidhani ni utundu wa kijana wangu lakini hata jirani kalazimika kumuhamisha kijana wake kwa sababu hiyo hiyo. Wanafunzi wanapokuwa ktk maandalizi ya usiku, hiyo inayoitwa prep, kila wakati wanakuwa na wasi wasi maana patron akiingia huamua kupiga wanafunzi eti tu wanasoma wameinua vichwa, sic! Hata mlinzi wa shule anapiga wanafunzi viboko, eti tu ni usiku na anawasikia wakiongea.

Imani yangu hawa ni waalimu waliosomea, pamoja na yeyote aliyeko hapa ukumbini, hebu nipeni ushauri juu ya haya machache maana yapo mengi ambayo nadhani yanaharibu maana ya shule na huenda yatawaathili wanafunzi. Je, mtindo huu ni wa kawaida ktk ufundishaji?

Maana labda mimi kama mlezi namkinga sana kijana huyu!
Kwani hakuna vikao vya wazazi ili muwaambie ukwelikulingana na taaluma yangu si vyema kumchapa mtoto bila sababu na kiboko sio njia suluhishi ya tatzo,hivyo uongee na uongozi wa shule ujue kwanin wanafanya hivyo
 
Back
Top Bottom