Shule ya Bendel Memorial Moshi wanachapa sana watoto

MchunguZI

Platinum Member
Joined
Jun 14, 2008
Posts
4,047
Reaction score
2,239
Naomba ushauri toka kwenu wataalamu wa taaluma na ufundishaji kutokana na tabia niliyoisikia ktk shule hii. Nina mtoto ninayemsomesha ktk shule hii ya Bendel memorial iliyoko moshi eneo la soweto, ambayo inaendeshwa na shirika la kikatoliki. Kwa ujumla matokeo yao ya mitihani huwa ni mazuri.

Tatizo kubwa ni uhusiano kati ya waalimu na wanafunzi wa shule hii. Ni miaka miwili sasa, mtoto anaporudi hadithi anayoisimulia ni wingi wa viboko unaotokana na maamuzi ya mwalimu yeyote ktk maeneo ya shule. Mshauri wa wanafunzi, yaani Patron hana ushauri anaotoa zaidi ya viboko.

Nilidhani ni utundu wa kijana wangu lakini hata jirani kalazimika kumuhamisha kijana wake kwa sababu hiyo hiyo. Wanafunzi wanapokuwa ktk maandalizi ya usiku, hiyo inayoitwa prep, kila wakati wanakuwa na wasi wasi maana patron akiingia huamua kupiga wanafunzi eti tu wanasoma wameinua vichwa, sic! Hata mlinzi wa shule anapiga wanafunzi viboko, eti tu ni usiku na anawasikia wakiongea.

Imani yangu hawa ni waalimu waliosomea, pamoja na yeyote aliyeko hapa ukumbini, hebu nipeni ushauri juu ya haya machache maana yapo mengi ambayo nadhani yanaharibu maana ya shule na huenda yatawaathili wanafunzi. Je, mtindo huu ni wa kawaida ktk ufundishaji?

Maana labda mimi kama mlezi namkinga sana kijana huyu!
 
Nadhani shule za Kikatoliki ndivyo zilivyo, jamaa wangu hufundisha pale Kristu Mfalme Tabata, wanapiga balaa. Usiogope, wale ni wataalamu na wanajua wanachofanya.

Usiogope, inawezekana mwanao unamdekeza sana, hajazoea kuchapwa au unaumia sana kuona anachapwa. Hakuna tatizo kwenye viboko vya adhabu, hayo ya saikolojia sijui blah blah ni ya wazungu.

Kumbuka watoto pia wana tabia ya kukuza mambo wanapokuwa wanashitaki, usiwatilie sana maanani, lakini usipuuze concern zao. Mfano kama anasema amepigwa sana muambie akuoneshe mahali alikochapwa, kama hakuna madhara yoyote ya kimwili basi hakuna la kuhofu.

Tatizo langu na shule za Kikatoliki ni ule mchezo ambao huwa wanawafanya watoto wa kiume huku tukiwavumilia kwa kuwa ni wawakilishi wa Mwana wa Mungu.

Karibu!
 
Pamoja na mazuri unayoeleza, tusiwachoke watoto wetu na kudhani mashuleni watatusaidia kuwabadilisha. Na kama unavyosema, isije ikawa ni njia ya kuwalainisha ili wawaingize kwenye mambo ya ki anglikana.

Ni ajabu kuruhusu mlinzi kutoa adhabu ktk shule. Hiyo inaonyesha hakuna mpangilio wa utawala. Hata kama mwanafunzi kamtukana mlinzi, hatua muhimu ni kufuata mpangilio wa utawala hadi muhusika atoe hukumu na adhabu. Kwani mlinzi anajua ethics za ualimu? No! No!

Munaowasiliana na mkuu wa shule hiyo tunaomba apate taarifa hii.
 
Kama mtoto wako anafaulu na hana madhara ya dhahiri unayoyaona zaidi ya mashitaka,wachunguze watoto hao kama ni watukutu.Mimi ni mzazi ila mtu anayemkanya mtoto wangu hata kwa kiboko kwa kumfunza,zawadi yake ni kinywaji anachopenda!
 
Kama hutaki mwanao achapwe muhamishe mpeleke wanakolea watoto kama mayai....

Kama unamjibu housemaid vile!
Ungehangaisha brain kidogo tu ungeona sababu ya mzazi huyu kuuliza. Tatizo nadhani umechoshwa na wanao na sasa unadhani kila mtoto ni yai na anastahili kubadilishwa.Una watoto au ngoma? Caning at our schools is a legacy of colonial rule and so, some of your type, appreciate it, bluffed by this old-type-way of teaching.
 
Yep! Nadhani mtu kama Evelyn Salt karukia mjadala kwa upondo. Mimi nimeleta swali na kuonyesha kutofahamu kwangu hatua ya kiasi hiki. Suala la viboko limekuwa ni mjadala mkubwa wizarani na haiwezekani kuliacha, lakini pia nafahamu watoto wa mawaziri hawaguswi na viboko hivyo.

Ktk msg yangu ni kiwango. Viboko kutolewa na mlinzi wa shule!!! Nonsense! Hizi siyo enzi za kudhani kuna mtu anakusaidia kulea mtoto. Kuna walawiti kibao mtaani. I like your comment, hata kama hutaki mwanao alelewe kama yai, hustahili kumfanya ni ngoma ya burudani.
 
We ndo umewaza mchunguzi ni housemaid mi nimemjibu kama mzazi
Sina watoto wa kunichosha mtoto wangu ndo kwanza hata mwaka hajafikisha na sidhani kama atakuja kunichosha make hakunaga tembo anaechoshwa na mkonga wake
back to topic, nlivomwambia huyu hata mzazi mwingine ntamwambia pia, shule nnayofundisha wanakujaga wazazi na malalamiko haya haya mara mtoto siju kapewa adhabu, mara kachapwa utakuta mtoto mwenyewe hata sie walimu anatuchosha ni basi tu tunakomaa nae kutimiza majukumu, yap tunalea watu hatulei mayai, mie kama mwalimu adhabu na viboko ni part ya kumfundisha na sio kumkomoa mtoto wa mtu, hivo kama unaona mwanao anaonewa, anachapwa sana beba peleka wasikochapwa ambako hakuna old way of teaching
 
Mmmh hadi hapa nilipo sijawahi sikua mlinzi akichapa mwanafunzi hiyo shule ni ya kipekee, wewe kama mzazi umefanyaje umeenda shule ukapata uhakika au ndo mwanao kakusimulia tu, basi pole ndo nshakushauri kama wachukizwa na viboko mpeleke shule wasiochapwa hilo la kuchapwa na mlinzi I guess ni chai tu
 
We ndo umewaza mchunguzi ni housemaid mi nimemjibu kama mzazi
Sina watoto wa kunichosha mtoto wangu ndo kwanza hata mwaka hajafikisha na sidhani kama atakuja kunichosha make hakunaga tembo anaechoshwa na mkonga wake
back to topic, nlivomwambia huyu hata mzazi mwingine ntamwambia pia, shule nnayofundisha wanakujaga wazazi na malalamiko haya haya mara mtoto siju kapewa adhabu, mara kachapwa utakuta mtoto mwenyewe hata sie walimu anatuchosha ni basi tu tunakomaa nae kutimiza majukumu, yap tunalea watu hatulei mayai, mie kama mwalimu adhabu na viboko ni part ya kumfundisha na sio kumkomoa mtoto wa mtu, hivo kama unaona mwanao anaonewa, anachapwa sana beba peleka wasikochapwa ambako hakuna old way of teaching

Very weak way of making argument. Yaani kwa kuwa shuleni kwako yapo ya aina hiyo, ulipoona la huyu MchunguZI ukajua ni yaleyale ya kwako na majibu ukatoa yale yale ya huko kwako! Ktk taaluma yako ya ualimu kuna sehemu ulifundishwa kwamba viboko ni sehemu ya kufundisha?

Which useless college was that? I hope you are not a certified dog trainer?
 
Sasa ulitaka majibu yapi while kitu tunachoongea ni habari ya viboko?katika taaluma yangu sio kila nnachokifanya ndo nlifundishwa chuo, hata kukagua wanafunzi usafi sikufundishwa ila ni moja ya majukumu yangu
haya wewe mwenye strong argument zimwage hapa,
 
Huwezi kuendesha taaluma kwa ubunifu wako binafsi wakati unadai umesomea. Even acrobatic gymnastics have do and don'ts. How can you make routine caning part of your training and shamelessly, appreciate using it? We have proven facts that only circus animals and the likes go by carrot-and-stick.

Eti ubunifu! Ubunifu gani huo? Hii ni mchezo wa kangamoko? Unadhalilisha taaluma wee!
 
Kuna neno ubunifu hapo nmeandika? Jojoa ulale kesho ukiwa wewe sio kwa hisani ya ngano mention me nije tuchangie mjadala
 
Aaah! nimekosea nini?
Believe me, you are below the required teachers' level of thinking. Mexico is banning the use of animals in circus entertainment simply because of the torture accompanying their training, how is it that you still want to apply the same stupid technique to human being?

Wewe kama mwalimu ulistahili kabisa uonyeshe kiwango cha juu cha kufikiri badala ya kumtafutia fear factors mwanafunzi. btw, do you know the connection between body pain and brain functioning? Hilo ni somo langu kesho utakapoamka.
 
Nimesoma pale aisehh fimbo unaamka nazo asubuhi wakati wa kwenda church ukichelewa yaani dahhh lakini nashukuru nlifaulu kwenda chuo ........huyo patron nemes ni shida ananyuka fimbo balaaaa sio kama anaonea sema anafanya haki maana fimbo utachapwa kama umedodge kanisani asubuhi, umechelewa kuingia assembly, umedodge kuingia darasani, hufuati sheria za shule vizuri, ukifeli mitihani, na mambo kibao hapo ni kwa ufupi mengi zaidi ni pm
 
Aaah! nimekosea nini?
Believe me, you are below the required teachers' level of thinking. Mexico is banning the use of animals in circus entertainment simply because of the torture accompanying their training, how is it that you still want to apply the same stupid technique to human being?

Wewe kama mwalimu ulistahili kabisa uonyeshe kiwango cha juu cha kufikiri badala ya kumtafutia fear factors mwanafunzi. btw, do you know the connection between body pain and brain functioning? Hilo ni somo langu kesho utakapoamuka.
oooh kumbe case study ni Mexico? Hebu fanya iwe Tanzania ili twende sawa.
i see thinking capacity yako ndo unafaa kabisa kuwa mwalimu ila ndo hivo mi nshakua na hamna namna
 
Wewe kama mlezi au mzazi ulishafika shule kupeleka malalamiko yako ?

au kuulizia, halafu kuhusu mlinzi pale na yeye anachukua nafasi kama mlezi ,kwa hiyo ana haki ya kumwajibisha mtoto pale anapoona kafanya kosa,

mwisho kabisa usipende kusikiliza maneno ya mwanafunzi tu kisha ukaweka hitimisho fika shule update maelezo unaweza kuta mtoto ana majanga zaidi ya umjuavyo.
 
Back
Top Bottom