Viboko vikisha tumika inakuwa ni adhabu. Lengo la adhabu ni deterrent. Kama mtoto akiwa ni mwizi kiboko kinaweza kuwa ni deterrent ili asiibe, kama mtoto wako anatukana watu kwa ukorofi wake, kiboko ni deterrent aachane na ukorofi.
Sasa tofautisha hayo na mwalimu anayefundisha Vita ya maji maji, wanafunzi hawaelewi au anafundisha Archimedes's Principle halafu anaamua kutumia kiboko. Lengo ni nini? Hiyo ni adhabu, deterrent, ili iweje? Angeweza kusema labda wanafunzi hawakuingia darasani na sasa anatumia kiboko kama deterrent ili waingie Darasani na wafundishwe, lakini hakuna! yeye anaamua tu kupiga kama ile amri ya Pinda bila kujali au kujiuliza udhaifu wake wa kuwaelimisha wengine au hata tofauti ya binadamu kuelewa mambo. Tunatofautiana kuelewa mambo tofauti. Hiyo ni anthropology tutaelezana siku nyingine ukipenda.
Shule nyingi sana za aina ya kwako, ambazo wanapigwa kama ngoma, wanafunzi hawajiamini maana wanazoea kuepuka mtu anayewazidi, ambaye angewafundisha lakini sasa ni adui yao. Hata baba au mama wa aina hiyo anawafanya watoto wasiulize na kila akiingia wanatokomea vyumbani. Eti mama au baba ni mkali. Rubbish!
Kwa ujumla sisi ni binadamu, wenye utashi, wenye maaamuzi baada ya kufikiri. Matokeo ya viboko vya kipuuzi kama hivi ni tofauti kwa kila mtu na hakuna universality.
Hebu angalia video ifuatayo halafu niambie kama kweli kuna darasa ambalo wanafunzi wanaweza kuwa wapuuzi wote kiasi cha kupewa fimbo wote. Ni matokeo ya kuwaruhusu waalimu kama wewe kuchapa vijana, munakuwa addicted, munapenda fimbo kama pochi au handkerchief na kujikuta sasa kila sehemu ni kuulizia umpige nani kama huyu mzazi alivyouliza. You can't make caning part of training human being, it is a deterrent!
https://www.youtube.com/watch?v=KJq8PqvMFaM