Shule hii Mbeya iko wapi?

Hapo sasa naanza kuelewa hivyo CCM iliichukua shule ya serikali! Haikubaliki.
 
Mkuu kama umesoma Sangu Sec School bila shaka utakuwa unayajua haya maeneo Msichoke Pub.. upande wa pili ukivuka barabara ya lami...kulikuwa na mishkaki na pombe za kienyeji hapo.....Savoi Bar...na Vamponji...moja kati ya maeneo ambayo tumegonga sana ulabu enzi hizo...
 

Madom mengine ni Amri Abeid, Sokoine, State ya Juu na State ya Chini.... States zilikuwa bweni za wajanja ukiachilia mbali Mkapa ilipoungua.
 
Madom mengine ni Amri Abeid, Sokoine, State ya Juu na State ya Chini.... States zilikuwa bweni za wajanja ukiachilia mbali Mkapa ilipoungua.
Kati ya bweni zote Luthuli A ndio baba lao
 
Luthuli A hiyo.... Kushoto unaweza liona bweni la mkapa au disp zamani
 
Asante kwa picha hizi, naiona main hall, haikujengwa kiswahili lilikuwa na jukwaa kubwa lenye pazia kubwa, nakumbuka kikundi kimoja cha utamaduni toka Guinea kiitwacho Djoriba kilikuja kutumbwiza hapa, ni kikundi cha serikali kama tulichokuwa nacho Tanzania, pia naona mabweni mimi nilikuwa la kushoto kuelekea madarasani nilikuwa kwenye chumba cha attachment watu watatu, kuelekea kulia dining hall na bakery.
 
Mkapa ni bweni lipo nyuma ya Luthuli. Kama unaweza kuvuta picha, kuna jengo lilikuwa kule Karibu na Luthuli.

Pia kuna jengo jipya lilijengwa mbele ya Luthuli, linatizamana na mlango wa Luthuli...Lile niliondoka lilikuwa bado halijaanza kutumika.
Lile jengo lilitumika miaka 2 kama sikosei.
Lilishaanza kuharibika.
Labda baada ya huu ukarabati mpya ndo limeanza kutumika.
 
Tumerudi nyuma babu.
Tena hatau kumi nyuma ..daaah
 
Hahahaa...Daaah! Naomba nijibu kwanza tumerudi nyuma
.

Sie ratiba ya msosi ilikuwa kama jeshini


Toka kuamka, mnafanya usafi...mnaenda Assembly, mnaenda darasani (hapo hatujala kitu).

Tunatoka Darasani Saa Tano na Nusu asubuhi...Tunapeleka vikombe kwa ajili ya kunywa uji (na hapo uji unaweza usiupate
, kuna wakt uji hautoshi, wakt kikombe kinaibiwa)...Kunywa huo uji inaweza kuwa mpaka saa sita mchana ndo tunaanza kunywa)

Saa Nane mchana tunatoka Class, ila kula msosi iliweza kutukuta mpaka Saa kumi ndo tunakula....msosi full ugali maharage, sometimes wali, sometimes makande, sometimes nyama (nyama ilikuwa mara moja au mbili kwa wiki).


Jioni ugali harage.

Noma sana.
 
Ilikuwa ya wazungu ila baada ya uhuru tukawa wanafunzi wa mwanzo kusoma hapo, idadi kubwa ya walimu walikuwa ni wazungu na wanafunzi pia pamoja na wahindi wengi zaidi na waafrika.
Basi mzee wazazi wako walikuwa na uwezo wa kifedha
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…