Umeambiwa kaisaidia Chadema au kamsaidia Regia? Usikurupuke mkuu, Mbona kamshukuru Kafulila ambaye ni Mbunge mteule wa NCCR? Hizo ni shukrani tuu kama zile alizotoa JK kumshukuru kwanza Mke wake kabla ya kukishukuru chama chakekumbe saidi kubenea ni mkereketwa wa chadema!!! Silisomi tena gazeti la mwanahalisi maana litakuwa upande wa chadema tu badala ya kuandika hakika!!!!
Ndugu zangu wanaJF,habari za majukumu mbalimbali mliyonayo.
Napenda kuchukua fursa hii kuwashukuru wale wote kwa njia moja ama nyingine mmeshiriki kuniunga mkono kabla,wakati na baada ya uchaguzi.Ninathamini sana sapoti mliyonitendea sina cha kuwalipa ila Mwenyezi MUNGU atawalipa kwa niaba yangu.
Hapa ninawashukuru members wa JF tu wale walionisapoti nikiwa sijui na wale ambao nilikuwa ninafahamu.Napenda kuchukua fursa hii kuwatambua kwa majina.Samahani kwa wale ambao nitakuwa nimewasahau,orodha ni ndefu.
1.David Kafulila-ndiye aliyenihamasisha niingie CHADEMA Makao Makuu.
2.John Mnyika-Ndiye aliyenilea nilipofika makao makuu na kunisapoti mpaka dakika ya miwsho
3. Zitto Kabwe- ndiye aliyefundisha siasa za nje ya makao makuu,alinitetea kwa nguvu zote kwenye Kamati Kuu jina langu lisichakachuliwe baada ya kushinda kura za maoni
4.Dr Slaa-Amekuwa akinitia moyo na kunishauri
5.Freeman Mbowe- ndiye aliyeshauri nishiriki kwenye operesheni za chama nje ya makao makuu mfano Sangara n.k
6.John Mrema-Ushauri
7.Mzee Mwanakijiji-Alinitetea jina langu lisichakachuliwe baada ya kushinda kura za maoni,alipitia Ilani yangu na kuiboresha pamoja na kunifanyia kampeni.
8.Remmy-mchango wa hali na fedha
9.Dr Ndege ya Uchumi-Financial support
10.Erck Ongara-Financial support
11.Ben-Financial support
12.Saed Kubenea-Financial support
13.Dark City-Financial support
14.Maxence Melo-Muda wa maongezi
15.The invincible-Muda wa maongezi
16.FirstLady-Financial support
17.Firstlady1-Maombi mbele za MUNGU na kunipigia simu au kunisms kunipa moyo.
18.Bht-sms za kunitia moyo
Hawa ni wale walionisapoti nikifahamu wananisapoti lakini natambua kwamba kuna wengine mmenisapoti nikiwa sina habari,asanteni sana wote.
Nina washukuru sana wote na MUNGU awabariki sana.Tupo pamoja.Kwa wale ambao nitakuwa sijawataja majina yenu na mliniunga mkono kwa namna moja ama nyingine ninaomba radhi sana,sio lengo langu kuwasahau.
Aluta continua.
With Love Regia
Mpaka mwakani ndio ujiunge na CHADEMA,why?uko mbali sana?
tuko pamoja ,mapambano bado yanaendelea
Ni kweli wengine hawapendi kuanikwa majina yao hadharani,nadhani ni jambo jema kama ulishauriana nao kuwa utatoa majina yao humu kuwashukuru na wakakubali.Mimi Pia nakupongeza kwa jitihada ulilizozifanya ili kupata fursa ya kuwatumikia wananchi.
Lakini napenda kuwa Muwazi, SIJAFURAHISHWA NA APPROACH YAKO YA KUANIKA MAJINA YA BAADHI YA WATU HADHARANI. Amini usiamini jambo ulilolifanya lina tafsiri nyingi sana na hasa kutokana na baadhi ya watu uliowataja wana-influence kubwa kwenye jamii. Najua nitapingwa kwa hili lakini ndo hivo dada Regia nakupa constructive feedback.
Mwisho kabisa ukisoma between lines utagungua kuna issues nyingi za kuwafungua watu macho zimezungumzwa. Msinichukie Kwa sababu lengo ni kujengana pale mtu anapokosea, badala ya kujifanya kipofu!
Ndugu zangu wanaJF,habari za majukumu mbalimbali mliyonayo.
Napenda kuchukua fursa hii kuwashukuru wale wote kwa njia moja ama nyingine mmeshiriki kuniunga mkono kabla,wakati na baada ya uchaguzi.Ninathamini sana sapoti mliyonitendea sina cha kuwalipa ila Mwenyezi MUNGU atawalipa kwa niaba yangu.
Hapa ninawashukuru members wa JF tu wale walionisapoti nikiwa sijui na wale ambao nilikuwa ninafahamu.Napenda kuchukua fursa hii kuwatambua kwa majina.Samahani kwa wale ambao nitakuwa nimewasahau,orodha ni ndefu.
1.David Kafulila-ndiye aliyenihamasisha niingie CHADEMA Makao Makuu.
2.John Mnyika-Ndiye aliyenilea nilipofika makao makuu na kunisapoti mpaka dakika ya miwsho
3. Zitto Kabwe- ndiye aliyefundisha siasa za nje ya makao makuu,alinitetea kwa nguvu zote kwenye Kamati Kuu jina langu lisichakachuliwe baada ya kushinda kura za maoni
4.Dr Slaa-Amekuwa akinitia moyo na kunishauri
5.Freeman Mbowe- ndiye aliyeshauri nishiriki kwenye operesheni za chama nje ya makao makuu mfano Sangara n.k
6.John Mrema-Ushauri
7.Mzee Mwanakijiji-Alinitetea jina langu lisichakachuliwe baada ya kushinda kura za maoni,alipitia Ilani yangu na kuiboresha pamoja na kunifanyia kampeni.
8.Remmy-mchango wa hali na fedha
9.Dr Ndege ya Uchumi-Financial support
10.Erck Ongara-Financial support
11.Ben-Financial support
12.Saed Kubenea-Financial support
13.Dark City-Financial support
14.Maxence Melo-Muda wa maongezi
15.The invincible-Muda wa maongezi
16.FirstLady-Financial support
17.Firstlady1-Maombi mbele za MUNGU na kunipigia simu au kunisms kunipa moyo.
18.Bht-sms za kunitia moyo
Hawa ni wale walionisapoti nikifahamu wananisapoti lakini natambua kwamba kuna wengine mmenisapoti nikiwa sina habari,asanteni sana wote.
Nina washukuru sana wote na MUNGU awabariki sana.Tupo pamoja.Kwa wale ambao nitakuwa sijawataja majina yenu na mliniunga mkono kwa namna moja ama nyingine ninaomba radhi sana,sio lengo langu kuwasahau.
Aluta continua.
With Love Regia
kumbe saidi kubenea ni mkereketwa wa chadema!!! Silisomi tena gazeti la mwanahalisi maana litakuwa upande wa chadema tu badala ya kuandika hakika!!!!
Mimi Pia nakupongeza kwa jitihada ulilizozifanya ili kupata fursa ya kuwatumikia wananchi.
Lakini napenda kuwa Muwazi, SIJAFURAHISHWA NA APPROACH YAKO YA KUANIKA MAJINA YA BAADHI YA WATU HADHARANI. Amini usiamini jambo ulilolifanya lina tafsiri nyingi sana na hasa kutokana na baadhi ya watu uliowataja wana-influence kubwa kwenye jamii. Najua nitapingwa kwa hili lakini ndo hivo dada Regia nakupa constructive feedback.
Mwisho kabisa ukisoma between lines utagungua kuna issues nyingi za kuwafungua watu macho zimezungumzwa. Msinichukie Kwa sababu lengo ni kujengana pale mtu anapokosea, badala ya kujifanya kipofu!
Dada Regia na Keil;
Kwa miaka mingi nimekuwa mpinzani wa vyama vya siasa na nikaamua kujikalia bila chama. Ila kitendo cha Said Nkumba kushinda tena na kuwa mbunge wa Sikonge, kumenitibuwa sana na sasa nataka kufanya mikakati ya kuanza kumtoa mwaka 2015.
Ningeliweza kusema nijiunge na CCM ila nafahamu kuwa huko ana mizizi yake mirefu sana na ni vigumu kumtoa. Hivyo itakuwa vema kama ntaingia na gia ya kumshambulia ndani na nje ili mradi tu atolewe. Hadi mwakani nitakuwa nimeshajipanga tayari kuingia kwenye Siasa au lahh. Ndiyo maana hadi leo hii sina Chama na kwangu mie chama si muhimu sana ila cha muhimu ni maendeleo ya Wanyamwezi wangu wa Sikonge. Nitakuwa tayari kushirikiana hata na Shetani, kama tu atakuwa tayari kuwatumikia na kuwasaidia Wanyamwezi wangu hawa.
Ngoja kwanza nijiweke sawa kimawazo maana mwaka huu umekuwa mwaka wa kushindwa kwangu. Nimempigia kampeni Mwakalinga tangu mwaka jana, tukashindwa. Tangu miaka miwili iliyopita, nilianza kampeni za Dr. Slaa for President, uppsss!!! Inasemekana tumeshinda au kushindwa kwa point chache sana ila matokeo ya mwisho, NEC wamechakachua.
Hii inanipa wasiwasi mzito sana kwa hatua nzima ya kuacha shughuli zangu na kuingia kwenye Siasa. Kuna jamaa yangu mmoja ambaye kwa sasa yuko nje ya nchi na mwakani akirudi Tanzania, tutakaa na kujadili kwa kina hili swala. Tutakubaliana kati yangu na yeye nani aende na aende kwenye chama gani.
Tatizo la chama kwa Sikonge / Wanyamwezi ni kubwa sana. Kule watu wanafahamu CCM tu na hakuna zaidi. Kitendo cha kuingia kwa kutumia chama kingine inakuwa ni kujipa kazi ya ziada. Ila kuwepo tu vyama vya upinzani, kutaanza kuwapa watu wa huko Mwanga wa kufikiri kuwa Mtanzania anaweza kuwa kwenye chama chochote kile na hakuna vita itatokea. Hiyo tu inaweza kuanza kuwafungua watu macho na kuanza kufikiri au kuona mbali zaidi ya Sikonge.
Nitaendelea kuwa karibu na Kila Mtanzania bila kujali Chama ili mradi anaweka Maslahi ya Taifa mbele. Sintataka kuwa fanatic wa Siasa ambaye hata akisikia chama chake ni Mafisadi, Majambazi, wezi, wauwaji, watoa hongo, wazembe nk yeye bado anasimama na kusema bila wasiwasi Chadema Oyeeee!!!!!!
KEIL: Kabla sijanunua kadi ya Chadema, utakuwa wa kwanza kusikia na hapo ujuwe TUMEANZA KAZI. Kabla sijaenda Chadema, nafikiri nitataka kwanza kuwa na mazungumzo marefu na wewe maana msaada na ushauri wako, utakuwa ndiyo RISASI ya kwanza kwa Said NKUMBA.
Dada Regia,
Hongera kwa kampeni nzuri na pole kwa hujuma mbaya uliyofanyiwa. Kama nilivyosema nitakuwa tayari kutoa msaada wa kisheria pindi itakapohitajika. Lakini unatakiwa kufungua kesi mapema kwani muda ni siku 14 baada ya matokeo kutangazwa. Itakuwa vizuri nikipata simu yako ili tuweze kuwasiliana katika suala hilo.
Asante na mapambano yanaendelea kwa nguvu zote.