Shukrani zangu za dhati kwa wanaJF baada ya Uchaguzi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Shukrani zangu za dhati kwa wanaJF baada ya Uchaguzi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Regia Mtema, Nov 8, 2010.

 1. Regia Mtema

  Regia Mtema R I P

  #1
  Nov 8, 2010
  Joined: Nov 21, 2009
  Messages: 2,974
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 0
  Ndugu zangu wanaJF,habari za majukumu mbalimbali mliyonayo.

  Napenda kuchukua fursa hii kuwashukuru wale wote kwa njia moja ama nyingine mmeshiriki kuniunga mkono kabla,wakati na baada ya uchaguzi.Ninathamini sana sapoti mliyonitendea sina cha kuwalipa ila Mwenyezi MUNGU atawalipa kwa niaba yangu.

  Hapa ninawashukuru members wa JF tu wale walionisapoti nikiwa sijui na wale ambao nilikuwa ninafahamu.Napenda kuchukua fursa hii kuwatambua kwa majina.Samahani kwa wale ambao nitakuwa nimewasahau,orodha ni ndefu.

  1.David Kafulila-ndiye aliyenihamasisha niingie CHADEMA Makao Makuu.
  2.John Mnyika-Ndiye aliyenilea nilipofika makao makuu na kunisapoti mpaka dakika ya miwsho
  3. Zitto Kabwe- ndiye aliyefundisha siasa za nje ya makao makuu,alinitetea kwa nguvu zote kwenye Kamati Kuu jina langu lisichakachuliwe baada ya kushinda kura za maoni
  4.Dr Slaa-Amekuwa akinitia moyo na kunishauri
  5.Freeman Mbowe- ndiye aliyeshauri nishiriki kwenye operesheni za chama nje ya makao makuu mfano Sangara n.k
  6.John Mrema-Ushauri
  7.Mzee Mwanakijiji-Alinitetea jina langu lisichakachuliwe baada ya kushinda kura za maoni,alipitia Ilani yangu na kuiboresha pamoja na kunifanyia kampeni.
  8.Remmy-mchango wa hali na fedha
  9.Dr Ndege ya Uchumi-Financial support
  10.Erck Ongara-Financial support
  11.Ben-Financial support
  12.Saed Kubenea-Financial support
  13.Dark City-Financial support
  14.Maxence Melo-Muda wa maongezi
  15.The invincible-Muda wa maongezi
  16.FirstLady-Financial support
  17.Firstlady1-Maombi mbele za MUNGU na kunipigia simu au kunisms kunipa moyo.
  18.Bht-sms za kunitia moyo

  Hawa ni wale walionisapoti nikifahamu wananisapoti lakini natambua kwamba kuna wengine mmenisapoti nikiwa sina habari,asanteni sana wote.

  Nina washukuru sana wote na MUNGU awabariki sana.Tupo pamoja.Kwa wale ambao nitakuwa sijawataja majina yenu na mliniunga mkono kwa namna moja ama nyingine ninaomba radhi sana,sio lengo langu kuwasahau.

  Aluta continua.
  With Love Regia
   
 2. K

  KunjyGroup JF-Expert Member

  #2
  Nov 8, 2010
  Joined: Dec 7, 2009
  Messages: 352
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  Karibu na hongera. Mapambano daima
   
 3. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #3
  Nov 8, 2010
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,435
  Likes Received: 19,789
  Trophy Points: 280
  tuko pamoja ,mapambano bado yanaendelea
   
 4. Kaizer

  Kaizer JF-Expert Member

  #4
  Nov 8, 2010
  Joined: Sep 16, 2008
  Messages: 24,647
  Likes Received: 1,475
  Trophy Points: 280
  Aluta Continua Regia, tupo pamoja. Hongera kwa uthubutu wako huo...unaweza na Inshallah utapata nafasi ya kuwatumikia wana Kilombero wakati mwingine. K4C
   
 5. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #5
  Nov 8, 2010
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,503
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  Mie sikukusaidia zaidi ya maombi.

  Itakuwa vema badala ya kuwaambia hao ASANTE kwa msaada wao, basi na wewe usaidie wengine kuwaingiza Chadema na kuwalea. Hao wakija kusema asante, basi uwaambie wawape asante hao walioanza kukujenga wewe. Nina imani watafarijika zaidi kwa kujua kazi zao na misaada yao imeendelea zaidi na zaidi na kufika mbali ya walipotegemea.

  NUSU UTANI NUSU KWELI: Nategemea kuwa mgombea wa Sikonge mwaka 2015 na nina imani hautaniweka pembeni. Tatizo kwa leo hata kadi sina ila nina tegemea hapo mwakani kuwa nitakuwa Mwanachadema na kuhitaji sana misaada yenu katika Siasa na kufungua tawi la Chadema hapa Sikonge maana mwaka 2015, kila jimbo Tanzania lazima liwe na Mgombea ubunge wa Chadema.
   
 6. Anyisile Obheli

  Anyisile Obheli JF-Expert Member

  #6
  Nov 8, 2010
  Joined: Dec 13, 2009
  Messages: 3,304
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Mapambano bado yanaendelea dada angu songa mbele tuko pamoja, na tutakuwa mfano wa kuigwa
  kwa kuitumikia jamii ya watanzania
   
 7. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #7
  Nov 8, 2010
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  Nilikusapoti na kukuombea.
  tutaendelea kuwa pamoja Regia.
  Naamini umejiandaa kuburuza mtu mahakamani kurejesha ushindi ulioporwa. wewe ni mshindi you must walk like the one.

  Pamoja sana
   
 8. K

  Keil JF-Expert Member

  #8
  Nov 8, 2010
  Joined: Jul 2, 2007
  Messages: 2,214
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Mkuu Sikonge,

  Naomba isiwe utani, fanya kweli. Kama kweli una nia inabidi summer ya mwaka kesho shughuli hiyo ianze rasmi. Mpaka kufikia 2015 kitakuwa kimeeleweka.

  Ahadi yangu iko pale pale [kusaidia kupiga debe, haikuwa utani, nilikuwa serious siku niliposema], nitasaidia kupiga debe kuanzia Kipanga cha Katisho mpaka Mtakuja. Wewe nitakuachia maeneo ya Chabutwa, Kikungu, Ipole, Sikonge yenyewe, Tutuo, Mole na maeneo yote yanayofuata baada ya Kipalapala.

  Nina uhakika ukiweka ka-network kazuri kila Kata unaweza kupata mpiga debe wa uhakika na wa kuaminika na kama anafahamika kwenye hayo maeneo inakuwa ni rahisi zaidi kukuuza plus sera za kueleweka.

  In addition, wakati wa kuweka network ni vyema ukawa una-identify potential candidates kwa ajili ya nafasi za madiwani. Wagombea udiwani watarajiwa ni muhimu sana kuwa-identify mapema kwa kuwa ni rahisi kufanya kampeni kama timu badala ya kusubiri mpaka baada ya final nominations.
   
 9. K

  Keil JF-Expert Member

  #9
  Nov 8, 2010
  Joined: Jul 2, 2007
  Messages: 2,214
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Hongera Regia kwa kutikisa mizizi ya Chama Tawala kwenye jimbo lako. Yaliyotokea yasikukatishe tamaa, yachukulie kama changamoto ya mapambano na pia yawe ni chachu kwa ajili ya wengine watakaotaka kuingia kwenye kinyang'anyiro kingine cha 2015.
   
 10. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #10
  Nov 9, 2010
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Dada Regia,

  Naomba pia upokee shukrani zangu kwa juhudi ulizozionesha katika mpambano huu ambao naamini ni mwanzo tu. Natumai somo la hii kampeni ni zaidi ya PhD na litatusaidia siku za usoni. Hata hivyo nasikitika binafsi kwamba nimeshindwa kushiriki kampeni za mwaka huu kwa kiwango nilichotamani kutoka na majukumu mengine ambayo pia ni muhimu sana. Nikipata nafasi nitakutafuta ili tuongee ki-undani zaidi.

  Kwa mwenenendo wa Uchaguzi huu, ..naamini safari ya kuikomboa Kilombero na Tanzania nzima ndo imaanza na footprints za 2010 zitabaki kuwa mhuhuri usiofutika. Kama nilivyosema huko nyuma," after Oct. 31 2010, Tanzania will never be the same again"!
   
 11. Regia Mtema

  Regia Mtema R I P

  #11
  Nov 9, 2010
  Joined: Nov 21, 2009
  Messages: 2,974
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 0
  Mpaka mwakani ndio ujiunge na CHADEMA,why?uko mbali sana?
   
 12. MwanaHaki

  MwanaHaki R I P

  #12
  Nov 9, 2010
  Joined: Oct 17, 2006
  Messages: 2,403
  Likes Received: 122
  Trophy Points: 145
  Safari bado ni ndefu. Nitumie namba yako kwa PM, nitakuwa nakupa SMS za ushauri na muda wa maongezi pia, nipatapo fursa, nitakuchagia!
   
 13. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #13
  Nov 9, 2010
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,124
  Likes Received: 1,707
  Trophy Points: 280
  Asante mama kwa yote na pole na mchakato mzima, nilikuwa pamoja nawe katika kuwahamasisha watz wauone ukweli. na namshukuru mungu vijana wengi kule home B'mulo wamekiunga mkona chama chetu na tumempata mpiganaji Mbassah dr wa ukweli. jumkumu tunalo kuwa nalo ni kujiandaa kwa uchaguzi unaofuata ikiwa ni pamoja na kukiimarisha chama hadi kule vijijini kwani hawa mafisadi wanatumia kutoelewa wa wabongo kama mtaji wao kisiasa.

  Tunapaswa kuwaelimisha vilevile mawakala na watendaji wa chama chetu wa ngazi za chini ili wawe na msimamo wasikubali kushawishika kwani mafisadi wanautumia umasikini wetu kama kiboko cha kutuchapia.

  Tusikubali kurubuniwa na tusifee moyo Mapambano yamekwisha na mapambano yameanza tena kwa moyo wote.

  Maisha na utendaji mwema.

  Gene!
   
 14. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #14
  Nov 9, 2010
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  So where the hell is Kiranga in this list??????????? Anywayz Regia all the best the journey has just began.
   
 15. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #15
  Nov 9, 2010
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,435
  Likes Received: 19,789
  Trophy Points: 280
  dont call him like that...hujui kuwa watu wakikucriticise ndio unajuwa where is your mistakes and then you can be able to correct them...but if no one to criticise you ..lazima utajisahau a.k.a % kubwa ya wana ccm
   
 16. Malafyale

  Malafyale JF-Expert Member

  #16
  Nov 9, 2010
  Joined: Aug 11, 2008
  Messages: 11,214
  Likes Received: 3,626
  Trophy Points: 280
  Naichukua Kyela bila ubishi wowote Mwaka 2015;vuguvugu la Mageuzi Kyela limewaingia wakazi wa Kyela na ndiyo maana kura za U-Rais wamegawana JK na Dr Slaa lkn Ubunge wakampa Mwakyembe huku wakimtaka atimizie ahadi yake aliyoisema kuwa huu ni muhula wake wa mwisho kugombea!

  Maandalizi ya 2015 yanaanza sasa;Kyela nitaichukua bila ubishi wowote ule;na tofauti kubwa kati ya Mwakyembe na Malafyale(mimi) ni kuwa"Wakati Mwakyembe alikuwa Mbunge wa Taifa;mm nitakuwa Mbunge wa kuwakilisha na kutafutia ufumbuzi Matatizo ya wana Kyela Bungeni maana ndiyo walio nipigia kura na kunipeleka Bungeni!

  Nitawaletea mwaliko rasmi wana JF muwepo kijijini kwangu Talatala-Ipinda siku natangaza nia ya kugombea Ubunge wa Kyela mapema tu mwakani!
   
 17. K

  Kadogoo JF-Expert Member

  #17
  Nov 9, 2010
  Joined: Feb 26, 2007
  Messages: 2,072
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  kumbe saidi kubenea ni mkereketwa wa chadema!!! Silisomi tena gazeti la mwanahalisi maana litakuwa upande wa chadema tu badala ya kuandika hakika!!!!
   
 18. K

  Keil JF-Expert Member

  #18
  Nov 9, 2010
  Joined: Jul 2, 2007
  Messages: 2,214
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Kama utakuwa unagombea kupitia CCM, mimi naomba usinipe mwaliko.
   
 19. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #19
  Nov 9, 2010
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Mbona magazeti yako mengi? Ukiacha Mwanahalisi utasoma Rai, Mtanzania na Uhuru. Au wewe ndiye ulikuwa unamuungisha nakala zote anazotoa kwa week?
   
 20. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #20
  Nov 9, 2010
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,435
  Likes Received: 19,789
  Trophy Points: 280
  :blah::blah:
   
Loading...