Shukrani kwa ukaribisho - Anna Tibaijuka

Shukrani kwa ukaribisho - Anna Tibaijuka

Profesa Anna Tibaijuka,

Ni kweli ulisema maneno haya hapo chini au uliandikiwa na maofisa wa Wizara hivyo ukalazimika kuyasema mbele ya wawekezaji? Kama kweli uliyasema, una vielelezo gani vya kitakwimu na kisheria vinavyothibitisha kuwa huo ni ukweli?


- The Minister for Lands, Housing
& Human Settlements Development, Professor Anna Kajumulo Tibaijuka, to the Tanzania Agribusiness Investment Showcase Event
<http://www.sagcot.com/uploads/media/3._SAGCOT_Showcase_Min_Land.pdf>​
​
​
 
karibu jamvini'unajisikiaje kufanya kazi na kiongozi dhaifu??naomba kujua kuhusu viwanja vya Tabata Kinyerezi'ni lini mtatoa hati ili tuendelee na ujenzi?
 
Karibu mama ni matumaini yangu kuwa utayajibu yale tunayofikiri yapo ndani ya uwezo wako
 
Karibu Mama Tibaijuka. Mimi pongezi zangu ni kwa jinsi alivyoiangalia JF kwa mtazamo wake.

JF imepondwa na kuonekana dude hatari ndani ya bunge. Yeye kwa sifa zake za kitaaluma, kisiasa na kiuongozi kaliangalia eneo hili kwa jicho lake na kuona kitu, nampongeza.

Hapa JF utasikia au kusoma mengi, muhimu sana ni kuwa kati ya 10 lile moja litakalokugusa ukalifanyia kazi hapo utakuwa umefanya kazi ya taifa na wala si ya JF. Sehemu kubwa ya wanaJF na wageni wasomaji ni wale wanaotoka kule kusikosikika na hii ni fursa yako na wengine tulio nao humu kupata habari za ''saiti''.

Nina Maswali machache kwa kuanzia
1. Kuanguka kwa jengo:
Tumesikia zimeundwa tume kuchunguza tukio hilo. Huko nyuma ziliundwa tume zikachunguza na habari zake hatukuzisikia tena. Je, hii tume ya sasa unatuhakikishiaje kuwa ni tofauti na zile zilizopita?

2. Wakati uchunguzi unaendelea kuna watu ambao walipaswa wakae pembeni ili kutoa nafasi ya uchunguzi huru.
Wahusika bado wapo maofisini. Uchunguzi huu, uhuru wake upo wapi na je dhana ya kuwajibika au kuwajibishwa inaanzia wapi na kuishia wapi na kwanini hadi sasa sehemu kubwa ya watuhumiwa wa uzembe au njama wapo makazini.

3. Ukiwa kama kiongozi mstaafu wa UNHABITAT ninahakika unafahamu vema tatizo la ujenzi wa makazi holela.

Jiji letu la Dar ni mfano wa upangaji mbovu sana wa majiji duniani. Hatuoni hatua zozote zile za kurekebisha hali hiyo.
a) Hali iliyopo inarekebishika au ndio tuanze kujenga jiji lingine nje ya hili lililopo?
b) Tatizo la makazi hovyo na holela chanzo chake ni nini hasa, je, ni siasa au ukosefu wa wataalam?

Ahsante
 
Mama
Ningependa useme mawili matatu kuhusu
Matatizo yanayotokea Lolliondo sasa.

Uko upande wa Wananchi au Waarabu wa UAE?
Ningeomba ujibu hili Asante .
 
Ninaomba kuchukua fursa mbali na kumkaribisha Mh.Tibaijuka pia Kwa kumpongeza kuchukua uamuzi Wa kujiunga na jukwaa hili.

Ningependa kuwakilisha swali langu kwako linalohusu ardhi. Swali langu ni Kama ifuatavyo:

Ni wapi umefikia Katika hatua zako na jitihada gani unafanya kurejesha VIWANJA VYA WAZI vilivyokuwepo Katika mikoa mikubwa Kama Dar, Mwanza na Arusha? Pia kuna Barabara zilizokuwa zinatakatiza mitaa ambazo Watu wamejenga nyumba na kuzuia mitaa Una taarifa na hilo? Na nini mkakati wako? Pia kwa nafasi yako, nini mkakati wako na itachukuwa kipindi gani kumaliza hili tatizo?
 
karibu mama,naamini utatoa dukuduku zilizojaa katika vichwa vyetu kuhusu ardhi
 
kama kashindwa serikalini sioni cha ajabu atakacho kifanya humu, nikikumbuka maneno aliyo wajibu wakazi wa kigamboni, maeneo kutopimwa mpaka sasa, nisawa na kumkataza mtu kucheka eti anakupigia kelele wakati we unalia.kulia na kucheka zote ni kelele
 
Karibu sana Prof.
Nategemea hutajiondoa hasa pale critics zitapokuja kuzidi.
Otherwise, wewe ni mmoja wa dhahabu chache katika jalala 'CCM'
Karibu sana
 
Karibu sana Prof. Binafsi naona mwamko umeanza kutokea miongoni mwa wazee wa CCM na wameanza kutambua ujana si upinzani kama baadhi ya vijana wenzetu akiwemo Nape anavyoelewa. Tafadhali weka ushawishi kwa wazee wengine wa CCM hasa mawaziri wajiunge hapa ili tuweze kuwafikia.

Kuhusu majukumu yako, nilitaka kufahamu hivi kwa nini Wizara yako inaendelea kuwaachia wananchi kuendeleza makazi yasiyopimwa (squatter) ili hali kuna Tume ya Mipango ya Ardhi?. Tulitarajia kwa kuwa huko nyuma tulikosea na kusababisha miji isiyo na mipango, Wizara ingeanza kidogo kidogo kuwalazimisha wananchi kuzingatia ujenzi wa makazi yenye mipango hata kama sio rasmi. Cha kushangaza leo hata katika maeneo yaliyopimwa wananchi wanaendeleza ujenzi holela.

Pili, nilitaka kufahamu iwapo kuna tofauti yeyote ya umiliki Ardhi ya mwananchi wa kawaida iwe kupitia hati ya kimila au hatimiliki chini ya sheria Na.4 ya Ardhi ya mwaka 1999 na ile anayopewa Mgeni kupitia TIC? Bimafsi naona kuwa masharti yaliyopo ya umiliki japo kwa mgeni haruhusiwi kuuza lakini muda wa ukomo wa umiliki ni ule ule na manufaa ya kuitumia ardhi na haki nyinginezo ni kama zinafanana na kwa ardhi ya mwekezaji ni kama inapewa kinga kubwa kuliko ya wazawa.

Je, iwapo sheria za Ardhi hazizuii mmiliki mzawa kumpa ardhi asiye mzawa kwa njia ya urithi kama ilivyowahi kuamriwa na hukumu fulani ya Mahakama Kuu ya Mhe.Jaji Twahib, Wizara haioni sasa ipo haja ya kurekebisha Sheria zilizopo za ardhi ikiwemo ya Usajili wa Ardhi (Land Registration) ili zioane na kuwa na azima moja kuzuia wageni kuitumia ardhi yetu kwa jinisi yeyote ile kinyume na malengo ya Sera ya Taifa ya Ardhi?
 
Karibu sana ukumbini, swali langu kwako hapo wizarani kuna wafanyakazi wanashirikiana na matapeli wa viwanja kufanya udanganyifu na kuwaibia wananchi hasa katika maeneo ya mbezi beach, kawe, kunduchi.

Matapeli wa viwanja watatumaliza mama hapo wizarani kwenu bila ya kuwa na mtu unatapeliwa na kuambiwa hati yako ni feki wakati umenunua kihalali kiwanja na umekifanyia taratibu zote hapa mwanzo.

Ahsante Mama Tibaijuka.
 
Mojawapo ya Wizara zinazoibomoa jamii ya Tz na kuharibu future ya nchi, ni hii ya Ardhi na Makazi. kila ukifungua magazeti, redio au Tv hutokosa habari za mitafaruku kwa sababu ya land-grabbing kwa visingizio vya uekezaji. Sasa hivi watz wavujajasho wamekua raia wa daraja la 2 au la 3 huku matajiri na wawekezaji uchwara ndio wanaonekana watu wa maana mbele ya serikali ya Tz inayojinadi ni serikali sikivu. Makabwela wamekua kama wakimbizi ktk nchi yao wenyewe, wakiminywa hata umiliki wa ardhi zao za kimila.

Ktk muktadha huu mie binafsi ningeona ni busara zaidi kwa waziri mwene dhamana husika kushughulika na haya matatizo badala ya kufungua profile JF na kuanza kupiga porojo. Mi nadhani kila wizara inayo maafisa habari au maafisa uhusiano ambao ndio haswa wanapaswa kupiga spins kwa niaba ya wizara husika.

Mwito: Ndg walipakodi wa Tz, Waziri kupiga porojo JF ni upotevu wa kodi zetu, tusikubali hizi sanaa nyepesinyepesi. Tunahitaji waziri 'adelive' kwa yale majukumu aliyokubali kwa kiapo na sio atuuzie maneno matupu JF.
 
karibu prof, ila ukae ukijua huku kuna watu wenye akili zao na kuna watu wenye akili za kuazima, utuvumilie sote usije ukakaa wiki 2 alafu ukajitoa, once again ya heartly welcome
 
karibu mama ana tibaijuka.....hivi ni kweli kuwa mama lwakatare,yule mchungaji na mbunge wa viti maalumu wa chama chako ana tabia ya kuvamia maeneo ya wazi hasa kwenye nyumba anayo kaa....samahani lakini mama....
 
Hoja yangu ni kuhusu nyumba ya Mh. Getrude Rwakatare iliyojengwa ufukweni. tunafahamu kuna nyumba zimebomolewa kule ufukweni. Mbona inapofika kwenye kubomoa nyumba za wakubwa kunakuwa na kigugumizi? au wao wako juu ya sheria na kuwa ni untouchable? Tunasubiri kwa hamu kuona serikali yetu ikilifanyia haki jambo hili kwa maslahi pana ya taifa
 
Mradi wa Kigamboni vipi? Mimi tahariri nyingi siangalii, je mradi wa Kigamboni mmefikia wapi? Wananchi tupo upande gani? Hebu rudia yale majibu uliyoongea pale viwanja vya Machava
 
Karibu sana mama Anna Tibaijuka.Bila shaka utakuwa chachu ya viongozi wengine wengi zaidi kujiunga hapa jamvini.Stay blessed
 
Karibu jamvini.

Mhe. Anna Tibaijuka binafsi nimefurahia ujio wako humu jukwaani, kwa kuwa nina imani ya kwamba tutashiriki kikamilifu katika kukupa mawazo ya kuboresha sekta ya ardhi na uendelezaji makazi, pia unaweza kutueleza ni vikwazo gani vinakabili sekta husika maana maendeleo ya makazi yanagusa wananchi wengi hasa vijana waishio mijini, kwani maendeleo ya sekta hii hapa nchini sio ya kuridhisha kabisa.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom