Mama thanks na tumefarijika sana. Nina imani kupitia JF utapata mawazo endelevu ya kuijenga nchi yetu ili kufikia viwango vya juu na vya kimataifa. Kwa kuanzia, tunafurahi kwa hatua Wizara inazozichukua kuubadilisha mji wa Dar es Salaam ingawaje harakati hizo kwa maoni yangu zinakwenda pole pole sana tofauti na miji mingine duniani ikiwa ni pamoja na Rwanda - Kigali, Nairobi (ingawaje wao walianza muda mrefu), etc.
Mji wa Kigamboni utabadilisha taswira ya mji wa Dar, lakini pia ni vizuri upimaji unaoihusisha serikali kuu moja kwa moja ukafanywa kwenye maeneo mengine kama Kibaha, Kisarawe, Bagamoyo, n.k. Upimaji binafsi na wa halmashauri umepelekea kufanya viwanja ghali na kufaidisha watu wachache.
Mji wa Dar unakuwa kwa kasi na ujenzi wake unaendelea kuwa wa holela sana. Hata yale maeneo yaliyopimwa zamani kama Kinondoni, Magomeni, Sinza na Mbezi yameanza kuwa na utaratibu wa ujenzi usiofaa. Maduka na baa kila mahali!!! Hii si sawa kabisa. Hata barabara za mitaa zilizowekwa kwa kipimo maalum zimeminywa. Viwanja vya wazi vimevamiwa au na matajiri au watu walioko kwenye system ya serikali (hili nadhani unalijua). Kwa kweli Dar es Salaam, Arusha, Mbeya etc inatia aibu.
Nilipata mgeni juzi kutoka US aliyepitia Nairobi kwanza kikazi. Aliniambia: "Ni mara yangu ya kwanza kufika Afrika. Watanzania ni watu wazuri na wakarimu ila nilipokuwa angani kabla ya kutua, niliona kama naelekea kwenye kijiji kikubwa sana Afrika, kumbe ndio nimefika Dar. Nairobi ukifika ukiwa angani unaona pattern ya plan ya mji".
I felt embarrassed kwani alikuwa anasema ukweli na mimi sikuwa na la kusema". Ili kuleta mabadiliko ya mjii huu tunatakiwa kufanya maamuzi magumu (hata kwa gharama) ikiwa ni pamoja na kufuata city/area plan ya mwanzo kuhakikisha zimefuatwa, kupima maeneo mapya, kusaidia sekta binafsi kuingia kwa nguvu kubwa kwenye mortgage/housing project (Hii itasaidia kurasimisha na kuboresha maeneo yaliyojengwa hovyo kama Manzese, Mburahati, etc).
Kuwe na coordination baina ya Wizara ya ardhi na nyingine ili kuondoa overlaps (e.g. utoaji wa huduma maeneo yasiyo rasmi), Maeneo ya wazi au public kama vile eneo la ilipokuwa inachimbwa kokoto la Kunduchi kuendelea kuwa public (lile eneo la Kunduchi bila shaka ni mali ya serikali lakini hadi sasa limevamiwa na vibanda vimetapakaa kila mahali (another upcoming Manzese along Mwai Kibaki Rd).
Hapa ni uzembe wa serikali kwani mwisho wa siku serikali hiyo hiyo itatumia kodi za wananchi kulipa fidia isiyokuwa na msingi. Najua Lowassa alishaanza kupafanyia kazi kwa kuondoa watu na sijui ni kwanini watu wameruhusiwa kujenga pale leo hii). Makosa ya sasa ni gharama ya baadaye. Ni hayo tu kwa sasa!!