Shukrani kwa ukaribisho - Anna Tibaijuka

Shukrani kwa ukaribisho - Anna Tibaijuka

Joined
Apr 20, 2013
Posts
15
Reaction score
424
WanaJF

Walionikaribisha – Ninawashukuru. Sikutegemea wala kustahili ukarimu huu. Asanteni sana.

Walioona sistahili
- Ninawapongeza kusema ya moyoni mwao.. Naomba mnikubali kama siyo kwa nafsi yangu, kwa sababu nyie kama mimi ni waumini wa demokrasia ya kweli. Kila mtu awe na haki ya kushiriki katika Jukwaa hili. Hata wa miaka 47 tunaweza tukaleta ya historia ambayo ndiyo hujenga ya kesho. Wenzetu wanasema " A people with no history have no future".

Na mbona nimechelewa wengine wamehoji?
Ni kweli. Ila, nadhani ni vyema kutambua kwamba Jukwaa hili, wengi wenu mkiwa vijana, ilibidi lipewe nafasi kukua na kuchanua kabla watu kama mimi hatujaingia na mawazo ambayo labda yangelifanya kusinyaa. Sasa limekomaa, hoja na maswali muhimu yanajitokeza kwa hiyo tunaweza tukajibu inapostahili. Ninawapongeza waanzilishi na Gold Members. Hongereni sana.

Imeulizwa, je nitashiriki mara kwa mara?

Wakati ninaomba "moderator" anisaidie kukusanya maswali yenu yote yanayohusu kazi yangu, na nitakuwa ninayajibu baada ya kufanya utafiti ili nilete "evidence based reporting" katika jamvi letu, kwa sasa niseme tu katika dunia ya leo, viongozi hatuna budi kuwa kwenye majukwaa ya wananchi hasa vijana, taifa la leo na kesho.

Nilipokuwa UN tulikuwa tunahimizwa na Katibu Mkuu wetu Kofi Annan kukutana na vijana MTV. Ni utamaduni ambao nimeona unaweza ukatufaa pia Tanzania. Pia kizazi changu tulimshuhudia Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere akifika mara kwa mara Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kuongea na wanafunzi na walimu. Chuo kilikuwa kimoja. Sasa ni vingi. Jamvi linatusaidia kuwafikia kwa pamoja. Wanasema "technology shapes institutions". Tunakwenda na wakati.

Kazi ni nyingi ninaweza kuchelewa kujibu hoja zenu ila kwa msaada wa mode nitajitahidi.

Mbarikiwe. Pamoja tunaijenga Tanzania imara leo na kesho.


Mama Tibaijuka
 
Naam, tunafurahia kujumuika nasi.

Na kwa hakika hakuna suala linalogusa maisha ya watu wetu sana kama suala la Ardhi. Na kama sehemu ya kuanzia binafsi ningependa kujua sana suala la kubomoka kwa jengo Dar hali ikoje hadi hivi sasa. Ulitoa maagizo ya baadhi ya majengo kuvunjwa na mengine kuchunguzwa kama yana uimara unaostahili au kama yamefuata vigezo vya ujenzi. Hili nalo limefikia wapi?

Lakini zaidi ni kwanini jengo lile liliachwa kwa muda mrefu vile hadi kuja kuanguka hasa baada ya matukio mengine kama hilo miaka michache tu iliyopita?
 
Ok,
Yapo maswali ambayo tumeuliza kwenye thread ya ukaribisho, unaweza ukaanza kuyajibu.

Otherwise karibu tena!!
 
Karibu saana Prof. Anna Tibaijuka.

Mie ni moja wa wengi hapa jamvini ambao tupo so humbled kwa uwepo wako hapa. Tambua kuwa tunataraji mengi sana toka kwako HASA yanayogusa nyanja yako na yaliyo ndani ya uwezo wako. Na kwa kiasi kikubwa sana nina imani kuwa wewe pia hutakuwa disappointed na hutatoka kapa. Imani yangu utapata mengi pia bila kujalisha ni kwa misingi ya chanya ama hasi.

Naomba nikiri kuwa ni faraja na furaha kwa kutambua na kukubali kwako kwa Jukwaa na kuona kuwa limekuwa kwa kiasi cha kuridhisha. Kuongezeka kwa viongozi, ni kuongezeka kwa hoja na majibu ya hakika na hivyo kuongezeka kwa mawasiliano kati ya Viongozi wetu na siye ambao mnatuwakilisha.

Hopefully utakuwa umefungua mlango kwa Viongozi wengi wa juu. Karibu Saana!
 
Last edited by a moderator:
Imeulizwa, je nitashiriki mara kwa mara?
Wakati ninaomba "moderator" anisaidie kukusanya maswali yenu yote yanayohusu kazi yangu, na nitakuwa ninayajibu baada ya kufanya utafiti ili nilete "evidence based reporting" katika jamvi letu, kwa sasa niseme tu katika dunia ya leo, viongozi hatuna budi kuwa kwenye majukwaa ya wananchi hasa vijana, taifa la leo na kesho.

Safi sana mama Tibaijuka, umetoa kipande cha habari kinachoeleweka sana, ila mi napenda kukupa tahadhari hapo kwenye red, majibu yawe "evidence-based reporting" kwelikweli, vinginevyo ukija na majibu ya Bungeni, mmh! humu jamvini kuna vijana wana facts zinazojumuisha picha, sauti, historia na vinavyohusiana.
 
Karibu sana mama Anna Tibaijuka! Nami kama Mwanakijiji alivyouliza, niongezee tu kwamba kama Wizara, mmemchukulia hatua gani Mkurugenzi wa NHC kwa uzembe uliotokea hadi maafa yanatokea katika jengo lile wakati yeye ni Strategic Joint Venture Partner. Mengi yaliongelewa kuhusiana na NHC kuhusika kwake katika hili kama ilivyo katika thread hii https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...ra-yamweka-kitimoto-mchechu-na-timu-yake.html
 
Swali langu ni la kisiasa zaidi niwie radhi. Huku mitaani unasemwa semwa kama mmoja kati ya watu ambao huenda wakaomba kuwania kiti cha urais kwa ticket ya ccm, je unasemaje kuhusu hili?
 
Huenda sasa tukapata maoni yako kuhusu wananchi wa Loliondo waliozaliwa na kukulia katika ardhi yao kuwa inakuwaje wananganywa ardhi hiyo ili kupewa Mwarabu? Ni kwa sababu ni watu wa kuhamama au ni kwa sababu gani? Je nani mtetezi wao?
 
Asante sana mama ANNA,,,
umeonesha njia kwa wengine,na uwaambie wengine kuwa wasiishambulie jf wakat huwa wanaiskia,waambie waingie hapa
 
hon it is my honour to welcome you to the interesting forum,we expect many more ministers will join this forum
 
Sasa naamini kuwa mama amejiunga, Tupo pamoja mshawishi na mheshimiwa rais nae ajiunge.
 
Mama Tibaijuka binafsi nilifuatilia maisha yako kwa kifupi hasa pale ulipotaka UWT ijitegemee wakubwa wa CCM wakakuona mpinzani, lakini Mungu si athumani sasa hivi uko nao mnakula nchi kwa pamoja!
 
:welcome::welcome::welcome::welcome::welcome::welcome::welcome:Karibu sana mama etu mpendwa Anna Tibaijuka
 
Hongera mama kwa ujasiri wa kuingia kwenye jukwa hili,ila mi nakuhurumia maana maswali mengine yatakuwa magumu na ukizingatia nafasi yako kama waziri nahisi itakuwa ngumu kwako kujibu baadhi ya maswali katika kutunza siri za serikali.(baraza la mawaziri)........Mikataba ni siri?????
 
Back
Top Bottom