Shukrani kwa ukaribisho - Anna Tibaijuka

Shukrani kwa ukaribisho - Anna Tibaijuka

Adhere to true democracy, be flexible to upcoming Movement For Change...karibu jamvini..
 
We mama mi huwa nakukubali sana
Unafiki tu huo, unamkubali kwa lipi? Katika wizara zenye ukiritimba wa hali ya juu ni pamoja na hii wizara tangu enzi za Mwinyi na hata sasa. Ana lipi la kukubaliwa huyu mama? Watu hadi hivi sasa Tanzania hii wanakwenda kama headless chicken. wanajenga wanavyojisikia kwa sababu serikali haipimi viwanja na hata kwa wale waliojenga kiholela inatoa lessen za makazi bila kutengeneza barabara. Unakuta mitaa ina vichochoro vya kupita kwa miguu tu hakuna hata barabara angalau ya kupita mkokoteni achilia mbali gari la wagonjwa au zima moto na bado wizara ya ardhi inatoa lessen ya makazi maeneo kama haya.

Sasa hiyo tisa, kumi nenda kawaombe watu wa wizara waje wakupimie kiwanja ambacho umekinunua. Utakula jeuri yako. Kama huna fungu la kutosha hutakaa upimiwe, otherwise utaishia tu kuletewa masurveyors wa kuja kusoma GPS kwa gharama ya up to 200000. na Kazi iishie hapohapo. This is one of the most disorganized ministry in the country. Bado tukae chini kumpongeza? Kwa lipi?

Bado sijapata cha kunishawishi kumpongeza hata kidogo. Prof. Anna Tibaijuka ni failure Minister kama walivyoshindwa akina Chiligati na wengine wengi kuendesha hii wizara.
 
Last edited by a moderator:
Karibu sana JF natumaini umefungua njia kwa viongozi wengine wa kitaifa.
 
Prof. Tibaijuka,

Kuna sera iliyoanzisha na Rais Mkapa ya kuwawawezesha watu wa chini kwa kurasimishia ardhi (kuwapimia ardhi na kuwapa hati ili waweze kuitumia kutafuta mikopo, nk.). Kwa nini wizara yako/administration ya awamu hii imetupilia mbali mkakati huu (uliopokelewa vizuri na watu wengi)?

Karibu.
 
Karibu Waziri. Tutajifunza mengi kutoka kwako. Pia huenda nawe utachota hekima kutoka kwetu.
 
Karibu sana mama
Hopefull tutajifunza mengi kutoka kwako!
 
Hongera sana Mama etu uliye makini. Tunaomba umshaur na Anna Makinda ajiunge, tuna maswal mengi ambayo nahisi yeye atakua na majibu.
 
Karibu sana Mama Tibaijuka, sina wasi wasi na utendaji wako pia siasa zako. Wewe ni moja ya viongozi wachache wa kuigwa, Mungu akubariki na kukusimamia vyema ktk shughuri zako za ujenzi wa Taifa.
 
Prof. Tibaijuka, hongera saaaaana. Wewe ni kati ya wanawake wachache wanaotufanya wanawake tutembee kifua mbele. Kweli wanawake wanaweza na hawangoji kuwezeshwa. Umethubutu, umeweza na unasonga mbele.

Karibu JF mtandao mzuri kisima cha elimu na pia burudani kwani humu hakuishi vituko.

I tell you my dear, You will not regreat to be a member of JF.

love you mama.
Queen Esther
 
karibu mama,siipendi ccm,ila sina ubaya na mtu binafsi,na kuhusu wewe najua wewe ni mpenda demokrasia,karibu sana mama
 
Unafiki tu huo, unamkubali kwa lipi? Katika wizara zenye ukiritimba wa hali ya juu ni pamoja na hii wizara tangu enzi za Mwinyi na hata sasa. Ana lipi la kukubaliwa huyu mama? Watu hadi hivi sasa Tanzania hii wanakwenda kama headless chicken. wanajenga wanavyojisikia kwa sababu serikali haipimi viwanja na hata kwa wale waliojenga kiholela inatoa lessen za makazi bila kutengeneza barabara. Unakuta mitaa ina vichochoro vya kupita kwa miguu tu hakuna hata barabara angalau ya kupita mkokoteni achilia mbali gari la wagonjwa au zima moto na bado wizara ya ardhi inatoa lessen ya makazi maeneo kama haya.

Sasa hiyo tisa, kumi nenda kawaombe watu wa wizara waje wakupimie kiwanja ambacho umekinunua. Utakula jeuri yako. Kama huna fungu la kutosha hutakaa upimiwe, otherwise utaishia tu kuletewa masurveyors wa kuja kusoma GPS kwa gharama ya up to 200000. na Kazi iishie hapohapo. This is one of the most disorganized ministry in the country. Bado tukae chini kumpongeza? Kwa lipi?

Bado sijapata cha kunishawishi kumpongeza hata kidogo. Prof. Anna Tibaijuka ni failure Minister kama walivyoshindwa akina Chiligati na wengine wengi kuendesha hii wizara.


Nnakuunga mkono mkuu mia kwa mia,binafsi nina kiwanja Arusha ila suala la kupimiwa kiwanja na hawa watu wa ardhi ni tatizo linalowakumba wananchi wengi tusiotoa rushwa katika kununua haki zetu.
 
Last edited by a moderator:
Nadhani kama ni ukaribisho na maswali tayari vimeshafikia kiwango. Tusubiri sasa majibu. La sivyo tutaacha mgeni asite kukaa jukwaani. Asanteni kwa kunisamehe, maana si kwamba nawakataza kuendelea bali hebu tuvute subira kidogo.
 
Mama karibu sana, nikukumbushe mama kuwa hata Papa mstaafu Benedicto wa 16 siku ajiunga na mitandao ya jamii mtandao wa tweeter alisema kuwa Ameamua kuwa fuata wakristu waliko maana wengi wao siku hizi wametingwa na shughuli wanashinda ktk mitandao wanakosa muda wa kukutana na wachungaji akaamua kuwafuata huko.Hata wewe umeamua sawa mitandaoni kuna mengi mazuri ya kuvuna. mama tutashukuru kama utamshauri mama makinda pia atinge JF ni wazo tu.karibu
 
We mama mi huwa nakukubali sana

Radhia,
sidhani kama kuna kijana mwelewa asiyeweza kumkubali Mama Tibaijuka. Tatizo politics za nchi yetu zitam-polute mpaka aonekane hafai. Kaza uzi Mama. Nakukubali sana pia.

ANGALIZO: Wale wenye "majina ya nyumbani” waliovamia fukwe likiwemo jina la Rwakatare watakuharibia kazi.

Wako wengi mno na wamejenga kivamizi kwenye maeneo ambayo siyo sahihi kujenga kisheria. Hata wewe unajua ila pakuanzia panakusumbua.
 
Mama Tibaijuka zile nyumba zilizojengwa ufukweni mwa bahari na mkaagiza zivunjwe zimefikia wapi?Kama zitavunjwa fidia inalipwa na Serikali au sababu hao waliojenga ufukweni vibali vya kujenga mlivitoa ninyi Wizara ya ardhi.
 
Back
Top Bottom