Karibu sana mama,tuko pamoja sana umefanya jambo la maana sana kujiunga kwani tuko na mambo mengi ya kufahamu moja kwa moja kutoka kwako so welcome so much.
Mama Tibaijuka hii inatia moyo sana. Karibu sana kwani hii itasaidia kuwaonyesha wengine UMUHIMU WA MAWASILIANO YA KUPITIA HAPA JF ili ile issue ya kutaka JF ifungwe ionekane kuwa HIZO ZILIKUWA NI NDOTO ZA MAWAZO MABOVU.
Mama tunakuomba hata ukitukanwa hapabusije ukakimbia kwani jukwaa lina watu tofauti tofauti kama bungeni ilivyo kwa hiyo matusi wewe yaangalie tu na kuyaacha sisi tutaelewa.
Karibu
Kwa niaba ya Uongozi wa JamiiForums, nachukua fursa hii kukukaribisha ndani ya JamiiForums na kukushukuru kwa uamuzi wako huu wa kushiriki nasi katika mijadala anuai.
Aidha, nachukua fursa hii kuwakaribisha wengine ambao wangependa kushiriki kwa majina halisi wasisite kuwasiliana nasi ili tuweze kuwathibitisha (verify).
Hata hivyo, kila mmoja ataupokea ujio wako kwa mtazamo tofauti. Utakuwa binadamu wa ajabu sana ikiwa hutapingwa walau na asilimia 0.001 ya wanachama wetu. Wako wengi watakaopenda ujio na ushiriki wako lakini pia wako baadhi watakaotamani usingejiunga hapa. Sikiliza wito ndani yako uliokufanya wewe kujiunga na JF, kidhi kiu na wape haki walio wengi.
Naamini utaendelea kuvaa ngozi ngumu, utasimama imara na itakapobidi utachota uzoefu kutoka kwa wakongwe kama Dr.W.Slaa. Huyu ni miongoni mwa viongozi wanaoheshimika ambaye amekuwepo hapa JF na ameweza kuhimili mikikimikiki ya wadau
Mama nakunda na kukuheshim sana ila mama nijibu swali moja tu;
Umekaririwa na vyombo vya habari ukisema kuhusu jengo lililoanguka kuwa eneo hilo halikuwa na ruhusa wla uhalali wa kisheria kujengwa jengo la gorofa zaidi ya kumi; sasa wewe ukiwa mwenye mamlaka ya juu kumsaidia Rais katika swala la ardhi na mtoaji wa vibari vya ujenzi wewe mwenyewe au wafuasi wako unao waamini, imekuwaje jengo linajengwa kwa vibari vibavyoruhusu gorofa 16 bila ofisi yako tukufu au za watu wako kukataza?
Unasubiri kujibu nini kama mwenye mamlaka juu ya hilo? Hukujua wala watu wako hawakupitia miongozo wala sheria zinazo ongoza ujenzi katika eneo hilo?
Mama samahani lakini dhahili umekula pilau ndefu!!!
Prof. nimependa majibu yako. Yamejaa hekima ndani yake. Bilashaka ujio wako na mwendelezo wa majibu utakayo yataoa yatakuwa faraja kwa wengi hapa JF.
Swali la kichokozi: Nini hatima ya ushiriki wako kisiasa hasa ukiwa ndani ya chama chenye tuhuma nzito na zisizo na majibu/suluhisho miaka nenda miaka rudi?
Karibu sana Mama Anna Tibaijuka. Baada ya president Mkapa mama wewe nakupenda kwa moyo wangu wote. Tangu ukiwa UN Habitat nilikuwa na kufuatilia sana.
Nashukuru sasa naweza kuongea na wewe through this media. Asante kwa upendo wako kuja kukaa na sisi wanao. Pale tunapokuudhi naomba uwe tayari kuvumilia.
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.