Naomba tuwatangaze mashujaa wetu bila upendeleo wowote. Awe mwana siasa au mwananchi wa kawaida aliyefanya kazi nzuri kwa ajili ya kuleta maendeleo ya Nchi yetu. Aliyefichua uovu kwa faida ya chama na wananchi nk
Mimi naomba pasipo aibu wala ubinafsi nimtangaze Saa nane Umefanya kazi nzuri sana! uwe umetumwa au hapana lkn imenisaidia kujua mengi kuhusu siasa na imani yangu imezidi kuwa Imara. Kuna mambo mengi umesaidia yasiharibike kuliko ungekaa kimya. Katika hili wewe ni shujaa!
mwakyembe ndo shujaa wangu. Walimtegea sumu afe lakini jamaa baada ya kupona anazidi kupiga kazi bila woga. Viongozi wachache wenye kudhubutu namna hii.
Aiseee hapa bila kusitasita shujaa wangu wa mwaka 2012 ni kamanda, jemedari Ben Saanane kwani kawafichua masalia na kuwavungua nguo hadharani na hatimaye kukomesha uasi ndani ya chama.
Aiseee hapa bila kusitasita shujaa wangu wa mwaka 2012 ni kamanda, jemedari Ben Saanane kwani kawafichua masalia na kuwavungua nguo hadharani na hatimaye kukomesha uasi ndani ya chama.
Shujaa wangu ni Zitto Zuberi kabwe kwa kutoa muongozo wa swiss money,kuwa na msimamo lmara japo Ben Sanane na Dr.Slaa wanamchafua,ingawa alinichefua kujivuna uchawi hadharani.
nk
Dr. Wilbrod Peter Slaa. Amevumilia mengi waliyomzushia, anaendelea kuchapa kazi bila kukata tamaa. Naomba wote wenye moyo wa upendo tuendelee kumwombea mzee huyu kwa Mungu mwenyezi aendelee kumlinda ili azma yake ya kulikomboa taifa letu dhidi wezi wa mali asili zetu itimie.
Mimi mashujaa wangu wa hapa JF ni Yericko Nyerere , Ben Saanane na Exaud Mamuya hawa watu wamenifanya nigundue mambo mengi mpaka kufahamu dhumuni la ID ya TUNTEMEKE iliyotumika kuwatukana viongozi wa CDM.