Huyu ndiye shujaa wa Afrika aliyefahamika Kimataifa zaidi licha ya kuimba kwa lugha za kiasili

Jul 4, 2016
23
41
bonizacharia.bz@gmail.com.
Wamekuwepo wengi katika tasnia ya muziki hasa muziki wenye radha halisi ya kiafrika, na wamesaidia mengi katika kutangaza utamaduni wenye maadili ya kiafrika, lakini huyu! Hakika sio rahisi kusahaulika, huenda itachukuia muda mrefu kutoka katika vichwa vya watu wengi, masikio ya wapenzi wa aina hii ya muziki, kumbukumbu za vyombo vya habari na wandaaji wa matamasha ya muziki ndani ya Taifa la Zimbabwe, ndani ya Afrika nzima na hata nje ya Afrika kwa maana ya mataifa ya Ulimwengu. Sio mwingine bali ni Nguli wa muziki wenye radha halisi ya Kiafrika Oliver Tuku Mtukudzi. Basi! hata akisahaulika baada ya karne nyingi nina imani muziki wake kupitia nyimbo zake ndani ya Album Zaidi ya 67 utaendelea kuishi hasa kupitia ujumbe ulio ndani ya nyimbo hizo. "Tunapotokea huwezi kupata nafasi ya kuimba kama huna chochote cha kusema." ni msemo maarufu aliopenda sana kuutumia nguli huyu

Mnamo tarehe 23/01/2019 katika hospitali ya Avenues, iliyopo Jiji la Harare ambalo ni mji mkuu wa nchi ya Zimbabwe, kwa ghafla mno taa hiyo ya nuru ya muziki huo wenye radha adimu Afrika na ulimwenguni ilizima pasipo kutarajiwa mithili ya upepo mzito juu ya mshumaa unaotegemewa katikati ya giza nene, Islael mbele ya Mtukudzi bila kujali jitihada za madaktari, hisia njema za wanaotarajia kusikia habri njema za uponyaji wake alikamilisha kazi yake. Oooh! Jamani inasikitisha, inauma na ngumu kuelezeka Poleni wote mnaoendelea kuguswa mpaka leo.

Taifa la Zimbabwe na wananchi wake, mashabiki wake walio wengi katika kila kona ya ulimwengu walipokea taarifa hizi za majonzi na kwa masikitiko makubwa huku wengi wakishindwa kuzuia hisia zao za majonzi na kuhisi upweke wa ghafla mithili ya kinda wa njiwa pori jangwani aliyeachwa na mama yake kwa jiwe la mwindaji.

Katika hospitali hiyo Mtukudzi alikuwa akipatiwa matibabu ya maradhi ya KISUKARI aliyokuwa akiugua kwa muda mrefu hali iliyomlazimu kukatisha baadhi ya mialiko ya matamasha katika sehemu mbalimbali ulimwenguni
Hatimae shujaa huyo wa muziki wa kiafrika alizikwa kiheshima tarehe 27/01/2019 siku ya jumapili majira ya mchana katika makaburi ya kwao maeneo ya mashona land kijiji cha Madziwa nchini humo na Waziri wa wizara ya ulinzi akiwa ndo msomaji wa hotuba kwa niaba ya Raisi Emmerson Mnangagwa mbele ya maelfu na maelfu ya waombolezaji waliohudhuria tafrija hiyo ya kumuaga shujaa huyo.
TUUUU-.jpeg

MMMMM.jpeg

Kabla ya mazishi hayo mwili wake ulichukuliwa na jeshi la police siku ya ijumaa na kupelekwa kwenye uwanja wa Taifa wa mpira wa miguu mjini Harare ambapo sherehe za kumuaga zilifanyikia na baadae kuchukuliwa kwa helkopta na kumpelekwa nyumbani kijijini Madziwa kaskazini mwa mji wa Harare kwa ajili ya mazishi yaliyofanyika jumapili mchana kiheshima huku risasi kadhaa zikifyatuliwa hewani na askari jeshi kama ishara ya ushujaa.
“Alikuwa kijana mfano wa utambulisho wa taifa la Zimbabwe, mtu wa tabia ya unyenyekevu mwenye kuvutia sana na kujihusisha na njia ya upekee kupitia Tuku music.” Ni maneno yaliyonukuliwa kutoka kwa Rais wa Taifa hilo Emmerson Mnangagwa.
Licha ya kuwa mashujaa wa Taifa hilo huzikwa katika maeneo ya Majeshi ya Acre ila familia ya Mtukudzi iliomba Nguli huyo kuzikwa katika maeneo ya nyumbani alikozaliwa, hivyo serikali haikuwa na budi kukubali na kutekekeleza ombi hilo la familia.

KABLA YA KIFO CHAKE.
Oliver Tuku Mtukudzi mwana umahiri wa kucharaza gitaa aina ya solo na nguli wa radha halisi ya kiafrika alizaliwa usiku wa Septemba 22 mwaka 1952 katika mji wa Harare nchini Zimbabwe kwenye familia ya watoto sita. Akiwa na umri mdogo alianza kujihusisha na muziki wa kiutamaduni kama kupiga mbira na ngoma katika kabila la korekore/Shona na Ndembele, hatimae taratibu akaanza kufanikiwa kuwa na sauti pekee yenye radha ya muziki wa kiafrika zaidi.

Akiwa na umri miaka 25 mnamo mwaka 1977 harakati zake za muziki zilianza rasmi alipojiunga na kundi la nchini humo la Wagon wheels kundi ambalo walikuwemo wananmuziki wengine nguli kama Thomas Matfumona mpiga gitaa maarufu James Chimombe, lakini pia unaweza kuamini kuwa huenda uwezo mkubwa wa Mtukudzi katika kucharaza gitaa ulikuwa na kuongezeka Zaidi baada ya kukutana na Chimombe ndani ya kundi la Wagoni Wheels.
Ndani ya mwaka huo huo wa 1977 alifanikiwa kutoa wimbo wake wa kwanza uliofahamika kwa jina la Dzandimometera na baadae album yake ya kwanza ilifuata na hapo muziki wake ulianza kukua na kuwa muhimu katika kuelimisha uhuru katika jamii, siasa na kiuchumi.

Miaka miwili baadae Alianza kufanikiwa na kusimama peke yake kama muimbishaji (sololister) na hapo aliamua kuanzisha kundi lake la Black Sprit lililo saidia kuuza album yake iliyofanikiwa kuvunja rekodi kimauzo chini ya lebo yake ya TUKU MUSIC na hapo alianza kuona mafanikio kuelekea Taifa hilo la Zimbabwe kutangaza uhuru kutoka kwa wakoloni wareno mwaka 1980.

Baada ya kuwa amepata jina kimuziki Mtukudzi aliamua kuwa muigizaji wa filamu na hapo alianzia katika Makala ya video mbalimbali na kuendelea kutoa nyimbo hadi kufikia mwaka 1992, alipotunga wimbo wa Neria wenye historia ya kweli ambayo ni moja ya tukio lililotokea nchini humo kisha kutengenezewa filamu iliyoongozwa na muongozaji Godwin Mawuru kutoka mwaka 1993 na yeye akiwa ni miongoni mwa wahusika wakuu ndani ya filamu hiyo na akiwa ndo muhariri wa muziki ndani ya filamu hiyo na inapatikana kwenye mtandao wa Youtube katika lugha mbalimbali ya Kiingereza na Kiswahili na imetazamwa na watu Zaidi ya laki tatu na elfu arobaini na mbili mpaka sasa, Kupitia filamu hiyo inayoonesha ujumbe wa namna wanawake wa Kiafrika wanavyo kabiliwa na matatizo na wakati mgumu wanapofikwa na ujane.

nee.jpeg

“Jitihada na ushirikiano mkubwa wa Neria na mume wake Patrick wanajitengenezea maisha waliokuwa wakiyataka siku zote. Lakini Patrick anapofariki katika ajali ya gari, maisha ya Neria yanagueka ghafla na kuwa mateso. Wakati Neria anaomboleza kifo cha mume wake kijijini, shemeji yake, Phineas, yuko mjini akishughulika kumnyang’anya mali zake zote. Phineas anadai kuwa mila za Kiafrika zinampa haki ya kurithi mali zote za kaka yake marehemu. Neria anashuku lengo halisi la shemeji yake, lakini Phineas anapowateka watoto wake, ndipo Neria anaamua kumpiga vita.” Hii ni sehemu ya ujumbe katika filamu hiyo.

Filamu hii imegusa watu wengi kwa namna inavyoakisi maisha ya mwanamke wa kiafrika chini ya mila na desturi kandamizi kwa wanawake na kupitia wimbo huo wa Neria imeshinda tuzo nyingi za kimataifa kama vile tuzo ya MNET Afrika kusini, tuzo za nchini misri za OAU na Filamu bora ya mwaka.
Na huenda kutumika kwa nyimbo za nguli huyo Oriva mtukudzi zilizo kuwa na ujumbe mzuri kwa jamii kimaadili umesaidia katika muunganiko mzuri wa visa ndani ya jamii nyingi za kiafrika.

Mwaka 1994 Mtukudzi na kundilake la Black Sprit walitumia Zaidi ya wiki nne kufanya matamasha ambayo huenda ndo yalikuwa matamasha ya kwanza makubwa kwa mwaka huo nje ya nchi katika mataifa ya Autria na Swetzland na baadae wakaungana na nguli wa muziki wa Reggae Luck Dube na kufanya tamasha la pamoja nchini Afrika Kusini na baadae kundi hilo la Black Sprit liliendelea nchini Holland, Marekani, San Francisco na nyumbani nchini Zimbabwe ikiwa ni ndani ya kati ymiaka ya 1998 na 2000. Ni hakika kuwa Kupitia album yake ya Paiveto waliyoizindua baada ya ziara hiyo ilizidi kuwapa umaarufu hasa baada ya kushika chati za juu.

Oliver Tuku Mtukudzi amefanikiwa kuimba dozen na dozen ya nyimbo nyingi ambazo zimempa tuzo ndani ya Zimbabwe na nje ya Zimbabwe ambazo ziliigusa moja kwa moja jamii ya Zimbabwe na Afrika, mila desturi na utamaduni, maadili ya kiafrika, siasa na hata mapambano katika maendeleo ya kiuchumi, walioguswa na mashairi ya nyimbo zake sio tu kumtazama kwa jicho la kwanini bali hata kutamani asiimbe tena.

poo.jpeg

Mfano mzuri ni wimbo wa Wasakara aliouimba mwaka 2001 kwa lugha ya kidembele na kishona ukiwa na maana ya “You have gotten too old” yaani umri wako umeenda, wimbo huo ulipigwa marufuku kwa kile kilichotafsiriwa kuwa ulikua ukimlenga Rais wa Taifa hilo la Zimbabwe Robert Mugabe toka uhuru wake mwaka 1980, Ambae baadae mnamo mwaka 2018 aliondoloewa madarakni kwa nguvu akiwa na umri wa miaka 93.

Wimbo wa Tozeza Baba kwa lugha ya kishona ukiwa na maan aya tunaogopa Baba, ndani akimaanisha mwanaume mlevi anayepigwa na mke wake na kuulenga moja kwa moja unyanyasaji, lakini baadhi ya mashairi ndani ya wimbo huo uliwagusa wale wanasiasa ambao huwachukiza walio dhaifu na wenye mazingira magumu.

HHHH.jpeg

Todii ni wimbo aliouimba akigusia ugonjwa wa ukimwi/VVU. Anaonekana kulaumu vifo vinavyosababiswa na virusi hivyo vya ugonjwa huo, Wimbo huo ulipata kukubalika Zaidi na kupata kibali cha UNICEF kutumika kwenye kampeni mbalimbali na mikusanyiko nchini Zimbabwe na nje ya nchi dhidi ya VVU. Unapatikana kwa lugha ya Kireno, Ndebele na Kiingereza.

Nyimbo nyingine zilizobamba zaidi ni kama vile Ndima ndapedza, Rirongere, Andinzwi, Dzoka Uyamwe, Hear me lord, Wake up, Cheka ukama, Neria, Chirimundari, Ngoromera, Tozeza Baba, Kunze, Todi, Mabasa, Zimero, Mutserendende na nyingine nyingi mno ambazo zimemsaidia kumpa tuzo mbalimbali huku akiwa ameshirikiana na wakali wengine kutoka ndani na nje ya Taifa hilo kama vile Ringo Madlingozi (South Africa) ft. Oliver Mtukudzi kwenye wimbo unaitwa Into Yami (2006), Winky D ft. Oliver Mtukudzi kwenye wimbo Panorwadza Moyo’ (2016), Hugh Masekela (South Africa) ft. Oliver Mtukudzi kwenye wimbo unaitwa Tapera (2017), Tocky Vibes ft. Oliver Mtukudzi wimbo ‘Usambotya’ (2018).

Kutoka nchini Tanzania ameshirikiana na msanii Jide, Lady Jay Dee mkongwe mwenye radha halisi ya bongo fleva wimbo unaoitwa mimi ni mimi jay dee aliimba kwa Kiswahili na kiingereza nae Olivier akiimba kwa lugha ya kishona na kiingereza wimbo ulitoka mwaka 2013.

JIDE.jpeg

Ng’ombe hazeeki maini bwana kwani mpaka miaka ya hivi karibuni mtukudzi aliendelea kuachia hit! alishirikiana na kundi la Ladysmith Black Mambazo mwaka 2016 walitoa wimbo wa Hello My Baby na ikawa hit song, mwaka 2017 nako akaachia hit nyingine na video nzuri kwa jina Haasat Aziva na huenda pia Wimbo wa NERIA waliourudia yeye na kundi la LadySmith Mambazo uliotoka mwezi wa tisa 2018 huenda ilikuwa ni kazi ya mwisho kabla ya kufikwa na umauti Januari 2019.

Wimbo huo wa neria waliuimba kwa mpangilio wa sauti wenye utofauti kidogo na ule wa mwanzo lakini wenye kuvutia Zaidi na kutazamwa na watu Zaidi laki nne kufikia Januari 28,2019.

Oliver na kundi lake la Black Sprit wamefanikiwa kupanda katika majukwaa mbalimbali makubwa ndani na nje wakifanya ziara ya muziki wao na matamasha yaliyozidi kuwapa umaarufu ulimwenguni na kuzidi kuwapa nafasi kupenyeza radha ya muziki wao mbali Zaidi. Haya ni baadhi tu ambayo huenda sio rahisi kusahaulika.

Mwaka 2012 may, jukwaa la San Francisco kusini mwa Califionia na August 2013 katika jukwaa la viwanja vya Shibuya ndani ya mji wa Tokyo nchini Japani, akiwa na kundi lake walionekana kukonga nyoyo za watu waliotafsiri furaha kupitia nyuso zao ambao walionekana katika mchanganyiko wa wazungu na waafrika waishio nje ya nchi, hali kadhalika nchini china mnamo Novemba mwaka 2016.

Mataifa mengine ni kama Afrika kusini, Australia, Italy, Uingereza, Ujeruamani na ziara mbalimbali za muziki wake katika vituo vikubwa vya kurusha matangazo kama vile radio ujerumani ya Voice of Africa (VOA), Shirika la BBC na studio za KEXP Washington DC kipindi kinachowahoji wasanii wakubwa Duniani na hupewa nafasi ya kutumbuiza mbashara nyimbo zao na mwaka 2011 alifanikiwa pia kufika katika kituo cha Clouds MEDIA nchini Tanzania na kukutana na mkurugenzi mkuu wa kituo hicho Joseph Kusaga na kubadilishana mawazo.

jose.jpeg

Nafasi adimu ya mwaka 2016 mwezi sita, alipata fursa ya kutumbuiza kwenye tamasha la tribal meats nchini Zimbabwe mbele ya Rais wa Taifa hilo na viongozi wengine wa serikali. Oliver na kundi lake waliimba nyimbo zao kadhaa na kutoa burudani yenye radha halisi ya Afrika, Upigaji wake wa gitaa na ala zingine za muziki zilitafasri taswira yote ya utamaduni pendwa.

Macho, masikio na nyuso za watu, viongozi wa serikali na wapenda burudani waliokusanyika na kuzingira jukwaa hilo ziliashiria kuridhika vyema kabisa na uzuri wa sauti na midundo iliyocharazwa vyema na kundi la Black Sprit chini ya Lebo ya Tuku music na kuwafanya baadhi ya viongozi mbalimbali wa taifa hilo kushindwa kumudu hisia zao hasa pale walipojikuta wakianza kutumia vyema viungo vyao vya mwili kufaidi uzuri na utamu wa muziki huo halisi.

TUZO
Toka Oliver Tutu Mtukudzi alipoanza kufahamika ndani na nje ya Taifa la Zimbabwe kupitia nyimbo zake na uigizaji amepata mafanikio makubwa hasa katika kupokea tuzo mbalimbali karibia kila mwaka au baada ya miaka kadhaa.

Mwaka 1985-1988 alipewa tuzo ya msanii mwenye mauzo bora ndani ya Taifa la Zimbabwe kupitia albamu zake za awali kama Hwena Handirase, Ndipeiwo Zano na Zvauya Sei? na mwaka 2002 kupitia tuzo za KORA AWARDS alipokea tuzo ya mpangilio bora wa wimbo kupitia wimbo wa Ndakuvara, wimbo huo aliuimba kwa lugha ya kishona/kidembele ukiwa na maana ya nimeumia au nimekuwa naumia.

Wimbo ulioonekana kuwa na maudhui ya kumtegemea mtu anayekujali kwa karibu “Seza mya mwana Ndakuvara”, Kama kumsifia mwanamke au Mama watoto na mwaka huo huo 2002 alipokea tuzo za SAMA kipengele cha wimbo bora wa kiutamaduni katika tamadaduni za Zimbabwe na tuzo za NAMA yaani National Artist Merits Awards.

Hii ilikuwa ni Tuzo yake ya kwanza na ya pekee na yenye heshima ya mwaka 2003 alipotunukiwa tuzo ya Shahada ya Heshima yaani Honorary Degree kutoka chuo kikuu cha Zimbabwe ilikuwa ni Disemba ya waka 2003, lakini wasemavyo wahenga mwenye nacho huongezewa basi kupitia tuzo za NAMA, alipokea tena tuzo ya kundi bora la mwaka Black Sprit chini ya TUKU MUSIC na tena tuzo ya mwimbishaji bora wa mwaka yaani best male vocalist.

Hakuna kulala kama wasemavyo waleo au Zege halilali bidii zikamfikisha mwaka 2005 na kuteuliwa kwenye tuzo za NAMA kipengele cha mwimbaji bora wa taifa na akashinda, mwaka 2006 akachukua tena tuzo ya Album bora iliyovuka mipaka ya Taifa hilo album ya NHAWA yenye nyimbo 8 kama vile Menza Kudzimba, Rudo Handina, Tiregerereiwo, Handiro Dambudziko, Tiri Mubindu, Dzokai, Tozeza baba, Dzidziso zote kwa lugha ya album hiyo ilionekana kuuza sana kutokana na kupendwa kwa nyimbo kama Handiro, Tozeza baba na Dzokai.

Na mwaka huo huo 2006 alipokea tuzo ya wimbo bora wa mwaka kupitia wimbo wa Handiro na kupewa ubalozi wa muziki wa Zimbabwe kwa sababu alionekana Zaidi kuubeba muziki wa Zimbabwe, Laahaula! Wakisema moja mbili huongezwa ubalozi haukuishia kwani mwaka 2007 baada ya kupewa tuzo ya mwimbaji bora Shirika la Utalii lilimpa tena ubalozi wa utalii chini humo.

oliver-Mtukdzi-2-1500x1200.jpg

Tena na tena ikafikia mwaka 2009 huduma ya muziki wake ikazidi kuwagusa wengi, Chuo cha wanawake cha Afrika kikampa tuzo ya heshima ya Sanaa bora na tuzo za M-NET Awards wakampa tuzo ya sauti bora ya wimbo wa Neria wa mwaka 1992.
Mwaka 2010 kutoka Chuo kikuu cha Zimbabwe na Baraza la kimataifa la wanawake wa Afrika kikampa tuzo kwa kutambua jukumu na mchango wake wa kuangaza na kuimarisha usawa wa wanawake Afrika kupitia kazi zake kisanii, na Serikali ya Italia ilimpa tuzo ya heshima katika tuzo za Merit Award kwa kutambua kazi zake kama msanii wa kimataifa mwaka 2011.

Kutokana na tuzo ya shahada ya heshima ya mwaka 2003 kutoka chuo kikuu cha Zimbabwe kwa mara nyingine mwaka 2014 Chuo hicho kilimpa tuzo kubwa Zaidi PHD ya heshima ya taasisi za kimataifa ya ushauri na Daktari wa falfasa.

Kwa hayo mengi, makubwa, mazuri na yenye mchango katika kuleta usawa wa kijinsia katika jamii, kukuza na kutangaza utamaduni wa Afrika, kuhamasisha maendeleo ya kisiasa na kiuchumi ni hakika kuwa nguli huyo ataendelea kukumbukwa Zaidi karne na karne.
Oliver Alifariki akiwa na watoto watano amabo ni Sam Mtukudzi nae alikuwa mwanamuziki aliyejaribu kufuata nyayo za baba yake na nyimbo kama Zvakanaka, Amai, Famba nk lakini alifariki mwaka 1998 kwa ajali ya gari.
Wengine ni Selmor, Jesca, Sandra na na wajukuu wawili Pia binti yake Selmor nae ni mwanamuziki.
NNN.jpeg

Kila lenye mwanzo halikosi kuwa na mwisho walisema wahenga sio mimi! Basi huo ndo ukawa mwisho wake na yote aliyoyafanya enzi za uhai wake, tunamtakia kila la kheri huko aliko na aendelee kupumzika kwa Amani.
He died because his body had served its purpose. His soul had done what it come to do, learned what came to learn, and then was free to leave

Boniphace Zacharia

View attachment 1186561

View attachment 1186572

View attachment 1186574

View attachment 1186576

Mfano mzuri ni wimbo wa Wasakara aliouimba mwaka 2001 kwa lugha ya kidembele na kishona ukiwa na maana ya “You have gotten too old” yaani umri wako umeenda, wimbo huo ulipigwa marufuku kwa kile kilichotafsiriwa kuwa ulikua ukimlenga Rais wa Taifa hilo la Zimbabwe Robert Mugabe toka uhuru wake mwaka 1980, Ambae baadae mnamo mwaka 2018 aliondoloewa madarakni kwa nguvu akiwa na umri wa miaka 93.

Wimbo wa Tozeza Baba kwa lugha ya kishona ukiwa na maan aya tunaogopa Baba, ndani akimaanisha mwanaume mlevi anayepigwa na mke wake na kuulenga moja kwa moja unyanyasaji, lakini baadhi ya mashairi ndani ya wimbo huo uliwagusa wale wanasiasa ambao huwachukiza walio dhaifu na wenye mazingira magumu.

View attachment 1186577

Todii ni wimbo aliouimba akigusia ugonjwa wa ukimwi/VVU. Anaonekana kulaumu vifo vinavyosababiswa na virusi hivyo vya ugonjwa huo, Wimbo huo ulipata kukubalika Zaidi na kupata kibali cha UNICEF kutumika kwenye kampeni mbalimbali na mikusanyiko nchini Zimbabwe na nje ya nchi dhidi ya VVU. Unapatikana kwa lugha ya Kireno, Ndebele na Kiingereza.

Nyimbo nyingine zilizobamba zaidi ni kama vile Ndima ndapedza, Rirongere, Andinzwi, Dzoka Uyamwe, Hear me lord, Wake up, Cheka ukama, Neria, Chirimundari, Ngoromera, Tozeza Baba, Kunze, Todi, Mabasa, Zimero, Mutserendende na nyingine nyingi mno ambazo zimemsaidia kumpa tuzo mbalimbali huku akiwa ameshirikiana na wakali wengine kutoka ndani na nje ya Taifa hilo kama vile Ringo Madlingozi (South Africa) ft. Oliver Mtukudzi kwenye wimbo unaitwa Into Yami (2006), Winky D ft. Oliver Mtukudzi kwenye wimbo Panorwadza Moyo’ (2016), Hugh Masekela (South Africa) ft. Oliver Mtukudzi kwenye wimbo unaitwa Tapera (2017), Tocky Vibes ft. Oliver Mtukudzi wimbo ‘Usambotya’ (2018).

Kutoka nchini Tanzania ameshirikiana na msanii Jide, Lady Jay Dee mkongwe mwenye radha halisi ya bongo fleva wimbo unaoitwa mimi ni mimi jay dee aliimba kwa Kiswahili na kiingereza nae Olivier akiimba kwa lugha ya kishona na kiingereza wimbo ulitoka mwaka 2013.

View attachment 1186579

Ng’ombe hazeeki maini bwana kwani mpaka miaka ya hivi karibuni mtukudzi aliendelea kuachia hit! alishirikiana na kundi la Ladysmith Black Mambazo mwaka 2016 walitoa wimbo wa Hello My Baby na ikawa hit song, mwaka 2017 nako akaachia hit nyingine na video nzuri kwa jina Haasat Aziva na huenda pia Wimbo wa NERIA waliourudia yeye na kundi la LadySmith Mambazo uliotoka mwezi wa tisa 2018 huenda ilikuwa ni kazi ya mwisho kabla ya kufikwa na umauti Januari 2019.

Wimbo huo wa neria waliuimba kwa mpangilio wa sauti wenye utofauti kidogo na ule wa mwanzo lakini wenye kuvutia Zaidi na kutazamwa na watu Zaidi laki nne kufikia Januari 28,2019.

Oliver na kundi lake la Black Sprit wamefanikiwa kupanda katika majukwaa mbalimbali makubwa ndani na nje wakifanya ziara ya muziki wao na matamasha yaliyozidi kuwapa umaarufu ulimwenguni na kuzidi kuwapa nafasi kupenyeza radha ya muziki wao mbali Zaidi. Haya ni baadhi tu ambayo huenda sio rahisi kusahaulika.

Mwaka 2012 may, jukwaa la San Francisco kusini mwa Califionia na August 2013 katika jukwaa la viwanja vya Shibuya ndani ya mji wa Tokyo nchini Japani, akiwa na kundi lake walionekana kukonga nyoyo za watu waliotafsiri furaha kupitia nyuso zao ambao walionekana katika mchanganyiko wa wazungu na waafrika waishio nje ya nchi, hali kadhalika nchini china mnamo Novemba mwaka 2016.

Mataifa mengine ni kama Afrika kusini, Australia, Italy, Uingereza, Ujeruamani na ziara mbalimbali za muziki wake katika vituo vikubwa vya kurusha matangazo kama vile radio ujerumani ya Voice of Africa (VOA), Shirika la BBC na studio za KEXP Washington DC kipindi kinachowahoji wasanii wakubwa Duniani na hupewa nafasi ya kutumbuiza mbashara nyimbo zao na mwaka 2011 alifanikiwa pia kufika katika kituo cha Clouds MEDIA nchini Tanzania na kukutana na mkurugenzi mkuu wa kituo hicho Joseph Kusaga na kubadilishana mawazo.

View attachment 1186581

Nafasi adimu ya mwaka 2016 mwezi sita, alipata fursa ya kutumbuiza kwenye tamasha la tribal meats nchini Zimbabwe mbele ya Rais wa Taifa hilo na viongozi wengine wa serikali. Oliver na kundi lake waliimba nyimbo zao kadhaa na kutoa burudani yenye radha halisi ya Afrika, Upigaji wake wa gitaa na ala zingine za muziki zilitafasri taswira yote ya utamaduni pendwa.

Macho, masikio na nyuso za watu, viongozi wa serikali na wapenda burudani waliokusanyika na kuzingira jukwaa hilo ziliashiria kuridhika vyema kabisa na uzuri wa sauti na midundo iliyocharazwa vyema na kundi la Black Sprit chini ya Lebo ya Tuku music na kuwafanya baadhi ya viongozi mbalimbali wa taifa hilo kushindwa kumudu hisia zao hasa pale walipojikuta wakianza kutumia vyema viungo vyao vya mwili kufaidi uzuri na utamu wa muziki huo halisi.

TUZO
Toka Oliver Tutu Mtukudzi alipoanza kufahamika ndani na nje ya Taifa la Zimbabwe kupitia nyimbo zake na uigizaji amepata mafanikio makubwa hasa katika kupokea tuzo mbalimbali karibia kila mwaka au baada ya miaka kadhaa.

Mwaka 1985-1988 alipewa tuzo ya msanii mwenye mauzo bora ndani ya Taifa la Zimbabwe kupitia albamu zake za awali kama Hwena Handirase, Ndipeiwo Zano na Zvauya Sei? na mwaka 2002 kupitia tuzo za KORA AWARDS alipokea tuzo ya mpangilio bora wa wimbo kupitia wimbo wa Ndakuvara, wimbo huo aliuimba kwa lugha ya kishona/kidembele ukiwa na maana ya nimeumia au nimekuwa naumia.

Wimbo ulioonekana kuwa na maudhui ya kumtegemea mtu anayekujali kwa karibu “Seza mya mwana Ndakuvara”, Kama kumsifia mwanamke au Mama watoto na mwaka huo huo 2002 alipokea tuzo za SAMA kipengele cha wimbo bora wa kiutamaduni katika tamadaduni za Zimbabwe na tuzo za NAMA yaani National Artist Merits Awards.

Hii ilikuwa ni Tuzo yake ya kwanza na ya pekee na yenye heshima ya mwaka 2003 alipotunukiwa tuzo ya Shahada ya Heshima yaani Honorary Degree kutoka chuo kikuu cha Zimbabwe ilikuwa ni Disemba ya waka 2003, lakini wasemavyo wahenga mwenye nacho huongezewa basi kupitia tuzo za NAMA, alipokea tena tuzo ya kundi bora la mwaka Black Sprit chini ya TUKU MUSIC na tena tuzo ya mwimbishaji bora wa mwaka yaani best male vocalist.

Hakuna kulala kama wasemavyo waleo au Zege halilali bidii zikamfikisha mwaka 2005 na kuteuliwa kwenye tuzo za NAMA kipengele cha mwimbaji bora wa taifa na akashinda, mwaka 2006 akachukua tena tuzo ya Album bora iliyovuka mipaka ya Taifa hilo album ya NHAWA yenye nyimbo 8 kama vile Menza Kudzimba, Rudo Handina, Tiregerereiwo, Handiro Dambudziko, Tiri Mubindu, Dzokai, Tozeza baba, Dzidziso zote kwa lugha ya album hiyo ilionekana kuuza sana kutokana na kupendwa kwa nyimbo kama Handiro, Tozeza baba na Dzokai.

Na mwaka huo huo 2006 alipokea tuzo ya wimbo bora wa mwaka kupitia wimbo wa Handiro na kupewa ubalozi wa muziki wa Zimbabwe kwa sababu alionekana Zaidi kuubeba muziki wa Zimbabwe, Laahaula! Wakisema moja mbili huongezwa ubalozi haukuishia kwani mwaka 2007 baada ya kupewa tuzo ya mwimbaji bora Shirika la Utalii lilimpa tena ubalozi wa utalii chini humo.

View attachment 1186584

Tena na tena ikafikia mwaka 2009 huduma ya muziki wake ikazidi kuwagusa wengi, Chuo cha wanawake cha Afrika kikampa tuzo ya heshima ya Sanaa bora na tuzo za M-NET Awards wakampa tuzo ya sauti bora ya wimbo wa Neria wa mwaka 1992.
Mwaka 2010 kutoka Chuo kikuu cha Zimbabwe na Baraza la kimataifa la wanawake wa Afrika kikampa tuzo kwa kutambua jukumu na mchango wake wa kuangaza na kuimarisha usawa wa wanawake Afrika kupitia kazi zake kisanii, na Serikali ya Italia ilimpa tuzo ya heshima katika tuzo za Merit Award kwa kutambua kazi zake kama msanii wa kimataifa mwaka 2011.

Kutokana na tuzo ya shahada ya heshima ya mwaka 2003 kutoka chuo kikuu cha Zimbabwe kwa mara nyingine mwaka 2014 Chuo hicho kilimpa tuzo kubwa Zaidi PHD ya heshima ya taasisi za kimataifa ya ushauri na Daktari wa falfasa.

Kwa hayo mengi, makubwa, mazuri na yenye mchango katika kuleta usawa wa kijinsia katika jamii, kukuza na kutangaza utamaduni wa Afrika, kuhamasisha maendeleo ya kisiasa na kiuchumi ni hakika kuwa nguli huyo ataendelea kukumbukwa Zaidi karne na karne.
Oliver Alifariki akiwa na watoto watano amabo ni Sam Mtukudzi nae alikuwa mwanamuziki aliyejaribu kufuata nyayo za baba yake na nyimbo kama Zvakanaka, Amai, Famba nk lakini alifariki mwaka 1998 kwa ajali ya gari.
Wengine ni Selmor, Jesca, Sandra na na wajukuu wawili Pia binti yake Selmor nae ni mwanamuziki.
View attachment 1186585

Kila lenye mwanzo halikosi kuwa na mwisho walisema wahenga sio mimi! Basi huo ndo ukawa mwisho wake na yote aliyoyafanya enzi za uhai wake, tunamtakia kila la kheri huko aliko na aendelee kupumzika kwa Amani.
He died because his body had served its purpose. His soul had done what it come to do, learned what came to learn, and then was free to leave

Boniphace Zacharia
bonizacharia.bz@gmail.com.

Hongera kwa kazi na bandiko murua
 
Back
Top Bottom